Greatest Of All Time
JF-Expert Member
- Jan 1, 2017
- 20,504
- 44,615
Klabu ya Yanga imeamua kutangaza utalii katika jezi zao katika mechi za kimataifa! Wamefikia makubaliano hayo na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia waziri wa wizara hiyo Dr. Damas Ndumbaro.
Yanga itatangaza bure Mlima Kilimanjaro pamoja na Visiwa vya marashi na karafuu (Zanzibar).
"Tumeamu kuunga mkono juhudi za Mh. Rais kwa kutangaza utalii kama alivyofanya kwenye royal tour" Alisema Kaimu CEO wa Yanga, Haji Mfikirwa.
Nembo hiyo ya kutangaza Utalii itakaa upande wa kushoto wa jezi hiyo!
Hii si mara ya kwanza kwa klabu ya Tanzania kutangaza utalii katika mechi za kimataifa, msimu uliopita Simba walitangaza utalii katika jezi zao walipokuwa wanashiriki hatua ya makundi ya klabu bingwa Afrika!
Hongereni Yanga, kuiga vitu vizuri sio jambo baya!!