Yanga iko kwenye utumwa wa Manji

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
75,223
157,419
Obrey Chirwa amegoma kukabidhi pasipoti yake, hivyo hatokwenda ALGERIA- SG Mkwasa....
Hii ni dalili mbaya klabuni kwetu, Yanga inashindwa kujiendesha kitaasisi, na haya tuliyapigia sana kelele kuwa timu isimtegemee Manji pekee timu inapaswa ijiendeshe kikampuni na iweze kujiingizia mapato kutokana na vyanzo vya kudumu katika tasnia ya mpira, vyanzo hivyo ni kama viingilio,ada ya uanachama, haki za matangazo ya televisheni, kuuza bidhaa zenye nembo ya klabu ya Yanga nk.
Cha kushangaza Yanga inajiendesha kama timu ya mtu mmoja, huyo mtu akiumwa tu timu nzima nayo inaugua, huyo mtu mkimkera tu, basi mtajuta,hili halikubaliki lazima klabu ijikwamue katika utumwa wa namna hii.
Klabu ya Yanga ni bidhaa inayolipa zaidi ya ngada na dhahabu kwa thamani iliyonayo, leo hii timu inakosa uwanja wa mazoezi, timu haina hosteli wala mgahawa wa chakula wakati tunauwezo wa kutumia rasilimali zetu kupata Mikopo katika taasisi za kifedha ambazo zinaweza kutumika kujengea uwanja utakaoweza kutumika kuchezea mechi zote za Yanga na hata kukodisha kwa timu nyingine.
Kumiliki uwanja kwa timu kama Yanga ni mtaji mkubwa sana ambapo uhakika wa kuingiza mashabiki elfu nane kwa wastani wa kila mechi inawezekana kwa kiingilio cha shilingi elfu 7 kwa mtazamaji sambamba kutoza viingilio mashabiki katika mazoezi na mechi za kirafiki.
Sambamba na hilo pia kama klabu tuna uwezo wa kuuza jezi, traki suit, kanga za kinamama, sandals, na vinywaji laini kama vile soda, juice, nk zenye nembo ya Yanga kwa uhakika tunaweza kupata wateja wengi na timu ikajiingizia pesa za kutosha.
Andiko hili limejaribu kugusia japo kwa uchache ni jinsi gani klabu yetu inaweza kujiendesha yenyewe kama taasisi ila itategemea na aina ya viongozi tutakaowachagua.
Klabu yetu hukutulipofikia ni aibu, hasa hili la baaadhi ya watumishi wetu kukosa malipo yao.
Mwisho wanaYanga tunapaswa kujisahihisha hasa katika viongozi tunaowachagua.
# DaimaMbele
Mussa SA.
 
Kuna kauli ya "Uzalendo kwanza-Mkataa kwao nimtumwa-Penda cha nyumbani".

Hawa Simba na yangu na viongozi wao wanatufanya kauli hapo Juu tuzione hazina Maana yoyote.

Huwa nashindwa kuelewa kwamba ni Njaa zimewazidia hawa viongozi au ni akili mgando ....Hizi timu zinatia aibu sana,Mimi naamini wanawezakufanya makubwa katika Soka na kuimarisha uchumi wao.


Sasa baadhi ya wabongo wamezitupa mkono na kujikita katika ligi za bara la Uropa.
 
Ni Azam pekee wasio utumwani kwa maana hiyo.
Yanga Ni club ya wanachama. Je wanachama kwa umoja wanaweza kuendesha timu?
Badala yake kuna watu wanataka kuvuna huko. Kwa njia hiyo utumwa ni lazima
Matopeni vivyo hivyo!
 
Manji alitaka kununua nyumba 50 jangwani ajenge uwanja "jangwani city"serikali haitaki..sasa Manji afanye miujiza?benki ya Posta ilitoa kadi za benk
i na ziwe kadi za Yanga...Mzee Akilimali akazikataa..wazee wote wafe ndio tutafanikiwa
 
Back
Top Bottom