Yanga kufungwa 5-0 na Simba je wana Yanga wamejiunza nini?

yaan naona simba waliwahurumia yanga tano bila c mchezo, yanga waache marumbano badala yake wajipange la sivyo watalia tena
 
Laana ya wazee wa Yanga kuna mmoja alionyesha korodani zake ndo laana hiyo
hawa watu wanajiita baraza la wazee Yanga ni tatizo kubwa,ongeza na wapiga domo kibao wanaoshinda klabuni wakiitegemea klabu kula yao! baada ya kitendo cha uhuni kwa wachezaji wa Yanga kumpiga mwamuzi nilitarajia kusikia adhabu kali ikitolewa kwa wachezaji mabondia,lakini hakuna hatua iliyochukuliwa. baadaye nikatarajia wanachama wangekuja juu kuulazimisha uongozi uchukue hatua za nidhamu,ikawa kimya!!! kwa hiyo Yanga kuanzia uongozi,wachezaji na wanachama wajitafakari upya kabla mambo hayajaharibika zaidi. mpira wa kutegemea akina Manji na kununua ushindi hautawafikisha popote! anguko linaloikabili CCM naliona linainyemelea na Yanga!
 
Ndiyo mambo poeni Yanga. Ila naona kama mulikuwa usingizini vile.

Samahani lakini mimi si mshabiki wa chama cho chote cha mpira ndani au nje ya nchi, napenda kutania tu.
 
Tumejifunza kwamba wazee hawafai kupewa timu maana mbinu zao bado za mwaka 47 wanategemea TOBOA TOBO!
 
..wajifunze kuwa hela haramu za kifisadi za akina RZ1, Rupia na JK zina nuksi. Na pia viongozi wenye njaa sio kitu powa. Na ukijumlisha ya hizo rangi ambazo hata kisiasa zimeanza kufulia ndo balaa..! Mnasajili players kwa sababu yule wa kucheka cheka na wenzake wanawapenda na sio kwa sababu ya uwezo wao..!
 
fundisho walilopata ni moja tu- mshindi wa mpirahupatikana baada ya mechi kuisha!
 
Wana JF hebu nifahamisheni kile kipigo cha Yanga jana dhidi ya mtani wake Simba je wana Yanga watakuwa wamejifunza nini, maana nimetafakari toka jana lakini sijapata jibu sahihi mpaka naleta maada hii:spy:

Simba wanalo la kujifunza pia pamoja na Ushindi mkubwa waliopata.

Somo kwa Simba: "Umoja na Ushirikiano ni siri ya mafanikio"
 
Mtanisamehe mashabiki wa Yanga hawana tofauti na wachama wa CCM. I mean they never learn anything from their mistakes
 
Kwani simba kukosa makombe ya tusker, kagame na ligi kuu mwaka jana simba walijifunza nini,. Mpira ndo ulivyo,. Bacelona walifunga real 6, man u kwa aseno 8, man city kwa man u 6,. Yanga itabaki mabingwa wa kihistori tanzania,. Subirini kagame muone,.

Walichojifunza Simba ni kuchukuwa ubingwa kwakumdunda mjingamjinga 5 ili ajue starehe ya ubingwa sio 3 au 1..........nyambafuuuuu kandambili kwake chooni tu sebuleni unatuletea kipindupindu
 
Yanga wajifunze kuwa msimu uliopita Mfumo wa Uongozi waYanga haukuwa endelevu. Uongozi imara ni ule unaojihakikishia kuwa chanzo cha Mishahara ya wachezaji na Mwalimu kina kuwa bayana na cha uhakika (km kulipwa moja kwa moja na wadhamini wa ligi), Kuachana na utegemezi wa mtu mmoja ambaye akigombana na hawala yake..ni kikwazo kwa klabu! Endesheni timu km kampuni, na si km kijiwe cha kuwanufaisha wapambe wa viongozi, na ma-bouncer uchwara.
 
Mtanisamehe mashabiki wa Yanga hawana tofauti na wachama wa CCM. I mean they never learn anything from their mistakes

sobhuza loves this post of you.
Wale wazee wamehujumu timu ili Nchunga aonekane mbaya, na washabiki wa Yanga nao wamekubaliana na hilo, eti wanamlaumu Nchunga kwa kufungwa huku. Kusoma hawajui hata picha hawaoni?
 
Last edited by a moderator:
sobhuza nakubaliana na wewe, binafsi hilo nililiona, mara Nchunga amekabidhi wazee timu, halafu Nchunga anakanusha, hiyo ilikuwa ni hesabu rahisi sana, ila sikutegemea kipigo cha mbwa nanma ile. Wale wazee nuksi...
 
Kwa mgogoro ule nilikuwa na uhakika lazima Yanga itafungwa, ningepata mtu wa ku-bet naye ningevuna besa za bora enzi zile mtu alikuwa radhi kuweka poni mke wake nadhani ningejipatia mke kwa ulainiiii. Tuachane na hayo, sasa umefika wakati wa kuachana na mambo ya wazee wa timu, wafadhili wa timu, sijui friends of what, kamati za ufundi, matawi ya timu, timu rafiki, mabaunsa, n.k. hao ndio wanaoleta matatizo inapokuwa interest zao ziko hatarini. Ni bora timu zikawa na uongozi wa kisayansi. Hizi timu zisiwe vijiwe vya watu fulani, kujifanya damudamu kumbe uwongo mtupu, njaa tu. Madega alikuwa na mipango mizuri ya kuifanya timu kuwa kampuni, watu wakaleta upinzani baada ya kuona ulaji wao uko hatarani, mpaka hakufanikiwa kama alivyotaka, kisa njaa za watu. Tuachane na mambo ya uanachama, tuingie kwenye wanahisa, nina uhakika mapato yatadhibitiwa na kuacha kutegemea wahisani wenye masharti yasiyo na maana na matajiri kuwa Miungu watu. Mimi ni mpenzi wa Simba lakini nakubali Madege ilikuwa kichwa bwana. Ni ujinga Yanga ikifungwa na timu nyingine hakuna noma ikifungwa na Simba au Simba ikifungwa na Yanga basi nongwa, hovyoooo!!
 
Mtanisamehe mashabiki wa Yanga hawana tofauti na wachama wa CCM. I mean they never learn anything from their mistakes
ni maneno yenye ukweli mchungu kwa wapenzi na mashabiki wa Yanga na hata Simba,ingawa kwa Yanga uswahili umezidi sana! utadhani hii klabu haina vijana wasomi na waelewa!
 
Hata mm nashauri yanga wabadiri rangi ya jezi,au wawe na utararatibu wa kuvaa nyeusi na njano,na nyeusi na kijani
 
ni maneno yenye ukweli mchungu kwa wapenzi na mashabiki wa Yanga na hata Simba,ingawa kwa Yanga uswahili umezidi sana! utadhani hii klabu haina vijana wasomi na waelewa!
Nimewaangalia kwenye Taarifa ya habari ya ITV jana usiku hao wanaoitwa eti wanachama wakereketwa wa Yanga kwa macho tu ukiwatizama unajuwa kabisa hapa mwenye Elimu kubwa ni darasa la saba, na ukiwascan vizuri mifukoni wote kwa ujumla wao unaweza usipate hata shilling laki moja, lakini kazi yao kubwa majungu na kelele tu.
 
KATUNI(691).jpg
 
Wamejifunza kwamba Simba ya leo ya 5-0 ina huruma zaidi kuliko ile Simba ya 7-0 ya enzi zileee!

Unapokuwa Senior Member wa forum makini kama JF hlf unaandika vitu usivyovielewa unatukatisha tamaa sana sisi Members wa kawaida,hiyo Simba ya 7-0 ya enzi zileee ni Simba ipi?..Simba imeshawahi kumfunga Yanga 7-0? revise your memory.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom