Yanayoweza kumfanya mumeo atembee na mashosti wako | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yanayoweza kumfanya mumeo atembee na mashosti wako

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by mito, May 3, 2012.

 1. mito

  mito JF-Expert Member

  #1
  May 3, 2012
  Joined: Jun 20, 2011
  Messages: 7,612
  Likes Received: 1,991
  Trophy Points: 280
  Wadau hii nimeipata mahali, nikaona si vibaya kushea na wanaJF.

  Ndugu zangu, maisha ya kimapenzi yanahitaji uvumilivu wa hali ya juu sana kwani kuna changamoto nyingi zinazoweza kujitokeza kiasi kwamba usipoangalia unaweza kuishia kusema hutakuja kumpenda mtu, heri uishi peke yako!

  Tatizo kubwa ambalo limekuwa likiwasumbua wengi walio kwenye ndoa na wale walio kwenye uhusiano wa kawaida ni usaliti. Uaminifu umepungua kwa kiasi kikubwa, mke wa mtu kutembea na rafiki wa mumewe si kitu cha ajabu siku hizi, mume wa mtu kutembea na mpangaji mwenzake siyo ishu. Nashindwa kuelewa tunaelekea wapi.

  Yaani imefika hatua ya mume wa mtu kutembea na ‘hausigeli’ wake tena anafanya hivyo kwenye kitanda anacholala na mkewe, hii si laana jamani? Usiulize kwa nini nimetoa mfano huu, hili limetokea juzi tu kwa mtu wangu wa karibu sana. Alitoka safari na aliporejea usiku akamfumania mumewe akiburudika na ‘hausigeli’, eti mwisho wa siku mwanaume anaomba asamehewe akidai ni shetani kampitia.


  Anyway nimeona nianze na hilo ambalo lina uhusiano wa kile ninachotaka kukizungumzia leo. Kama nilivyotangulia kusema hapo mwanzo, imekuwa si jambo la ajabu kusikia mume wa mtu katembea na rafiki wa mke wake.
  Wewe utakuwa ni shahidi wa hiki ninachokizungumza kwani kama hakijakutokea basi rafiki yako au ndugu yako kimempata.

  Lakini katika uchunguzi wangu nimebaini baadhi ya wake za watu wamekuwa wakitengeneza mazingira ya waume zao kutembea na marafiki zao.
  Unaweza kushituka kusikia hivyo lakini ndiyo ukweli wenyewe na utakubaliana na mimi baada ya kusoma vipengele vifuatavyo.


  1.Ukaribu wa mume na marafiki wa mke
  Kuna baadhi ya wanawake wamekuwa na tabia ya kuwaweka waume zao karibu sana na marafiki zao. Unakuta mwanamke eti anamruhusu mumewe kwenda klabu au baa na shosti wake. Katika mazingira hayo unatarajia nini?
  Sisemi uanze kumfikiria tofauti rafiki yako lakini unachotakiwa kujua ni kwamba, sasa hivi kuna wasichana micharuko ambao ukiwapa nafasi kidogo tu kwa mumeo wanakupindua.

  Kwa maana hiyo kitendo cha kumuweka mumeo karibu na mashosti wako unatengeneza mazingira ya kusalitiwa kwa kujitakia hivyo unatakiwa kuwa makini na watu ambao wanastahili kuwa karibu na laazizi wako.


  2. Mawasiliano ya mume na marafiki wa mke
  Sisemi marafiki zako wasiwasiliane kabisa na mumeo lakini unatakiwa kuangalia wanawasiliana kwa mambo gani? Utakuwa ni mtu wa ajabu kama utakubali mumeo apigiwe simu au achati na marafiki zako halafu hakuna cha maana wanachoongea, walahi utaula wa chuya!
  Unatakiwa kuwa mkali pale unapoona mumeo anawasiliana sana na marafiki zako wa kike kwani waliosalitiwa walianza kuchukulia poa mazingira kama hayo mwishowe wakalia.


  3. Mke kuanika siri za mumewe
  Lingine ni tabia ya baadhi ya wanawake kuwasimulia mashosti wao siri ambazo hawastahili kuzitoa nje. Kuna wanawake sijui nisema ni ulimbukeni au ushamba!
  Eti unamkuta mke anasimulia mashosti wake jinsi mumewe anavyompa furaha wanapokuwa faragha. Unajiuliza ni kwa nini mtu anafikia hatua hiyo.
  Kimsingi hili ni kosa kubwa linalofanywa na baadhi ya wanawake na kujikuta wakikaribisha usumbufu kwa waume zao kutoka kwa wanawake micharuko.


  4. Mwanamke kutochukua nafasi yake
  Kwa kifupi mwanamke kushindwa kumdatisha mumewe ni kumfanya aangalie wapi kwingine anakoweza kupatiwa kile anachokihitaji.
  Hili liwe fundisho kwa wanawake waliobahatika kuingia kwenye maisha ya ndoa. Kumridhisha mumeo ni kumfanya aepukane na vishawishi vinavyoweza kumfanya akusaliti.

  Mpe mapenzi atosheke asifikiria kukusaliti, mpe kila anachokitaka kutoka kwako (ila usimruhusu kuruka ukuta). Hii itamfanya asiwe na tamaa ya kupoteza muda wake kwa marafiki zako ambao ni micharuko wanaotamani kuonja asali yako.
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  May 3, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Acha atembee na mashost wangu
  Hawajui njia ya kwenda Mlimani City
  Wasije wakapotea bure.

  Akiten=mbea nao kawasaidia maana wao wako singo
  wasimchukue tu jumla
   
 3. Asabaya

  Asabaya JF-Expert Member

  #3
  May 3, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 1,317
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Nakubaliana na wewe hasa namba 4 wala sio uwongo wako wanawake wengine midomo yako hawaiwezi kabisa,na hawajua kama ni kosa kubwa sanaaa sito kaa nilifanye kwenye maisha yangu,utasikia ah mumewangu mie mambo anayaweza ananifanya hivi ananifanya vile yani unamuuza kiaina flani,na hakuna hata moja alolifanya aweze kumthibiti mumewe asitoke,
  usafi zero,mapishi uchafu mtupu,hapo kwenye sita kwa sita ndio gogo,loh mungu anistiri na wehu kama huo......
   
 4. vanilla

  vanilla JF-Expert Member

  #4
  May 3, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 218
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unaweza ukawa upo sawa.ila sababu kuu ni mtu kutokuwa commited kwenye ndoa yake.hzo sababu nyingne ni very minor.
   
 5. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #5
  May 3, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,276
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Kwa sie ambao hatunaga marafiki hiyo kitu haiwezi kutokea. Office mates wangu story na biashara nyingine zinaishia offisini. Najua kuwa na marafiki wakati ni mke wa mtu ni personality ya mtu; mi nashukuru Mungu am more of 'loner personality'
   
 6. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #6
  May 3, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Mwanaume hata uwe kama simba kutegwa kupo sema ni heshima tuu na soni hutufanya kushinda, alitegwa Mfalme Daudi, mfalme Solomon, mfalme Edward wa UK, raisi Clinton, Jacob Zuma, Tiger woods, ntakuwa mimi
   
 7. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #7
  May 3, 2012
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Sasa umeamua kumwaga rasmi mumeo kwa ajili ya yule mfanyakazi mwenzio, kumbuka naye anae mkewe!
   
 8. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #8
  May 3, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  wanasema hakuna urafiki kati ya mwanaume na mwanamke...watakua washkaji kwa mda flani ila ipo siku watabanjuana....
   
 9. farkhina

  farkhina Platinum Member

  #9
  May 3, 2012
  Joined: Mar 14, 2012
  Messages: 12,831
  Likes Received: 774
  Trophy Points: 280
  Topic nzr maana mashosti wa siku hizi macho juu.
   
 10. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #10
  May 3, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Hii habari ya kuwa na ukaribu wa marafiki wa mume au mke huwa sipendagi, ndio chanzo cha balaa.
   
Loading...