Yanga na Simba Jiondoeni Kwenye Minyororo ya Wafadhili kwa Kutumia Mkakati Huu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yanga na Simba Jiondoeni Kwenye Minyororo ya Wafadhili kwa Kutumia Mkakati Huu

Discussion in 'Sports' started by Sabi Sanda, Feb 22, 2011.

 1. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #1
  Feb 22, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Naamini kila Mtanzania anajua na kutambua ukweli kuwa timu zetu za Simba na Yanga ndiyo timu zilizo na wapenzi, washabiki na wanachama wengi hapa nchini. Makisio yangu ni kuwa kati ya Watanzania milioni 45, timu hizi kila moja ina wapenzi na mashabiki wasiopungua milioni 12.

  Kutokana na nguvu hii kubwa ya Watanzania walio nyuma yao inapendekezwa kila timu ianzishe Mfuko wake wa AKIBA NA UWEKEZAJI. Kwa upande wa Simba Mfuko wake wa Akiba na Uwekezaji unapendekezwa uitwe SIMBA SAVING AND INVESTMENT FUND (SISIF) na kwa upande wa timu ya Yanga, Mfuko wake unapendekezwa uitwe YANGA SAYING AND INVESTMENT FUND (YASIF).

  Mifuko hii yote inapendekezwa iwe na mfumo kama wa Umoja Fund, mfuko ambao unasimamiwa na kuendeshwa na UNIT TRUST OF TANZANIA.

  Ili Mifuko hii inayopendekezwa iweze kuwa na fedha za kutosha ili kuweza kutimiza malengo yake, yafuatayo yanapendekezwa:-

  1. Bei ya Kipande Kimoja cha Mfuko husika inapendekezwa iwe shilingi elfu moja tu na kila MwanaSimba au MwanaYanga anunue angalau wastani wa Vipande Vitano Kila Wiki.

  2. Juhudi za dhati na za kudumu pamoja na Kampeni ya kudumu nchi nzima ifanyike ili kuhakikisha kuwa kila Mfuko unakuwa na wanunuzi wa vipande vya Mfuko wasiopungua milioni 3 kila mwaka ambapo kila mmoja kwa mwaka atanunua angalau vipande 260.

  Iwapo hayo yatafanyika na kutekelezwa kwa ukamilifu wake, kwa mwaka mmoja tu kila Mfuko utakuwa unakusanya akiba isiyopungua shilingi bilioni 780. Kwa mfano fedha hizi zikiwekezwa katika Dhamana za Serikali, kila Mfuko utakuwa unapata faida ya angalau shilingi bilioni 81 kila mwaka.
   
 2. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #2
  Feb 23, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kimsingi ni aibu kubwa kwa timu zetu hizi kutokuwa zikijitegemea. Viongozi wetu wakiamua ni rahisi sana kwa Simba na Yanga kuwa timu zenye uwezo mkubwa wa fedha na kuweza kujiendesha bila tatizo na kuwa na uwezo wa kuwalipa wachezaji wake angalau mshahara usiopungua shilingi milioni moja kwa wiki kwa kila mchezaji.
   
Loading...