Balantanda
JF-Expert Member
- Jul 13, 2008
- 12,472
- 4,737
Kamati ya nidhamu ya TFF imewafungulia mabingwa wa soka wa Tanzania,Yanga kutoka katika adhabu iliyokuwa imepewa na TFF kufuatia Yanga kutopeleka timu uwanjani katika mchezo wa kombe la Kagame dhidi ya Simba..............Hata hivyo licha ya kufunguliwa Yanga imetozwa faini ya dola za kimarekani 20000(elfu ishirini) pamoja na viongozi wake kutakiwa kuomba radhi kwa TFF kwa kitendo kisichokuwa cha kiuanamichezo cha kutopeleka timu uwanjani..............Mwenyekiti wa kamati ya nidhamu ya TFF SAID HAMAD EL-MAAMRY amesema kwamba kamati yake imetengua uamuzi huo wa TFF kwa vile hakuna kifungu kinachoeleza adhabu ya miaka miwili(02) kwa timu itakayogoma kuingia uwanjani.Kwa hali hiyo TFF ilitakiwa kutumia kifungu cha adhabu cha FIFA ambacho ni adhabu hiyo (ya dola 20000) iliyotlewa na kamati ya nidhamu ya TFF