Yanayojiri sherehe za kuadhimisha miaka 39 ya kuzaliwa CCM uwanja wa Namfua Singida

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,950
29,532



Leo February 06, 2016 ni sherehe za maadhimisho ya chama cha mapinduzi kutimiza miaka 39 tangu kuundwa kwake, sherehe hizi zinafanyika katika viwanja vya Namfue mkoni Singida. Miongoni mwa waliopo ni Rais wa jamhuri ya muungano Tanzania, ndugu John Pombe Magufuli, Rais mstaafu, ndugu Jakaya Mrisho Kikwete, makamu wa Rais na waziri mkuu.

Alieanza kuongea ni katibu mkuu wa chama cha mapinduzi, AbdulRahman Kinana baada ya kukaribishwa na Nape Nnauye. Kwa sasa anaeongea ni Rais wa Jamhuri, Rais John Magufuli.

Magufuli: Leo sio siku yangu ya kutoa hutuba, leo ni siku ya bosi wangu, mheshimiwa mwenyekiti wetu wa chama cha mapinduzi, chama tawala ambapo sisi viongozi tunatekeleza ilani ya chama cha mapinduzi. Lakini nataka nichukue nafasi hii chanya ambayo nimepewa niwashukuru wananchi wa Singida na watanzania kwa ujumla kwa kunipa kura nyingi na kuwa Rais wenu.

Napenda kukuthibitishia mwenyekiti wetu, mimi pamoja na serikali ninayoiongoza tutaendelea kukienzi chama cha mapinduzi na tutatekeleza ilani ya uchaguzi ili wananchi wote waweze kuondolewa kero zao. Na nitoe wito kwa watendaji wote wa serikali, watendaji wote wa serikali kuanzia juu mpaka chini, anaejijua ni mtendaji wa serikali ana jukumu moja tu la kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi.

Asieweza atupishe pembeni, uwe mkuu wa wilaya, tekeleza ilani ya CCM, uwe katibu tarafa, wewe uko ndani ya CCM kwa sababu tunaoteua ni sisi, mimi ni Rais lakini ni Rais niliechaguliwa na chama cha mapinduzi. Kwa hio nitoe wito kwa watendaji wa serikali ambao wanapokuwa kule wanajifanya wao ni watendaji wa serikali, wajue serikali hii inaongozwa na Rais mwana CCM ambae yuko hapa kwa ajili ya kutekeleza. Nilitaka hili niliweke wazi, tumedhamiria kufanya kazi na ninasema tutafanya kazi kwelikweli na ndio maana kauli yetu ni hapa kazi tu lakini pia imeungwa mkono na chama changu na mheshimiwa mwenyekiti kwamba kazi ipo pale.

Hata katika maandiko matakatifu yanasema asiefanya kazi na asile, kwa hio nataka nikuhakikishia mheshimiwa mwenyekiti. Serikali ninayoiongoza ambayo ukweli serikali hii nimepewa na chama cha mapinduzi, kisingekuwa chama chama mapinduzi mimi nisingekua Rais.

Na ndio maana leo nimevaa nguo yangu ya kijani nimependeza, inafurahisha na ninatembea kifua mbele nikijua mimi ni mwana CCM.

Wale wengine ambao wanategemea siku moja watakuja kuitawala hii nchi ni marufuku kwa sababu katika kazi wanazozifanya na wananchi hicho na wananchi ndicho hicho wanachotaka kukipata, tutakitekeleza ili wananchi mawazo ya kufikiria vyama vingine yaishe kabisa. Hata kama wana tabia ya kuota-ota, wasiote kabisa kufikiria mavyama mengine.

Hakuna mtawala yeyote anaependa kutawaliwa na bahati mbaya atawaliwe na vyama vya hovyo hovyo, vya ajabu ajabu, kwa hio napenda kukuhakikishia mwenyekiti wangu sisi ndani ya serikali tumejipanga kutekeleza yale yote tunayotakiwa kutekeleza na ambayo yapo kwenye ilani ya uchaguzi.

Tulisema lazima wanafunzi wasome bure, ni kweli tumepata changamoto kubwa kwa sababu kabla ya hapo wanafunzi waliokuwa wanaingia darasa la kwanza saa nyingine walikuwa hawafiki sabini lakini imejitokeza katika shule nyingine unakuta wanafunzi 600 mpaka 900.


===============
Tarehe 6 mwezi wa pili 2016 CCM mpya inaadhimisha miaka zaidi ya 39 ya kuzaliwa kwake.

Sherehe za mwaka huu ni za aina yake kwa kuwa CCM imeweza kufanya maamuzi magumu ya kufuta mtandao uliousumbua toka mwaka 1995?? na hatimaye ikamuweka mgombea urais ambaye ni mzalendo kwa lengo la kukirudisha chama kwa wafanyakazi na wakulima na waadilifu.

Kuna mengi yamesemwa juu ya uwepo wa makundi ndani ya chama hata baada ya Rais Magufuli kushika hatamu.

Kuna wanaosema kuwa kuna mvutano kati ya Rais Magufuli na mwenyekiti wa sasa wa CCM kwani Magufuli anaonekana kama ni candidate aliyepita kwa bahati mbaya baada ya msuguano wa kambi mbalimbali zilizoundwa ndani ya CCM.

Kuna wanaosema kuwa Magufuli anashindwa kutekeleza majukumu yake kiserikali kwa kuwa sio Mwenyekiti wa CCM kwa sasa na anapangiwa majukukumu au kuzuiwa kufanya yale aliyoyataka kwa uhuru kwa kuwa hajashika uenyekiti wa CCM.

Zipo kauli kadhaa za Magufuli na Kikwete zinazotafsiriwa na watu kuwa ni ishara za wazi kuwa kuna mvitano ndano ya CCM hqsa kati ya Mwenyekiti na Rais!

Pia kuna suala tata sana kuwahi kutokea tangu kuundwa kwa CCM nalo ni mkwamo wa uchaguzi katika visiwa vya Zanzibar.

Tunategemea yote hayo niliyoyasema yatatolewa tamko zito na mkutano huu wa Chama Tawala na kikongwe Africa!

Rais Magufuli ameelekea Singida kwa njia ya barabara huku akisimamishwa mara kadhaa na wananchi waliomueleza shida mbalimbali...ni sherehe zake za kwanza kama Rais wa JMT na mwenyekiti mtarajiwa kuhudhuria sherehe hizi huku kukiwa na shauku ya wananchi na wanaCCM wazalendo wakitaka kusikia kauli zake !

CCM OYEE!!

Stay tune for updates
 
"Hakuna Chama Tawala kinachopenda kutoka madarakani..." - John Magufuli, Feb. 5 2016!
 
Niko nasikiliza hotuba ya JK katika sherehe ya maadhimisho ya siku ya kuzaliwa ccm huko Singida.
Hotuba za JK zinaonekana ziko lightweight sana, anaongea vitu ila viko simple simple sana kulinganisha na hotuba za rais Magufuli.
 
  • Thanks
Reactions: MTK
Niko nasikiliza hotuba ya JK katika sherehe ya maadhimisho ya siku ya kuzaliwa ccm huko Singida.
Hotuba za JK zinaonekana ziko lightweight sana, anaongea vitu ila viko simple simple sana kulinganisha na hotuba za rais Magufuli.
 
Ok, kwahiyo hili ndiyo mnaligundua leo? Tulipo waambia Kikwete ni dhaifu mlitetea kwa ngumi na mateke.
 
Niko nasikiliza hotuba ya JK katika sherehe ya maadhimisho ya siku ya kuzaliwa ccm huko Singida.
Hotuba za JK zinaonekana ziko lightweight sana, anaongea vitu ila viko simple simple sana kulinganisha na hotuba za rais Magufuli.

Mipasho, kejeli na dharau tupu. Ndio silika ya mkwere!
 
Back
Top Bottom