Yanayotokea sasa nchini na mabomu yale ya Arusha hayana utofauti

KAKADO

JF-Expert Member
Nov 8, 2012
230
336
Hakika hali yataharuki imeendelea kutanda nchini, tumesikia baadhi yawatanzania wakitekwa na wengine kuuwawa Kikatili, wapo waliokotwa mtoni na kuzikwa wapo waliopotea na mpaka leo hawajapatikana hali hii tukiangalia kwa makini haitofautiani na ile yaulipuaji mabomu iliyodumu kwa kipindi fulani kule Arusha.

Mabomu ya Arusha yalitunyanyasa na kutesa wengi hali iliyopelekea nyumba za ibada kupewa ulinzi mkali na serikali kwa kila anayeingia na kutoka.Matukio yale yaliwatoa mafichoni baadhi ya wanasiasa wakiokiri kuwajua wanahusika ila mpaka leo hawakudiriki kuwataja adharani (rejea kauli ya mh.Mboe mara baada ya bomu la soweto).

Ndugu zangu picha tunayoipata wahusika wa matukio yanayotokea sasa huenda hawatofautiani na wale Wa Arusha mbinu na Mikakati yao inashaabiana, kwa sasa wanaonekana ku deal na watu maarufu na sio kurusha mabomu kama ilivyowahi kutokea Arusha,huenda lengo ni kutia doa uongozi uliopo madarakani hali itakayowapelekea kupata huruma wa wanachii na kuwajengea chuki dhidi ya serikali yao.
Kundi hili la watu wa chache lipo kimaslahi binafsi bila kujali adhari zinazoweza kuipata nnchi mara baada yakushindwa kutawalika.

Nihabari njema kusikia Roma na wenzake wamepatikana ila
Serikali inapaswa kukomesha tabia hii kwa kuanza na hawa kina ROMA naamini wanaweza wakabanwa na kuwataja watekaji na mwisho wa siku tabia hii ikakoma kabisa..

Wasalaam
Brazado
 
Back
Top Bottom