Yanga, GSM kuweni makini na ajira/usajili wa kocha msaidizi

mito

JF-Expert Member
Jun 20, 2011
10,522
10,440
Juzi na jana nimesikia Yanga na GSM wako ktk hatua za mwisho kumtambulisha kocha msaidizi. Ni hatua nzuri kuelekea maboresho ya benchi la ufundi. Lakini umakini mkubwa unatakiwa ili yasitokee tena yale ya Mkwasa na Luc au Mkwasa na Zahera.

Club makini zote duniani zinaanza kusajili kocha mkuu, kisha yeye ndo anapendekeza kocha msaidizi. Hii inaepusha migogoro ktk benchi la ufundi. Sasa Yanga nasikia wanataka kuanza na kocha msaidizi, kisha ndo walete kocha mkuu. Kwa staili hii benchi la ufundi halitakaa litulie.

Ni wazo tu natoa kwa uongozi wa Yanga na wadhamini GSM
 
Kocha mkuu ndie aamue kocha msaidizi awe nani.. ili kusiwe na majungu

Ulaya kocha mkuu ndie anaajiri wasaidizi wake wote hadi ma daktari wa timu.. anaamua yeye nani anafaa
Tatzo uchumi kiongozi. Akikuletea benchi la ufundi mtaweza kuwalipa. Sometyme timu zetu zinaepuka hilo kwa kuogopa gharama coz km kocha msaidizi akatoka ulaya pia n gharama kuwahudumia Bora wakwetu hapa mtapeana kiswahili mtaelewana
 
Hakuna fukuto,kusepeshwa kwa kishingo hakuhusiani na natola,kwahiyo unawasingizia tu unataka kusawazisha matatizo yenu ya Yanga as if simba tuna matatizo pia
Klabu kama ni kubwa na ina mashbiki zaidi ya milioni, lazima itakuwa na matatizo na majungu. Simba ipo organized to the point that matatizo yake yanapatiwa ufumbuzi kiofisi kwa kufuata protocols au policies za kimkataba.
Lakini matatizo yapo, na hata Senzo usimtegemee kuwepo pale kwa muda mrefu.
It's normal, hata timu kubwa duniani zina matatizo yaleyale.
 
Mkuu simba hata kama matatizo yapo hakuna prove kwamba yapo,matatizo ya simba kwa sasa hayawezekani kuonekana nje kiasi cha sisi kusema ina matatizo
Klabu kama ni kubwa na ina mashbiki zaidi ya milioni, lazima itakuwa na matatizo na majungu. Simba ipo organized to the point that matatizo yake yanapatiwa ufumbuzi kiofisi kwa kufuata protocols au policies za kimkataba.
Lakini matatizo yapo, na hata Senzo usimtegemee kuwepo pale kwa muda mrefu.
It's normal, hata timu kubwa duniani zina matatizo yaleyale.
 
Juzi na jana nimesikia Yanga na GSM wako ktk hatua za mwisho kumtambulisha kocha msaidizi. Ni hatua nzuri kuelekea maboresho ya benchi la ufundi. Lakini umakini mkubwa unatakiwa ili yasitokee tena yale ya Mkwasa na Luc au Mkwasa na Zahera.

Club makini zote duniani zinaanza kusajili kocha mkuu, kisha yeye ndo anapendekeza kocha msaidizi. Hii inaepusha migogoro ktk benchi la ufundi. Sasa Yanga nasikia wanataka kuanza na kocha msaidizi, kisha ndo walete kocha mkuu. Kwa staili hii benchi la ufundi halitakaa litulie.

Ni wazo tu natoa kwa uongozi wa Yanga na wadhamini GSM
Tunachofanya yanga sawasawa unamkabizi kondaka daladala alafu kondo atafute dereva lazima Gari lichoke na hesabu zizingue. Hili jambo ndilo linalotupata wana jangwani FUTA BENCHI LOTE LA UFUNDI LISUKWE UPYA
 
Mkuu simba hata kama matatizo yapo hakuna prove kwamba yapo,matatizo ya simba kwa sasa hayawezekani kuonekana nje kiasi cha sisi kusema ina matatizo
Ila huwezi kutuambia eti Simba haina matatizo. Utakuwa unajidanganya. Yapo, mengi tu na ndiyo maana kuna viongozi.
Klabu haitengenezi faida halafu isiwe na matatizo?
 
Back
Top Bottom