Yanga inyang’anywe point zote kwa kumtumia Kessy - Rage

PROSPER 05

JF-Expert Member
Oct 14, 2013
226
217
Daen-Rage.jpg

Mwenyekiti wa zamani wa Simba Ismail Rage ameitaka klabu ya Simba kwenda mbele zaidi kudai haki yao na si kukubali kiasi cha shilingi milioni 50 kama fidia kama livyoamriwa na Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji.

Katika hatua nyingine Rage amesema, Yanga inatakiwa kupoteza pointi zote katika michezo ambayo walimtumia Kessy kwenye kikosi chao.

“Maadam TFF wanakiri kwamba Kessy alikuwa mchezaji halali wa Simba SC na Yanga wamevunja mkataba kabla ya wakati, Yanga wanatakiwa wanyang’anywe pointi zote walizoshinda dhidi ya timu nyingine kabla ya uamuzi wa TFF,” amesema Rage wakati akihojiwa na kipindi cha michezo cha Sports Extra cha Clouds FM.

“Simba wanatakiwa wasichukue hizo milioni 50 watakuwa wamejidhalilisha sana, kwa mujibu wa mkataba wa Simba, wanatakiwa wapate 1.2 billion kama dola za 600,000 kimarekani. Waende FIFA kwa ushahidi wote uliokuwepo na TFF wameshiriki kuvunja mkataba kwahiyo ushahidi upo wa kuwatia hatiani Yanga.”

“Kessy alikwenda Uturuki na Yanga wakati bado anamkataba na Simba, akaenda Algeria wakati bado yupo ndani ya mkabataba, wakienda ubalozi watakuta ushahidi lakini wakienda uhamiaji watapata pia ushahidi.”

source:Mpenja blog

  • JE Madai Haya Yana Uhalisia Wowote Kisheria?
  • Kwani Kwa sasa (baada ya uamuzi wa kesi)Kessy ni Mchezaji Halali wa Yanga? Kuanzia Lini
 
Points zipi? Ligi ya mabingwa au shirikisho? Wakati Vpl inaanza kessy alikuwa na mkataba na simba?
Haijalishi! Inaangaliwa toka mwanzo wa usajili wake, ulikuwa na uhalali? Kama sivyo wangesubiri wasimtumie hadi mgogoro uishe.Sasa TFF waliwaingiza porini.
 
Points zipi? Ligi ya mabingwa au shirikisho? Wakati Vpl inaanza kessy alikuwa na mkataba na simba?
mkuu unapoteza muda wako kuwajibu mbumbumbu,akil zao fupi sana kwenye masuala ya mikataba na soka,ngoja tuje na tamko letu ili tukutane huko caf na fifa
 
Litakalokuwa na liwe tumechoka na ubabaishaji wa hizi club mbili, kila siku wao tu wao tu kama hawajui sheria, kanuni na taratibu za soka si wafute club zao waache wanaojua taratibu na kuzitii!!
 
Hayo maoni ya rage ni matatizo ya kuvutia bange chooni
Ingekuwa vyema akaisoma vizuri hiyo hukumu kabla ya kuropoka
 
Back
Top Bottom