Yanayoonekana kuwa Makosa ya Kiufundi wanayoyafanya CHADEMA na ACT - Wazalendo

KalamuTena

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
13,189
17,157
Inaeleweka kwa waTanzania wengi kwamba mwaka huu ni mwaka wa Uchaguzi Mkuu, ambapo waTanzania wanatakiwa wawachague viongozi wao wanaotaka wawaongoze ngwe nyingine ya miaka mitano.

Vyama vya siasa vilivyo makini, wakati huu ni wakati mhimu sana wa kuweka mikakati na mipango ya kupata ushindi kwenye uchaguzi huo.

Pamoja na ubovu wa CCM ilionao katika mambo mengine ya kuendesha nchi, lakini linapofika swala la kuhodhi madaraka siku zote wpo vizuri sana, mbali ya kuwa na mikakati ya kutumia njia zisizostahiri kupata ushindi.

Kwa upande wa vyama vya upinzani hali ni tofauti sana, angalau kwa kuangalia maandalizi yao ya kuikabili CCM.

Jambo mhimu ambalo vyama hivi vilitegemewa wawe wanalifanyia kazi kwa umakini mkubwa ni jinsi uchaguzi mkuu utakavyoendeshwa ili uonekane kuwa ni huru na wa haki. Kura za wananchi zihesabike kama walivyonuia wananchi hao.

Inajulikana kwa wengi kwamba moja ya jambo linalotakiwa kufanyiwa marekebisho ni Tume ya Uchaguzi, ili ionekane ni huru katika utendaji wake na itakapofikia kutangaza matokeo ya uchaguzi watangaze matokeo halisi na sio yale wanayoelekezwa kuyatangaza.

Sasa basi, makosa yanayoonekana kufanywa na hivi vyama vya upinzani ni kutoonekana wakilishughulikia hili jambo la tume huru. Hawa ndio wanaotakiwa kulishikia bango, ikiwa na pamoja na taasisi husika, ili wananchi waweze kuwa na ufahamu juu ya jambo hili mhimu.

Kwa sababu, wananchi ndio wanaoweza kuamua kwamba hapawezi kuwepo uchaguzi wowote bila kuwepo tume inayoaminika kutenda haki. Bila wananchi kulivalia njuga jambo hili, uchaguzi wowote ni kuipitisha tu CCM iendelee na raha zake.

CHADEMA walitangaza, 4/4/2020 kuanza shughuli; lakini inaelekea Coronavirus imewatoa kwenye mstari wao waliouchora.

Lakini haiwezekani shughuli za chama zikategemea mipango ya mikutano ya hadhara pekee ndipo ifanyike. Dunia ya leo mikutano ni nyongeza tu juu ya njia mbalimbali zinazoweza kutumika kuwafikia wananchi.

Sasa wanajua coronavirus itapita lini ndipo waanze kwenda kuwaeleza wananchi mambo mhimu wanayotaka kuwaelezea?

Tarehe ya uchaguzi ipo palepale, na tume isiyohuru ipo kwenye maandalizi tayari kuusimamia uchaguzi huo. Ina maana gani ya hivi vyama kuendelea kulaumu kama hawawezi kujimudu kufanya kazi wanayotakiwa kuifanya na wananchi.
 
Swala la Tume huru ilitakiwa waanze kulielezea kwa wananchi tangu mwanzo kabisa wa uongozi wa awam ya tano.Ila kwa muda uliopo sasa hv hata wakifanya mikutano washachelewa.Na Corona hii hapa,mbinu mbadala hakuna...
kuna nn hapo zaidi ya Magu kupenya tena
 
Swala la Tume huru ilitakiwa waanze kulielezea kwa wananchi tangu mwanzo kabisa wa uongozi wa awam ya tano.Ila kwa muda uliopo sasa hv hata wakifanya mikutano washachelewa.Na Corona hii hapa,mbinu mbadala hakuna...
kuna nn hapo zaidi ya Magu kupenya tena
Kwa maana hiyo sasa ni kwamba uchaguzi unaosogelea tayari umekwisha kamilika na mshindi anajulikana.

Safari hii wapinzani wakipata wabunge hamsini washukuru sana.
 
Back
Top Bottom