Yang Feng Glan 'Malkia wa Tembo' apigwa kalenda kortini

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
3,158
2,000

Malkia%20wa%20Tembo.jpgIkiwamo kufanya biashara ya meno ya tembo yenye thamani ya Sh. bilioni 13 inayomkabili raia wa China, Yang Feng Glan 'Malkia wa Tembo' hadi Jumanne ijayo baada ya shahidi kuugua.


Jana kesi hiyo ilipangwa kuendelea kusikilizwa ushahidi wa upande wa Jamhuri mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi.


Wakili wa Serikali, Simon Wankyo alidai kuwa upande wa Jamhuri hauko tayari kuendelea kwa sababu shahidi wake ni mgonjwa. Aliomba mahakama kupanga tarehe nyingine ya kusikilizwa kesi hiyo.


Wakili wa utetezi, Nehemiah Nkoko alidai kuwa hana pingamizi na maombi ya Jamhuri.


Hakimu Shaidi alisema kesi hiyo itaendelea kusikilizwa Jumanne ijayo.


Mbali ya Glan, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Salvius Matembo na Philemon Manase.


Katika kesi ya msingi, Malkia wa Pembe za Ndovu, Manase na Matembo wanakabiliwa na mashtaka ya kujihusisha na biashara ya nyara za serikali kati ya Januari Mosi, 2000 na Mei 22, 2014 zenye thamani ya Sh. bilioni 13.


Washtakiwa hao wanadaiwa kuwa kati ya Januari Mosi, 2000 na Mei 22, 2014 walijihusisha na biashara ya nyara za serikali.


Katika kipindi hicho washtakiwa hao wanadaiwa kufanya biashara ya vipande 706 vya meno ya Tembo vyenye uzito wa tani 1.9 vyenye thamani ya Sh. bilioni 5.4 bila ya kuwa na leseni iliyotolewa na Mkurugenzi wa Wanyamapori.


Wanadaiwa kuwa kati ya Januari mosi, 2000 na Mei 22, 2014 kwa makusudi raia wa China, China, Yang Feng Glan aliongoza na kufadhiri vitendo vya kijinai kwa kukusanya na kusafirisha vipande hivyo 706 bila ya kuwa na kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyamapori.


Kwa upande wa washtakiwa Salvius na Manase wanadaiwa kuongoza makosa ya uhujumu uchumi kwa kusaidia biashara ya nyara za serikali kwa kukusanya, kusafirisha na kuuza meno ya tembo kwa nia ya kujipatia faida.


Aidha, ilidaiwa kuwa Mei 21, 2014 katika eneo la Sinza Palestina wilaya ya Kinondoni mshtakiwa Manase alitoroka chini ya ulinzi halali wa askari wa Jeshi la Polisi D 7847 Koplo Beatus ambaye alikuwa akimshikilia kwa makosa ya kujihusisha na biashara za nyara za serikali.


Chanzo: Nipashe


 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom