Yanga kulilia Ufadhili wa Manji: Taswira ya Taifa letu, kutegemea Wafadhili! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yanga kulilia Ufadhili wa Manji: Taswira ya Taifa letu, kutegemea Wafadhili!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rev. Kishoka, Dec 29, 2009.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Dec 29, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Ni aibu gani hii ambayo watu tunaishia kuwa ombaomba na kutegemea wafadhili mpaka tunaamua wanastahili wapewe madaraka?

  Najua wengine wenu mtaliangalia jambo hili kama suala la mpira na ushabiki wa michezo, lakini kitendo cha wachezaji wa Yanga kumlilia Manji ni sawa na kile kitendo cha wale waliomlilia mkoloni na kumtukuza au wale manamba waliokuwa kwenye mashamba ya Wagiriki ambao waliwaabudu hao Wagiriki. Na nikiongezea ni jinsi Wana wa Israeli ambao waliona kuwa safari yao ya kwenda kwenye nchi walioahidiwa ilikuwa ni udhia na hivyo wakajuta kuyaacha masufuria ya Pharao!

  Ni lini Tanzania tutaachana na mambo ya kuwalilia na kuwanyenyekea hawa watu tunaowaita Wafadhili?

  Jambo hili si la Simba au Yanga pekee, ni LIUGONJWA kubwa na baya kuliko Malaria na Ukimwi!

  NI lini jamii na jumuiya zitaanza kujituma na kubuni mbinu za kuweza kujitegemea na kujizalishia bila kutumai cha mfadhili?

  Kibaya zaidi ni kuwa Manji huyu huyu, ni mtuhumiwa wa kuhujumu Uchumi wa nchi, sawa na wakati wa Gulamali na Dewji, nao walikuwa na tuhuma kibao za kuwa ni wafanyabiashara wa mambo haramu ambao walijipendekeza ndani ya klabu za mpira na hata ndani ya Siasa kiasi kufikia kwa Gulamali kuwa mbunge!

  Kuna haja ya kufanyika tathmini na kampeni kubwa mno ya kupiga vita ombapmba na kutegemea Wafadhili.

  Mimi ni Yanga, lakini kitendo hiki, kimenidhalilisha na kunisononesha, sawa na vile CCM inavyoendelea kukumbatia Wafadhili ambao wametuhujumu na kuangamiza uimara wa Serikali yetu na maadili ya Taifa letu.

  Jambo hili linaonyesha wazi ni vipi Tanzania ilivyo mbali sana kufikia azma ya kuwa Taifa linalojitegemea na kujenga jamii ya watu wenye kujitegemea!

  Narudia tena hii ni aibu kubwa sana kwetu kama Taifa, na sijali ikiwa wewe ni mshabiki wa Simba au Chadema, lakini hii ni hali halisi ya kisiasa na kijamii ya Tanzania kutegemea ufadhili kwa kila kitu.

  Tanzania tunapenda sana misaada, lakini kujituma tujizalishie kwa mbinu na juhudi zetu wenyewe hakuna!

  Asilimia 40 (40%) ya bajeti ya nchi inategemea Wafadhili. Wiki hii Serikali kupitia Hazina na Benki Kuu wametangaza tumefadhiliwa misaada si chini ya Dola za Kimarekani Millioni Mia Tatu!

  Za nini fedha hizi? kwa nini tunaendelea kama Taifa kuwalilia kina Manji na hata kuwaomba wawe wagombea wa nafasi ya juu katika jamii yetu?

  Ama tumelaaniwa!


   
 2. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #2
  Dec 29, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  yanga hawajui nani hasa ni ''mfadhili wao''!wanadhani ni manji:D
   
 3. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #3
  Dec 29, 2009
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,679
  Likes Received: 21,919
  Trophy Points: 280
  Rev.Kishoka, Niliisikia habari hii jana kwa masikitiko makubwa sana. Hivi sisi tatizo letu kubwa katika akili zetu ni nini? Bila kuwa na neno wafadhili ndio hatuendi mbele? na mbaya zaidi ufadhili huo hatujali unatoka kwa nani. Unamtuhumu mtu kakuibia usiku na asubuhi unampigia magoti kumwomba sukari.
  Natatizo hili la ombaomba haliko ktk Club tuu, hata serikali yetu ndio usiseme maana mpaka inajisifu kama vile kuomba ni SIFA.
   
 4. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #4
  Dec 29, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Tatizo pesa, wanachama hawachangi pesa, Vilabu vingi vimekufa kwa ajili ya pesa wamekosa wafadhiri, nyie mnafikiri bila NMB na Serengeti Taifa Stars ingeng'aa hivyo? Ziko wapi Lipuli, Costal, Bandari, Pamba n.k zote zimekufa kwa ajili ya kukosa ufadhiri.
  Angalieni na huko majuu Man U, Liverpool, Chelsea zinaendeshwaje?
   
 5. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #5
  Dec 29, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  CCM mbona wanachangisha wanachama na kuchota kutoka Serikalini lakini bado inawakimbilia Wafadhili kama kina Manji na Rostam?
   
 6. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #6
  Dec 29, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  yanga itashaini tu mwanzo mwisho!mfadhili wa yanga si MANJI!manji anatumiwa tu.....!stuka
   
 7. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #7
  Dec 29, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,056
  Likes Received: 24,060
  Trophy Points: 280
  Nahisi kama nimesahau mawani yangu! Ni wewe au kuna mtu kakamata pasiwedi yako?
   
 8. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #8
  Dec 29, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,377
  Likes Received: 3,140
  Trophy Points: 280
  watu wanaaminiwa na kupwa nafasi ili kutumikia lakini cha ajabu wanataka kutumikiwa wao badala ya wao kutumikia taifa/taasisi waliyopewa..........maslahi binafsi yalisumbua taifa hili................watu wamechoka kufikiri kwa hiyo pamoja na kupwa nafasi bado wanataka watu wengine wafikiri kwa niaba yao...............
  inatia aibu..
   
 9. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #9
  Dec 29, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  mkuu,
  yanga haiwezi kutetereka!yanga inafadhiliwa na mkuu mwenyewe!sema anamtumia manji...!naona manji amechoka KUTUMIKA!wana-yanga wasipate shida:D
   
 10. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #10
  Dec 29, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,056
  Likes Received: 24,060
  Trophy Points: 280
  Karibu msimbazi pale. Friends Of Mnyama tuna kikao leo.
   
 11. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #11
  Dec 29, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Yanga hawajui kuwa walikuwa wanatumiwa tu. Manji aliingia kuifadhili Yanga baada ya kuona Mengi anawashauri namna ya kujitegemea pale alipowashauri wajiendeshe kibiashara baada ya kuwa amewalipia tiketi za kwenda kucheza South Africa katika mojawapo ya mashindano yaliyokuwa yakiwakabili. Manji alitaka Yanga wasiwe na hayo mawazo ya kujiendesha kibiashara ili ................
   
 12. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #12
  Dec 29, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Ndo hapo umeona umuhimu wa wafadhii bila hao chama hakiendi kiko wapi NCCR? TLP?
   
 13. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #13
  Dec 29, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  yaani Yanga ijitegemee? ..
   
 14. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #14
  Dec 29, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  wanaoiua yanga TUNAWAJUA!na kwakweli leo nitamuomba mungu ujasiri niwataje hawa watu!.....
   
 15. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #15
  Dec 29, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,441
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  sisi watanzania tutaendelea kutawaliwa hadi lini sijui!!? yaani club inawanachama malaki lakini bado inategemea mtu mmoja aiongoze kifedha!! Huu ndio ukoloni mamboleo aliouita Mwalimu Nyerere...
   
 16. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #16
  Dec 29, 2009
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kumbe nchi yenyewe inategemea wafadhiri ambao ndio hao waliotutawala na kutunyonya,iweje leo ukaituhumu Yanga kukumbatia mfadhiri,au ndio ile adui yako mwombee njaa?Nina wasiwasi we si mwenzetu ila unatumiwa tuu.
   
 17. K

  Kamese B Magoti Member

  #17
  Dec 29, 2009
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi sishangai baadhi ya wana Yanga kulilia ufadhili wa Manji kwani hii imeshakuwa sehemu ya utamaduni wa Watanzania walio wengi! Manji ameeleza vizuri sana kuhusu malengo aliyojiwekea wakati alipoamua kuisaidia Yanga na sasa ameona ni wakati mwafaka kuiacha Yanga ijiendeshe yenyewe kwani inaouwezo huo! Hoja tunayopaswa kuijadili hapa ni kuwa iweje Manji aone uwezo Yanga ilionao lakini Viongozi wa Yanga,Kundi la Wazee,Wachezaji na Mashabiki wanaogaragara mlangoni kwa Manji wasione ? Tatizo la Watanzania walio wengi hawaamini kuwa wanaweza kufanya jambo lolote kwa mipango waliojiwekea bila wafadhili,iwe ni katika siasa, michezo,uchumi,dini n.k.
  Labda kitu ambacho napenda kuwajulisha Watanzania wenzangu ni kuwa kuna Watanzania wenzetu ambao wameamua kuishi katika Nchi yao iitwayo "Mediocrity Country" .Hii ni Nchi mpya inayopatikana ndani ya Tanzania na Jiografia yake iko hivi ;Upande wa kasikazini inapakana na Nchi iitwayo ''Compromise" ,upande wa Kusini inapakana na Nchi iitwayo "Indecision" ,upande wa magharibi inapakana na Nchi iitwayo "Past thinking" na Upande wa Mashariki inapakana na Nchi iitwayo "Lack of Vision".Kosa kubwa tulilofanya Watanzania ni kuwapa nafasi Watu wa Nchi hii mpya niliyoitaja kushika Madaraka makubwa katika Nchi yetu ya Tanzania kuanzia katika siasa,michezo,dini n.k.Sifa kubwa ya Watu wa nchi hiyo ya Mediocrity ni kwa wao ni "Normal People".Tusikubali kuongozwa na watu wa Nchi hiyo kama kweli tunataka maendeleo katika kitu chochote katika Nchi yetu!
   
 18. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #18
  Dec 29, 2009
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kama leo Yanga ikiamua kuuza hisa zake kwenye Dar Stock Exchange,watu wengi watanunua!Mnakumbuka Yanga Kampuni na Yanga Asili.Wazo la kampuni lililetwa na Mengi karibu miaka 10 iliyopita!Wahindi walipinga maana wanajua wanachokinya.Ndio hapo Mhindi na Mengi hawakai pamoja.
  Mbali zaidi "waswahili" Yanga always watanunuliwa na Wahindi.

  Manji anatuhuma kubwa lakini in Tanzania mambo ni big joke.
   
 19. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #19
  Dec 29, 2009
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,679
  Likes Received: 21,919
  Trophy Points: 280
  Kichuguu, maneno yako yamenikumbusha usemi mmoja kule kwa marehemu babu yangu. Alisema, ndugu yako akiwa na shida ya chakula kama unampenda mpe jembe na mbegu na sio unga maana na kesho na siku inayofata atakuja tena huku akidhalilika kwa kuomba.
  Mengi aliwapenda Yanga ndio maana aliwashauri jinsi ya kujinasua na uombaji na wajitegemee kwa kutumia rasilimali zao, lakini wao wakaona Manji anayewapa Unga wapike ndio anawapenda zaidi. Ok,Ndiyo Tanzania yetu ilipofikia
   
 20. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #20
  Dec 29, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  He he heee, Yanga-Bomba wewe !! Mbona Mo aliposema basi kwa Mnyama hawakuandamana? Tatizo viongozi wa Yanga (na Simba pia) hawana mikakati ya kweli, ndo maana akishatumikia miaka kadhaa anaona ameshajijengea jina, utamsikia ameenda kugombea ubunge, hayo ndio malengo yao. Kwani hukushtukia viongozi wa Yanga wanalazimisha uchaguzi wa klabu ufanyike haraka kabla ya muda wao wa madarakani haujaisha? Walishaona watachelewa kwenye maandalizi ya majimboni 2010.
   
Loading...