Malalamiko yamezidi sasa katika kila kona na nyanja mbali mbali za maisha. Kuanzia wafanyakazi serikalini, wafanyabiashara wakubwa na wadogo, wakulima, wavuvi, wasomi, wanafunzi na walimu, wanaume na wanawake na mifano ya hio.
Lakini kwanini yote haya?. Je, imekuja hali hii kwa bahati mbaya? kwangu mimi HAPANA.
Ndio hapana, kwa sababu hakukuwa na maandalizi juu ya Taasisi ya Uraisi huu ndio ukweli.
Wengine wanaiita ajali, wengine wataita kukosa weledi, wengine wanaita hulka ilimradi yote hayo yanarudi kwenye neno KUKOSA MAANDALIZI.
Kuna watu hatutawasamehe kwa haya.
- Wale walioshiriki kutumia nyadhifa zao kuchochea kuvurugwa taratibu za kumpata mgombea aliyeandaliwa kwa kujali mirengo yao na visasi- hatutawasamehe wote.
- Wale wote waliotumika kufanikisha mpango huo wa kumpata Mteule asiyeandaliwa.
- Wale wote waliodiriki kutumia rasilimali mbali mbali ili kufanikisha mpango uliokosa maandalizi.
- Wale wote waliotumika kushawishi na kuwaaminisha watanzania kuwa kibaya kitakuwa kizuri wakati wanajuwa hakuna maandalizi yaliyofanywa.
- Wale wote waliotumika kwa kufanya upendeleo wowote ilimradi mteule asiye maandalizi aweze kupita kwa urahisi siku ya uchaguzi kama wapo.
- Waandamizi wote na wazoefu wa mfumo(system) ambao walinyamaza hata pale taasisi iliyotwaa ushindi , ilivuruga taratibu kwa uwazi wakati wa kumpata mteule wao.
- Waandishi wote waliotumika na kuacha uweledi wa kazi zao ili kupotosha ukweli ilimradi mtu aliyekosa maandalizi ashinde.
Hayo ni maoni yangu, naamini watanzania wengi leo hii wanajuwa ukweli wa hili. Awamu ya tano ilikosa maandalizi kutoka awali na hiki kinachoendelea leo ndio natija yake.
Tujifunze lakini tusirudie makosa, hata hivyo waliotukosea watuombe radhi au hatutawasamehe.
Kishada