Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Picha za kutishaaa
bbf9775457be87c1f5638643f1079a40.jpg
 
TATHIMINI MECHI YA LEO KATI YA YANGA SC DHIDI YA TANZANIA PRISONS

Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara Yanga SC leo milango ya saa kumi kamili ndani ya uwanja wa Taifa watakuwa wenyeji wa Tanzania Prisons katika mchezo wao wa 26 ligi kuu nchini.

Yanga wanakwenda katika mchezo huu kama mbogo aliyejeruhiwa baada ya kupokea kichapo kwa Mbao FC katika mchezo wa nusu fainali ASFC.

Mara ya mwisho Yanga na Prisons zilikutana katika mchezo wa robo fainali ASFC na Yanga kushinda 3-0 magoli yakitiwa kambani na Obrey Chirwa, Saimoni Msuva na Amisi Tambwe.

Kambi ya Prisons imetamba kutoa upinzani mkali katika mechi ya leo ili wapate ushindi na kujiweka vyema katika msimamo wa ligi kuu. Baada ya kichapo cha 3-0 dhidi ya Yanga , walitimkia mjini Morogoro kwa ajili ya kambi maalumu kwa mchezo wa leo dhidi ya Yanga . Maandalizi haya yanaonesha jinsi gani walivyo dhamiria kuwatungua Yanga SC wenye kiu kali ya kushinda mechi ya leo ili kujiweka vyema kwenye mbio za kusaka ubingwa wa ligi kuu.

Tanzania Prisons wapo nafasi ya 10 katika msimamo wa ligi kuu wakiwa na alama 31 baada ya kucheza michezo 27 lakini anaeburusha mkia JKT Ruvu ana alama 23 na amebakiza mechi 3 sawa na Tanzania Prisons. Prisons akipoteza michezo yote mitatu iliyobaki kuanzia mchezo wa leo dhidi ya Yanga , atabaki na alama zake 31 ambazo zinaweza kufukiwa na timu sita chini yake akiwepo Ruvu kwa kufikisha alama 32 akishinda mechi zake zote tatu .

Mchanganuo huo unaipa ugumu sana mechi ya leo nakutoa taswira ya kuonekana ni mechi ngumu pande zote . Yanga wana alama 56 wakishinda mechi zao tano zilizobaki kuanzia leo , watafikisha alama 71 ambazo anaemfatia ( Simba SC ) hawezi kuzifikia . Yeye atakwamia alama 68! akishinda mechi zote tatu .

Utakuwa ni mchezo wenye tension kubwa kwa pande zote kuhitaji matokeo chanya . Tension ambayo inaweza kuleta burudani nzuri kwa kuona soka la ushindani kama wote wataamua kucheza mchezo wa kiungwana au kushuhudia mechi ya kukamiana na vurugu nyingi .

Tayari kocha msaidizi wa Yanga SC Juma Mwambusi ametanabaisha wanakwenda katika mechi hii kwa tahadhari kubwa na wametumia muda mwingi kuwajenga kisaikolojia wachezaji wao kuingia katika mchezo wa leo wakiwa watulivu kusaka ushindi pia kutambua dhamira ya klabu kusaka ubingwa kupitia michezo hii mitano iliyobaki .

" tumefanya mazoezi Geita na hapa Dar es salaam na vijana wameonesha uelewa mkubwa na kila mmoja ana kiu ya kuicheza mechi ya leo . Hii inatokana na nasaha zetu kisaikolojia pia mafunzo kimbinu na kiufundi kitu ambacho kimeongeza ari na morali ya kupambana . Kikubwa vijana waingie wakiwa na tahadhari kubwa na kuwaheshimu Prisons " alieleza Mwambusi jana akihojiwa na Yanga TV online.

Yanga wana faida ya kupona kwa mlinzi wao wa kati Vicente Bossou aliyeukosa mchezo wa nusu fainali FA jijini Mwanza . Bossou ndie mlinzi mnyumbufu kwa sasa katika nafasi hiyo akioana vyema na wenzake lakini mara nyingi anapokuwa hayupo , Yanga wanakuwa na ugumu wa eneo hilo .Kama bado Andrew Vicent hajajengwa kisaikolojia baada ya kujifunga Mwanza na kuingia katika migogoro ya mitandaoni na wadau wa timu hiyo , Ni dhahiri leo kati wanaweza kusimama Bossou na Nadir au Yondani kuzima kasi ya Prisons.

Bado Yanga wataendelea kuzikosa huduma za Donald Ngoma na Justine Zulu ambao ni majeruhi lakini uimara wa Niyonzima na Kamusoko unaifanya timu hiyo kutengeneza nafasi nyingi za kufunga kwenye safu ya ushambuliaji ambayo kwa sasa inaongozwa na Obrey Chirwa sambamba na Amisi Tambwe .

Prisons wanahitaji umakini kuwazuia Yanga kusaka ushindi leo endapo wataweza kuzuia mihimili ya ushambuliaji ya timu hiyo inayoanzia kwenye flanks na kiungo .

Juma /Kessy wote hawa wana uwezo wa kucheza kama wing backs na kupandisha mashambulizi ya kasi upande wa kulia wakishirikiana na Saimoni Msuva. Kama Prisons watawaacha kuvuka mstari wa kati wakiwa compact watawaumiza.

Mchezo uliopita Salumu Kimenya beki wa kulia wa Prisons alikuwa na kazi ya ziada kuzima mashambulizi ya Geofrey Mwashuiya ambaye hivi karibuni ameimarika vyema kwenye kipaji chake . Kimenya ni mzuri ila tatizo alikuwa ana mruhusu Mwashuiya asogee akiwa huru kitu ambacho kilikuwa kinamshinda pale winga huyo anapofanya maamuzi ya haraka kwenye final third.

Lwandamina atambue Prisons watakuja na mbinu ya kuufinya uwanja na kamwe hawatacheza open game hivyo kuna uwezekano mkubwa kujaza viungo kati na mbele wakamuacha striker mmoja kama " lone striker ' katika mfumo wa 4-5-1. Mzoefu Jeremiah Juma anaweza kupewa jukumu hili na mbinu zao zikasimama kwenye mashambulizi ya kushitukiza au kwenye mipira iliyokufa . Sare bado ni faida kwao lakini Yanga kwa asilimia 100 anazitaka alama 3.

Kujiandaa na approach hi ya Prisons GL hana budi kuimarisha kiungo chake . Hana haja ya kucheza kamari na safu yake kiungo kumwanzisha Makapu na Kamusoko kati , kazi hiyo awape Haruna na Kamusoko ili wawezi kufungua njia pale kati . Kamusoko anaweza kutumika kama box to box midfielder akilinda walinzi wa kati , kukaba na kuanzisha mashambulizi juu kwa kushirikiana na Niyonzima ambaye sifa yake kubwa ni holder na passer ila mwalimu anatakiwa kuwa mkali sana kwake kwa back passes zake . Mechi na Mbao aliigharimu timu kwa goli alilojifunga Dante baada ya yeye kurudisha mpira nyuma na Mbao kuunasa.

Samuel
 
Kikosi cha Yanga SC leo dhidi ya Kagera Sugar- VPL

1. Beno Kakolanya
2. Hassan Kessy
3. Haji Mwinyi
4. Kelvin Yondani
5. Nadir Haroub
6. Thaban Kamusoko
7. Saimoni Msuva
8. Haruna Niyonzima
9. Amisi Tambwe
10. Obrey Chirwa
11. Geofrey Mwashuiya

Akiba
Deogratius Munishi, Juma Abdul,Vincent Bossou, Matheo Antony, Deusi Kaseke , Emmanuel Martin na Said Makapu.
932c2a0ed6c7ef957982fc4c5ad823a0.jpg
 
Back
Top Bottom