Daniel Mbega
JF-Expert Member
- Mar 20, 2013
- 338
- 180
VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga, pamoja na mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati, Azam, leo wanajitupa viwanjani kucheza mechi zao za viporo vya ligi hiyo baada ya kuwa kwenye mashindano ya kimataifa.
Yanga, ambao ndio mabingwa watetezi, watakuwa kwenye Uwanja wa Taifa kuwakaribisha maafande wa Mgambo JKT katika mchezo unaotarajiwa kuwa mgumu kutokana na ukweli kwamba, mechi yao ya kwanza kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga Desemba 12, 2015 ilikuwa ya sare tasa.
Kwa habari zaidi, soma hapa => Yanga, Azam zatengewa viporo vya Ligi Kuu | Fikra Pevu