Yanayompata Ndugai ni onyo kwa wengine "usimchezee chatu(taasisi ya Urais), gongo usimtupie, utaukosa ushindi"

Wale waliodhani Wana deal na Samia, Sasa nadhani wanajua Wana deal na taasisi ya Urais moja kwa moja, taasisi hii ikifungua makucha yake, ni hatari sana.

Pale Kuna full squad ambayo imeapa kumlinda Rais na Urais dhidi ya chochote, pale ndio chem chem ya ulinzi na usalama wa nchi. Ni angalizo kwa watu aina ya Humphrey kwamba taasisi hii ikikufungukia, haina simile, inaweza kukujenga au kukubomoa kwa muda itakayo.

Ina vyombo vya Kila aina, watu wa Kila aina, wamezagaa Kila Kona ya dunia, acha Tanzania, Wana uwezo wa kumleta mtu yeyote mbele ya rais kutoka Kona yoyote ya nchi hii ndani ya muda mfupi saaana. Ndio maana wanasema "serikali Ina mkono mrefu"

Ukimchezea chatu, anajizungusha katika mwili wako, kinachofuata ni historia
Na washike adabu sasa , pumbavu zao,mda mrefu Sana wamemchezea Rais anawachora tuu na alikuwa anawaambia lakini wakaendeleza dharau,sasa kafinywa waliomtanguliza na wengine waropokaji wafinywe zaidi.

Mbowe aliambiwa awe na adabu haelewi subirieni moto.
 
Acha kutisha watu, hiyo taasisi kama ina nguvu imeshidwaje kupambana na umaskini na ujinga kwa miaka 60? Angalia taasisi kama hizo kwenye nchi za mashariki ya mbali
Kupambana na umaskini sio kazi ndogo, angali wewe binafsi tu umaskini wako umeshindwa kupambana nao, ukipewa upambane na umaskini wa taifa utaweza wewe?
 
Sijui kama ameshauriwa vizuri.yaani unaletwa na V8 au ile BMW na kurudi bila ulinzi.
Sidhani kama amepata ushauri,yaani ameachia mafao yake yote na kinga ya kutoshitakiwa.
Yaani kaachia mshahara wake wote na huduma za matibabu popote duniani?
Kisa mtu mzima kukataliwa msamaha,angekomaa tu wabunge wapate kazi za kuleta hoja na yeye atoe hoja hivi Tozo bajeti yake inatumika kufanya nini kama mkopo umemaliza shule zote?
 
Kwani Samia kamtisha nani? Si wamemchokoza wenyewe
NGONDOOO!
1641490242716.png
 
Kupambana na umaskini sio kazi ndogo, angali wewe binafsi tu umaskini wako umeshindwa kupambana nao, ukipewa upambane na umaskini wa taifa utaweza wewe?
Sina umaskini, hapa nipo nakula bia na mbuzi katoliki
 
Huyu Mama ni suala la muda tu ila cases za wakosoaji wake kufanyiwa fujo tutazishuhudia kwenye utawala wake.
 
Kwamba mhimili wa serikali unashinikiza spika wa bunge kujiuzulu... Na yeye anajiuzulu kwa kuandika barua kwa katibu wa ccm...
Katiba yetu ina mapungufu makubwa sana...
Ipo siku rais atalazimisha tujiuzulu kuishi...
 
Wale waliodhani Wana deal na Samia, Sasa nadhani wanajua Wana deal na taasisi ya Urais moja kwa moja, taasisi hii ikifungua makucha yake, ni hatari sana.

Pale Kuna full squad ambayo imeapa kumlinda Rais na Urais dhidi ya chochote, pale ndio chem chem ya ulinzi na usalama wa nchi. Ni angalizo kwa watu aina ya Humphrey kwamba taasisi hii ikikufungukia, haina simile, inaweza kukujenga au kukubomoa kwa muda itakayo.

Ina vyombo vya Kila aina, watu wa Kila aina, wamezagaa Kila Kona ya dunia, acha Tanzania, Wana uwezo wa kumleta mtu yeyote mbele ya rais kutoka Kona yoyote ya nchi hii ndani ya muda mfupi saaana. Ndio maana wanasema "serikali Ina mkono mrefu"

Ukimchezea chatu, anajizungusha katika mwili wako, kinachofuata ni historia
TOKA Bwana na maneno mepesi, elewa nchi yoyote zipo mifumo hata Rais hajui, wapo watu mtandao wao mkubwa hata Rais hajui , ACHA lisha watu ujinga, kwamba mtu ameamua jiuuzulu ndo mapambio yote ? Kuna watu tz wamewai jiuuzulu na badae kuwa watu wakubwa tu , kujiuzulu ni busara kubwa kuliko Jambo lolote sema Afrika ndo inaonekana ajabu
 
Nguvu ya Rais haipimwi kwa kuingilia mihimili mingine.Nguvu ya Rais huwa inapimwa kwa kuleta maendeleo ya watu,haki,demokrasia na uhuru wa watu kwa kasi.

Rais ambae hataki mihimili mingine kuwa huru na ifanye kazi zake ni hopeless fool.
Ungemlaumu Ndugai kwanza kwa kulewa sifa na kuwa arrogant. Muda wote anayo spirit ya ushindani na ninaweza kuamini maneno kwamba anautaka urais ingawa sio dhambi hata kidogo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom