Yanga na Man United kama wanafanana raundi ya pili ya Msimu wa 2020/2021

Ladder 49

JF-Expert Member
Dec 19, 2017
7,416
18,856
Wakuu Habari zenu bila shaka utakubaliana na mimi hizi timu kuanzia raundi ya pili ianze zimekuwa zinashindwa kuondoka na point 3, zinaishia kuchukua point 1 moja. Kuchukua point 3 labda refa awasaidie timu pinzani iwe pungufu bila hivyo hiyo mechi ni uhakika sare hiyo.

Yanga na Man U zitaendelea kupata sare raundi ya pili na kufungwa.

Ushindi wa moja bila kwa yanga kwenye karibia kila Mechi kwenye raundi ya kwanza unatosha kutoa picha raundi ya pili itakuwaje na ndio kinachotokea sasa hivi.

Kwa ushindi wa kubahatisha wa goli moja raundi ya kwanza kwenye ligi, hawana huwezo wa kushinda mechi zaidi ya sare maana kikawaida raundi ya 2 inakuwa ni ngumu sana kushinda ya kwanza kila timu inaitaji point kubaki kwenye ligi, kama ushindi wako ulikuwa wa ujanja ujanja kwenye raundi ya kwanza kupata ushindi raundi ya pili ni ngumu sana na ndio tunachokiona kwa yanga na kwa Man U, sare zimetawala.

Inavyoonekana Yanga hawana mabadiliko yoyote ya kiufundi timu inacheza vile tu kama ilivyokuwa raundi ya kwanza. Sasa tutegemee sare kwa kwenda mbele.

timu inashindwa kufunga magoli mengi raundi ya kwanza, raundi ya pili magoli lazima yapungue tu hakuna duniani timu inayofunga magoli mengi raundi ya pili kuzidi raundi ya kwanza. Hata hao wafungaji bora hawajawahi kufanya hivyo.

Kwa upande wa Man U, hawa jamaa ushindi wao wa comeback karibia kila mechi kwenye raundi ya kwanza kwenye ligi,ulikuwa na ulakini na ulikuwa unatoa picha kwamba wanafungika sasa raundi ya pili yeye na yanga wanashindwa kufanya comeback wanatanguliwa kufungwa wanarudisha mechi inaisha sare washabiki wakiwa wanajifariji eti sisi wazee wa comeback, wamebaki na mawazo mgando hii ni raundi ya pili point zinaitajika sana kushinda raundi ya kwanza. Timu zingine zikipata goli linazuiwa vizuri na na kwakuwa mnafungika wataendelea kufunga magoli hata kama mkirudisha,mwisho wa siku sare muda ujatosha tena kurudisha.

Sasa nachokiona Kwa yanga na Man U sare zao wote wanakuwa wanasawazisha wao kwa sasa na muda unakuwa hautoshi kwao sio kama kwenye raundi ya kwanza.

Yanga na Man U wanavyoendelea kupata sare ndio wanastahili hizo sare kutokana na mzunguko wa raundi ya kwanza walishinda kwa kubahatisha tu na huo ndio ukweli, ndio maana raundi ya pili inakuwa shida kupata point 3, ni suala la muda tu ndio mashabiki wa yanga na Man U ndio mtanielewa nilicho maanisha. Kwa sasa mtanibishia mwisho wa siku mtakubaliana na mimi.

Mashabiki wa yanga na Man U jiandaeni kushangilia sare. Sijaona utofauti kwenye matokeo ya hizo timu kwa sasa kwenye ligi zao huko.

Ni hayo tu wakuu.
 
Man utd hata top four anaweza asiione mwaka huu

Kwa mwendo huu utd hachomoki hizi game

Vs man city

Vs chelsea

Vs liverpool

Vs lecister city
 
VP Liverpool mkuu nayo unaizungumziaje
Hawa walitumia nguvu kubwa kuiaminisha dunia kwamba wao ni wataalamu. Anyways nisiongee sana kifupi nguvu za soda kwa Liverpool zimefikia Omega. Wapo kwenye point of diminishing return.
 
Sare zitaendelea kuiandama yanga kama vile kwenye ushindi wa moja bila ulivyowaandama. Sasa ni mwendo wa kushangilia sare tu.
 
Wakuu Habari zenu bila shaka utakubaliana na mimi hizi timu kuanzia raundi ya pili ianze zimekuwa zinashindwa kuondoka na point 3, zinaishia kuchukua point 1 moja. Kuchukua point 3 labda refa awasaidie timu pinzani iwe pungufu bila hivyo hiyo mechi ni uhakika sare hiyo.

Yanga na Man U zitaendelea kupata sare raundi ya pili na kufungwa.

Ushindi wa moja bila kwa yanga kwenye karibia kila Mechi kwenye raundi ya kwanza unatosha kutoa picha raundi ya pili itakuwaje na ndio kinachotokea sasa hivi.

Kwa ushindi wa kubahatisha wa goli moja raundi ya kwanza kwenye ligi, hawana huwezo wa kushinda mechi zaidi ya sare maana kikawaida raundi ya 2 inakuwa ni ngumu sana kushinda ya kwanza kila timu inaitaji point kubaki kwenye ligi, kama ushindi wako ulikuwa wa ujanja ujanja kwenye raundi ya kwanza kupata ushindi raundi ya pili ni ngumu sana na ndio tunachokiona kwa yanga na kwa Man U, sare zimetawala.

Inavyoonekana Yanga hawana mabadiliko yoyote ya kiufundi timu inacheza vile tu kama ilivyokuwa raundi ya kwanza. Sasa tutegemee sare kwa kwenda mbele.

timu inashindwa kufunga magoli mengi raundi ya kwanza, raundi ya pili magoli lazima yapungue tu hakuna duniani timu inayofunga magoli mengi raundi ya pili kuzidi raundi ya kwanza. Hata hao wafungaji bora hawajawahi kufanya hivyo.

Kwa upande wa Man U, hawa jamaa ushindi wao wa comeback karibia kila mechi kwenye raundi ya kwanza kwenye ligi,ulikuwa na ulakini na ulikuwa unatoa picha kwamba wanafungika sasa raundi ya pili yeye na yanga wanashindwa kufanya comeback wanatanguliwa kufungwa wanarudisha mechi inaisha sare washabiki wakiwa wanajifariji eti sisi wazee wa comeback, wamebaki na mawazo mgando hii ni raundi ya pili point zinaitajika sana kushinda raundi ya kwanza. Timu zingine zikipata goli linazuiwa vizuri na na kwakuwa mnafungika wataendelea kufunga magoli hata kama mkirudisha,mwisho wa siku sare muda ujatosha tena kurudisha.

Sasa nachokiona Kwa yanga na Man U sare zao wote wanakuwa wanasawazisha wao kwa sasa na muda unakuwa hautoshi kwao sio kama kwenye raundi ya kwanza.

Yanga na Man U wanavyoendelea kupata sare ndio wanastahili hizo sare kutokana na mzunguko wa raundi ya kwanza walishinda kwa kubahatisha tu na huo ndio ukweli, ndio maana raundi ya pili inakuwa shida kupata point 3, ni suala la muda tu ndio mashabiki wa yanga na Man U ndio mtanielewa nilicho maanisha. Kwa sasa mtanibishia mwisho wa siku mtakubaliana na mimi.

Mashabiki wa yanga na Man U jiandaeni kushangilia sare. Sijaona utofauti kwenye matokeo ya hizo timu kwa sasa kwenye ligi zao huko.

Ni hayo tu wakuu.
Sawa nabii Tito utabiri wako tumeupokea ngoja tufanyie kazi
 
Back
Top Bottom