Yanga kutangaza utalii kwenye jezi yao kimataifa

FORTALEZA

JF-Expert Member
Jan 1, 2017
8,504
2,000
Klabu ya Yanga imeamua kutangaza utalii katika jezi zao katika mechi za kimataifa! Wamefikia makubaliano hayo na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia waziri wa wizara hiyo Dr. Damas Ndumbaro.

Yanga itatangaza bure Mlima Kilimanjaro pamoja na Visiwa vya marashi na karafuu (Zanzibar).
"Tumeamu kuunga mkono juhudi za Mh. Rais kwa kutangaza utalii kama alivyofanya kwenye royal tour" Alisema Kaimu CEO wa Yanga, Haji Mfikirwa.

Nembo hiyo ya kutangaza Utalii itakaa upande wa kushoto wa jezi hiyo!

Hii si mara ya kwanza kwa klabu ya Tanzania kutangaza utalii katika mechi za kimataifa, msimu uliopita Simba walitangaza utalii katika jezi zao walipokuwa wanashiriki hatua ya makundi ya klabu bingwa Afrika!

Hongereni Yanga, kuiga vitu vizuri sio jambo baya!!

396229DD-D93D-4671-9F5A-79F516F27FF7.jpeg
 

FORTALEZA

JF-Expert Member
Jan 1, 2017
8,504
2,000
Hiyo project ya yanga na hao wizara ya utalii ni white elephant project..yanga na kimataifa wapi na wapi? Si wanaenda kukamilisha ratiba Nigeria kisha waanze Ruti za Namungo na ruvu
Waziri wa Utalii alisema kuwa anaamini Yanga wataenda kupindua meza Nigeria
 

FORTALEZA

JF-Expert Member
Jan 1, 2017
8,504
2,000
Wizara watu wa hovyo....

Uto wana mechi gani za kimataifa..!? Au msimu ujao wa 2022/2023!?

Bora hata wangeingia mkataba na Biashara au Azam.....
Waziri anaamini Yanga watafanya maajbu kisa tu takwimu zote zilimbeba Yanga mechi ya kwanza😂
 

Bukali

JF-Expert Member
May 7, 2018
932
1,000
Wazee wa kuiga hahaa
Mbona wabongo tunataka kuwa empty set sana vichwani mwetu?
Jambo jema lazima lifanyike, mbona kuna vist Rwanda ,ilipoanzishwa ya simba ulisijia wao wamesema wamekopy? Tumia akili kidogo msilete usimba na uyanga maandazi nyie mashabiki 2018.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom