- Source #1
- View Source #1
Nimeona mtandaoni Mkuu wa kitengo cha Digital, Crown Fm ameandika kuwa Mara ya mwisho Yanga SC kufungwa kwenye Ligi Kuu ni Oktoba 4, 2023 bado siku 3 itimize mwaka mmoja pasipo kupoteza mchezo kwenye Ligi Ligi Kuu ya NBC PL.
Eti wadau huyu anasema kweli au anatupanga maana huwa naona kama mnazi wa Yanga isijekuwa mapenzi ya timu yamefanya achakachue takwimu atupange.
JamiiCheck fanyenyi jambo tujue Ukweli.
Eti wadau huyu anasema kweli au anatupanga maana huwa naona kama mnazi wa Yanga isijekuwa mapenzi ya timu yamefanya achakachue takwimu atupange.
JamiiCheck fanyenyi jambo tujue Ukweli.
- Tunachokijua
- Young Africans S.C (Yanga) ni timu ya Mpira wa Miguu iliyoanzishwa mnamo mwaka 1935, inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara.
Mnamo 29, 2024 Septemba Yanga walishuka dimbani kucheza na timu ya KMC ambapo waliibuka na ushindi wa goli 1 kwa 0. Mara baada ya ushindi huo, Septemba 29, 2024 Benedict Anthony (Temidayo) ambaye ni Mkuu wa kitengo cha Digitali Crown Media Tanzania amechapisha kwenye ukursa wake wa X kuwa Mara ya mwisho Yanga SC kufungwa kwenye Ligi Kuu ni Oktoba 4, 2023 bado siku 3 itimize mwaka mmoja pasipo kupoteza mchezo kwenye Ligi Ligi Kuu ya NBC PL.
Je ukweli ni Upi?
JamiiCheck imepitia taarifa za matokeo ya Mechi msimu uliopita wa 2023/ 2024 na kubaini kuwa taarifa ya Yanga kufungwa mara ya mwisho Oktoba 4 na kwamba imebakiza siku 3 itimize mwaka bila kupoteza mchezo katika ligi Kuu ya NBC hazina ukweli.
JamiiCheck imebaini kwenye Mechi iliyochezwa Machi 17, 2024 katika mzunguko wa pili, Kati ya Yanga na Azam, Yanga alipoteza mchezo kwa kufungwa na Azam magoli 2 kwa 1, Mechi hiyo ilichezwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa, ambapo zimepita siku 197, sawa na Miezi 6 na siku 14 tangu Yanga kufungwa na Azam kwenye ligi Kuu ya NBC.
Aidha, ili kutimiza mwaka mmoja bila kupoteza mchezo Yanga imebakiwa na miezi 5 na siku 16 iwpo katika kipindi hiki haitapoteza mchezo wowote katika ligi kuu bara(Ligi ya NBC)
Funguakiungo hiki kutazama Magoli waliyofungwa Yanga na Azam mnamo Machi 17, 2024