Yanga inahitaji sajili 4 bora za uhakika ili kuwa na timu kamili

Me kama mwana yanga napendekeza au kutoa ushauri kwa rais hersi kufanya sajili za wachezaji kama ifuatavyo.

1. Striker, yanga inahitaji mfungaji mwenye ubora anaeweza kumililiki mpira,kufunga na mwenye nguvu. Hawana kina mzize sio wa wabovu ila ligi ya mabingwa hawana uwezo huo.

2. Kiungo mkabaji halisi au holding midfielder, sana sana apatikane holding midfielder mwenye ubora, aucho anapendeza kucheza kama Central midfielder na sio kama anavotumika pale yanga kama holding midfilder.

Kabla sijaendelea nieleze kidgo tofauti ya holding midfielder na Central midfielder na sifa zao.
-Holding midfielder ni kiungo ambaye eneo lake ni mbele ya mabeki na majukumu yake kuichezesha team kutokea chini na kusaidia kukaba, sifa zao wanakuwa na uwezo mzuri wakupiga pasi fupi na ndefu .

Central midfielder huyu ni kiungo wa kati na majukumu ya ni kuichezesha team kupitia yeye hapo kati kati ya uwanja, kiungo huyu huunganisha team team kutoka nyuma kwenda mbele na sifa zake ni awe mzuri ktk kupiga pasi za uhakika fupi fupi na ndefu, huyu ndo anaamua team ichezeje kutokana na uwezo wake wa kulitawala dimba na pasi zake za uhakika.

Ukiangalia sifa zao hapo utagundua kwanza aucho ni mzuri wa kupiga pasi sahihi na ni mchezaji anayelazimisha team iende mbele kwa pasi zake, ni mara chache sana aucho kupiga back pass.

Aucho hana kasi sana kumchezesha nyuma ndomna mara nyingi anapigwa sana kadi za njano akipitwa anacheza rafu,

Asajiliwe holding midfielder ili aucho apogee awe Central midfielder na pacome acheze eneo la aziz ki.

Winga mbunifu, moloko ni winga wa kizaman sana anapswa kuachwa haraka sana anaziba nafasi za wachezaji wa kimataifa, tunahitaji winga mwenye uwezo wa kulifata box la adui akiwa na mpira na mwenye kasi. Muangalie yule hussein el shehat wa Al ahly hawa ndo mawinga wa kisasa. Yanga itafute winga wa maana iachane na huyu moloko.

Beki 3 mwenye nguvu za kupanda na kushuka kama yao, huyu lomalisa mzuri sawa lkn nafikir anahitajika mbadala wake kama yule haji mwinyi.

Kingine kocha aache kukariri kwamba lazima aziz ki acheze, mechi hizi za kimatafa kwa uchezaji wa aziz ki wa kuchelewa kufanya maamuz tutamlaumu tu. Mechi kama Al ahly mtu kama max anapaswa kucheza lile eneo la aziz ki kwasabab max yupo faster sana hapotez muda kukaa na mpira na ana maamuz ya haraka sana kwenda mbele.

Yanga haina Tatizo lolote kwa Sasa
 
Kwakua umetaka kueleweshwa ngoja nikueleweshe, Holding midfielder sio namba 8, holding midfielder huwa pale mbele ya mabeki, ni kama DM lkn tofauti ni majukumu yao.

DM majukumu yake namba 1 uwanjani ni kukaba, hawa hawana majukumu ya kushambulia lbda kama ziada tu , ila jukumu lao namba 1 ni kukaba, DM huwa anazunguka sana uwanjan kuutafuta mpira na ndo jukumu lake namba 1 uwanjani ila eneo lake ni pale mbele ya mabeki mfano halisi muanglie ngolo kante .

Holding midfielder na yeye eneo lake ni hilo hilo kama DM ila majukumu yake ni tofauti, Holding midfielder yeye majukum yake ni kuichezesha team kutokea huku chini na huwa hana movement nying uwanjan kama DM. Alafu holding midfielder sio lazma awe na mwili au manguvu ila at awe na uwezo wa kupiga ndefu na fupi, ni mtu anayeanzisha mashambuliz kutokea chini, mfano kwa bongo ni mkude au alonso kama ulimuona enzi zake.

Sasa kitu kingine kila kocha na mfumo wake anaouamini, kuna makocha wanapenda kutumia holding midfielder na kuna ambao wanapenda kutumia DM au wapo ambao huwatumia wote kwa pamoja.

Kwa mfano yanga ya nabi ilikua ikimtumia bangala kama holding midfilder wakicheza na aucho eneo hilo wakiwa na majukumu sawa.
Twende kwa mifano zaidi ili usomeke.
Kama ulivyofanya kwa kutoa mfano wa Ngolo Kante,
by the way wewe ni analyst mzuri.
Unawazidi kwa mbali wachambuzi wengi uchwara.
 
Ni mashabiki wa soka dunia nzima hasa nchi za mpira tena si tuna nafuu lakini nchi zote zenye amsha amsha za mpira huwa mechi ikiisha lazima maoni yawe mengi
Ndio maana Bayern Kila Leo wanabadili kocha Chelsea ndio kabisa PSG nadhani mwenyewe huwa unaona
Ni kwamba mashabiki Wana push kupata kilicho bora kama haya huyapendi shabikia Azam hutasikia shida
Ulivyonijibu kama vile naujua mpiraa mm nachangamsha uzi tu kwenye mpira sijui kitu
 
Baada ya kufungwa na Medeama week ijayo tutamlakamikia pia hersi, mdhamini, na tff
Badala ya kuiwazia Yanga, iwazie timu yako ambayo mechi ijayo inacheza na Bingwa mtetezi kwenye uwanja wake wa nyumbani, huku huyo Bingwa mtetezi akiwa amepoteza mechi 2 mfululizo!

Hatutaki kusikia tena zile kelele zenu za kumkataa Mwenyekiti wenu Mangungu. Nawatahadharisha mapema.
 
Back
Top Bottom