Yanayojiri: Uzinduzi wa mbio za Mwenge wa uhuru 2021, Umewashwa na makamu wa pili wa Rais Zanzibar utakimbizwa siku 150!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,725
141,592
Mwenge wa uhuru umewashwa leo mjini Zanzibar na makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar mh Ameir.

Kiongozi wa mbio za mwenge ni luteni Josephine Mwambushi na ataukabidhi ukiwa unawaka siku ya tarehe 14/10/2021 kwa Rais wa JMT mh Samia Suluhu Hassan huko Chato, Geita.

Source: ZBC
 
Hili zindiko la mwenge ndilo linalotuongezea TU umaskini watanzania.

Hapa Watu wataambukizana Corona, ukimwi na magonjwa ya Kila Aina, Kila eneo ili dubwasha litakapopita.

Cha ajabu,
Kuna watu humu wanafaidika na hili zindiko, watakuja kulitetea
 
Hili zindiko la mwenge ndilo linalotuongezea TU umaskini watanzania.

Hapa Watu wataambukizana Corona, ukimwi na magonjwa ya Kila Aina, Kila eneo ili dubwasha litakapopita.

Cha ajabu,
Kuna watu humu wanafaidika na hili zindiko, watakuja kulitetea
Hama nchi mkuu ili usiambukizwe corona na ukimwi
 
Huu mwenge tangu uzinduliwe Miaka zaidi ya 50 iliyopita.

Unatumia gharama KUBWA Sana mpaka zoezi kukamilika nchi nzima.

Ila Hauleweki kabisa unamsaidia vipi mtanzania wa kawaida kuzitatua changamoto zake za maisha ya Kila siku.
 
Vipi na Mwenge wa Olympic nao ni ushirikina au kwa kuwa ni wa wazungu!!? Slavery Mentalic inakuhusu wewe dada!!
Usifananishe Olympic na hii jimshumaa lenu la kienyeji.

Olympic ilo pale kwa lengo la kuibua vipaji mbalimbali hasa vya michezo yote dunia nzima.

Nikuulize wewe,
Huo mwenge Wako unawashwa na kutembezwa kwa lengo gani
 
Zaman ilikua wanasema, Mwenge Ni kwa ajili ya kuzindua miradi.

Cha kushangaza,
Miradi kalibia yote mwendazake Kila alikopita alkua anazindua Kila kitu, adi choo Cha stendi anakizindua.

Sasa mwaka huu,
sijui mradi gani tena mtazindua.

Labda mtuambie mtazindua DISKO na KIGODORO Kila kata
 
Walimu (Mawakala wa kudumu wa kulinda kura) wajipange makato ya Lazima kuchangia Mwenge ili 'umulike hadi nje ya Mipaka na ukomeshe ubeberu na unyonyaji'

1.Rais wa Kwanza …Mwalimu
2.Rais wa Pili …Mwalimu

3.Rais wa nne …Mwalimu wa Jeshini na Mkewe Mwalimu

5.Rais wa Tano…Mwalimu Mtata na Mkewe Mwalimu
6. Rais wa sita… Mumewe alikuwa Mwalimu Chuo kikuu na Baba yake Mzazi alikuwa Mwalimu

Ualimu na uongozi wa juu wa nchi yetu ni kama maji na damu mwilini yaan 'lila na fila…'

Walimu wana bahati sana
 
Mwenge una umuhim mkbwa Sana .Ni ishara ya taifa kuendelea kuwa Nuru,namaanisha uendelevu wa taifa .Manake bado taifa linaishi.Tatizo Ni jinsi labda unavokimbizwa Kama vile galamu zinakua kubwa na wengine humo Ni wapigaji .Lakini mwenge Ni mhimu kuliko mnavojua wengi wenu.
Hili swala Ni la kiroho zaidi
 
Back
Top Bottom