Yanga kutumika kumvusha lowassa kwenye urais | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yanga kutumika kumvusha lowassa kwenye urais

Discussion in 'Sports' started by LUCIFER, Aug 14, 2012.

 1. LUCIFER

  LUCIFER Senior Member

  #1
  Aug 14, 2012
  Joined: Aug 14, 2012
  Messages: 181
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Kuna habari kwamba Waziri Mkuu aliyejiuzuru nafasi hiyo kutokana na kashfa ya mkataba tata wa Richmond, Edward Lowasa anajiandaa kuwekeza katika klabu ya Yanga kupitia kwa mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuf Manji, ambaye ni swahiba yake mkubwa kibiashara, kama moja ya njia za kumnusuru katika mipango yake ya kuelekea ikulu mwaka 2015.Jaribio la Lowassa kuingia Yanga lilianza kwa utawala wa mwenyekiti wa klabu hiyo aliyejiuzulu, Lloyd Nchunga,ambapo alidaiwa kwamba Lowasa aliomba kuingiza kiasi cha shilingi 800 milioni hasa wakati Manji ambaye alikuwa ndiye mfadhili mkuu wa klabu hiyo, alipogoma kutoa msaada kwa Yanga, lakini Lloyd Nchunga alikataa, linadaiwa kutomfurahisha Lowassa na watu wanaomuunga mkono akiwamo Manji na Rostam Aziz ambaye naye anaelezwa kuwa ni mpenzi wa Yanga.Itakumbukwa wakati wakisuguana na Manji baada ya mfadhili huyo kujiweka pembeni kama mfadhili wa klabu hiyo na baadaye kuonekana akijaribu kujiingiza kwa kutumia mgongo wa wazee wa klabu waliotaka kukabidhiwa timu, Nchunga alihoji wazee hao wangepata wapi fedha zakuendeshea klabu hiyo na akasema hawezi kukabidhi timu kwa watu ambao hajui itaishia mikononi mwa nani kwani huenda wazee hao wanataka kuikabidhi timu hiyo kwa wafanya biashara wa mihadarati.Ingawa hakuwa amemtaja mtu,lakini kauli hiyo ilionekana kuwaudhi wazee hao na kudai Nchunga amewatusi na kumtusi Manji hivyo watahakikisha anaondoka madarakani kwa njia yoyote na ndicho kilichotokea.Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya klabu ya Yanga, njama za kuondolewa kwa Nchunga zilitokana kushindwa kufuata matakwa ya matajiri wa klabu hiyo wanaodai wana mpango wa kuifanya Yanga kuwa tajiri, lakini liwe lengo la kujipatia vyeo nchini kutokana na historia ya kuhusika kwake na harakati za uhuru wa Tanzania tangu Tanganyika.Inadaiwa Lowassa anataka pia kuwa karibu na watu wenye sauti kwenye chama cha mapinduzi visiwani Zanzibar akiwemo mama Fatma karume ili kumsaidia kupata umaarufu na kujijenga visiwani, tayari kwa kuwania urais. Inafahamika kwamba viongozi wengi wa Baraza la mapinduzi Zanzibar wana mapenzi na timu ya Yanga kutokana na timu hiyo kuwa na urafiki na timu ya za Afrika Sports na Miembeni tangu wakati wa harakati za kuwania uhuru wa nchi hizi mbili na Lowassa ameliona hili.Inadaiwa kazi ya kumsafishia Lowassa njia ya kuingia kwenye enzi ya klabu hiyo, inafanywa na Yusuf Manji ambaye jukumu lake kubwa alilonalo ni kuhakikisha anaibadili Yanga kuwa kampuni, na kwa kutumia udhaifu wa wanachama na wapenzi wa Yanga kutotaka kujua kinachoendelea katika klabu yao, isipokuwa waifunge Simba tu ama kuchukua ubingwa,ndiyo sababu ambayo wenye fedha wameeleza kuwa ndiyo njia rahisi ya kumpachika Lowassa awe mmoja wa wadhamini wa klabu ya Yanga pamoja na kuwepo kwa madai ya muda mrefu kwamba Lowassa ni Simba damu.Lakini u-simba wake kwa mujibu wa vyanzo vya habari utafunikwa na fedha ambazo atazimwaga klabuni Yanga na ikiwa njia ambayo pia ilitumiwa na mtu mwengine aliyewahi kuingia kwenye uongozi waklabu hiyo, Seif Ahmed Magari ambaye licha ya wanaojua kwa asilimia mia moja niSimba, lakini alitumia udhaifu wa kutochimbua mambo kwa wanayanga na kwa kuwa yeye ni mfanyabiashara wa magari mwenye fedha, akajifanya anaongoza kutoa msaada kwa wanayanga, kumbe nia ilikuwa kuingia Yanga ili ahalalishe ujanjaujanja wake katika biashara zake.Miongoni mwa mambo ambayo yatafanywa Yanga ni pamoja na kuvunja jengo lililojengwa na Karume na Maalimu Nyerere nakulifanya la kisasa zaidi ambapo litajengwa kama lile la Quality Business Centre ambapo ndani yake kutakuwa na uwanja wa kisasa, maduka makubwa na kila aina ya starehe ambako kwa mawazo yao wanaamini watakuwa wamewamaliza wanachama ambao hamu yao ni kuiona Yanga inashinda na kuwa na vitega uchumi, lakini kwa wao lengo lao lilikuwa ni kumweka Lowassa kwenye kiti cha urais mwaka 2015.ANOTHER MOVIE….hayawale Mnaojiita WANAZI WA YANGA MUTIMU WA MAPESA MPO?SOURCE: AFRICA LEO, 8[SUP]th[/SUP] of August, 2012.
   
 2. K

  Konaball JF-Expert Member

  #2
  Aug 14, 2012
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 1,767
  Likes Received: 462
  Trophy Points: 180
  mhh kama ndio hivyo YANGA itakuwa timu bora kati ukanda wa Africa Mashariki na Kati
   
 3. LUCIFER

  LUCIFER Senior Member

  #3
  Aug 14, 2012
  Joined: Aug 14, 2012
  Messages: 181
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  na wanachama wake wataongoza kwa Umaskini katika ukanda wa Africa Mashariki na Kati.
   
 4. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #4
  Aug 14, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,445
  Likes Received: 5,832
  Trophy Points: 280
  Mhh.......mmiliki wa YANGA (Bw Mkubwa Riziwani) si alishatoa tamko kule Bagamoyo kuwa Rais ajaye hatatoka kaskazini? Hii vipi tena?
   
 5. K

  Konaball JF-Expert Member

  #5
  Aug 14, 2012
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 1,767
  Likes Received: 462
  Trophy Points: 180
  wewe komandoo nini unategemea pesa za club
   
 6. Kaliua urambo

  Kaliua urambo JF-Expert Member

  #6
  Aug 14, 2012
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 606
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Huyu jamaa mbona simba damu kitambo
   
 7. LUCIFER

  LUCIFER Senior Member

  #7
  Aug 14, 2012
  Joined: Aug 14, 2012
  Messages: 181
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Kwani wanaolipia zile ada za 22,elfu cjui 20 kwa mwaka elfu ni kina nan?si wanachama..mi si komandoo bro....ni FREELANCER ha ha ha
   
 8. LUCIFER

  LUCIFER Senior Member

  #8
  Aug 14, 2012
  Joined: Aug 14, 2012
  Messages: 181
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45

  Kwani wanaolipia zile ada za 22,elfu cjui 20 elfu kwa mwaka ni kina nan?si wanachama..mi si komandoo bro....ni FREELANCER ha ha ha
   
 9. M

  MKALIKENYA JF-Expert Member

  #9
  Aug 14, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,198
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 133
  Wewe ndio mpuuzi kweli kwani wanachama wa YANGA wanataka wawe matajiri kupitia YANGA nyie ndio wale hamna shughuli za kufanya mnashinda pale jengo la SIMBA mnamsubiri KABURU aje awape nauli na hela ya kula.
   
 10. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #10
  Aug 14, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Wish I were one of the Mod,ningeweka button ya "USHUZI" habari kama hii(ya mleta thread) inafanania na ile kitu inayotoka mtu anapopumua kwa ile njia nyingine ile.
  Wewe kweli Lucifer unafikiria sisi Wanachama wa Yanga ni Mapoyoyo kama nyinyi,sisi hatuwezi kushangilia picha ya Mwenyekiti wetu amemshika bega Mchezaji fulani na tukaamini kuwa ameshamsajili.
  Huyo Lowasa kama anataka kutumia Club ya mpira kama daraja la kuingia Ikulu aende kule Msimbazi akaanze na issue ya Uwanja ambao Rage kila siku anawadanganyia,huku Jangwani hataamini kitakachotokea.
   
 11. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #11
  Aug 15, 2012
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,784
  Likes Received: 1,038
  Trophy Points: 280
  kama anaona dar young african itamlipa akiwekeza kuna tatizo gani hata kama ni simba... acheni mambo ya kizamani.
   
 12. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #12
  Aug 15, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Huyu mzee ana damu ya kunguni kweli khaaaa...
   
 13. U

  Ubungo JF-Expert Member

  #13
  Aug 15, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Yanga hainunuliki, washashindwa wengi labda na hawa wajaribu bahati yao. Akina Virani, Gulamali, Murtaza Dewji, Mengi nk
   
 14. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #14
  Aug 15, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 21,995
  Trophy Points: 280
  Simba na Yanga zitakufa soon na itabaki Azam peke hake. Huoni Azam wame adopt rangi za Chadema?
   
 15. LUCIFER

  LUCIFER Senior Member

  #15
  Aug 15, 2012
  Joined: Aug 14, 2012
  Messages: 181
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45

  kwa kutumia udhaifu wa wanachama na wapenzi wa Yanga kutotaka kujua kinachoendelea katika klabu yao, isipokuwa waifunge Simba tu ama kuchukua ubingwa,ndiyo sababu ambayo wenye fedha wameeleza kuwa ndiyo njia rahisi ya kumpachika Lowassa awe mmoja wa wadhamini wa klabu ya Yanga .....Huyu bwana hapa ni USHAHIDI TOSHA......AU NI IBRAHIM AKILIMALI NINI?
   
 16. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #16
  Aug 15, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,966
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Bado gonjwa.
   
 17. yahoo

  yahoo JF-Expert Member

  #17
  Aug 15, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 3,424
  Likes Received: 363
  Trophy Points: 180
  ninavofaham mimi huyu jamaa simba damu,labda kama amegundua kama yanga inamvuto zaidi
   
 18. Makoye Matale

  Makoye Matale JF-Expert Member

  #18
  Aug 15, 2012
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 6,480
  Likes Received: 450
  Trophy Points: 180
  Mwandishi wa uzi huu ameishiwa sera.

  Kwani lazima kila mtu aanzishe uzi wake? Kama huna point si afadhali uwe unasoma tu nyuzi za Great Thinkers' badala ya wewe kuweka hisia binafsi na za kinazi kama hizi? Hivi umelenga kuisambaratisha Yanga kwa maneno yako haya ya kipuuzi? Nakuhakikishia, UMENOA! Kajipange upya kama yule jamaa asiye kuwa na TemboCard Master Card katika tangazo la CRDB.

  Yanga Imara, Daima Mbele, Nyuma Mwiko. Die to hell all who hate Young Africans Sports Club.
   
 19. dri ma

  dri ma Senior Member

  #19
  Aug 16, 2012
  Joined: Aug 5, 2012
  Messages: 106
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwli mbaaz ikikosa maua hucngizia jua kwan w nan kakwmbia wanachama wa yanga 2nataka utajir c 2nataka raha bwna
   
 20. LUCIFER

  LUCIFER Senior Member

  #20
  Aug 17, 2012
  Joined: Aug 14, 2012
  Messages: 181
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  aliyekwambia maskini ana raha nani?
   
Loading...