Yanayojiri Mwanza Mjini: RC, DC na CD hawataweza tena kukalia ofisi zao

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,797
71,215
FM Radio zote za jijini Mwanza sasa hivi ni mjadala wa maamuzi ya Rais na zinawekwa Clip za matamko ya Mkuu wa mkoa, Mkuu wa wilaya Nyamagana na Mkurugenzi (CD) wa jiji kuhusu suala la wamachinga waliyotoa siku zilizopita kuhusu suala hilo na kuonekana kuwa walikuwa tofauti kabisa na hiki alichosema Rais.

Hata mbunge wa Nyamagana alipohojiwa amepata nafasi ya kuwaruka kabisa viongozi hao kiasi cha kuonyesha maamuzi yao yalikuwa yao pekee kwa nia ya kukomoa Wamachinga na mama ntilie.

Hii ni fedheha kubwa sana kwa wateule hao wa kisiasa na kiutendaji na wanakosa kabisa sifa ya kuendelea kuwaongoza watu wa Mwanza kwa siku zijazo kwani hawawezi tena kuwa na maamuzi ambayo yatakuwa yamesimama bila kudharauliwa.

Je, wataamua wenyewe kujiuzulu ili kulinda heshima zao au watataka waendelee kufanya kazi kama picha tuu? Maana kila anayehojiwa mtaani anawaponda na kuwadharau kuwa kazi imewashinda ndio maana aliyewateua kaamua kuifanya mwenyewe.
 
Tanzania hii kuna viongozi wanafanya 'madudu' na hakuna hata mmoja wa kujiuzulu mwenyewe. Mpaka watumbuliwe..

Mfano ni huku mkoa wa Pwani ambako mkuu wa wilaya ya Kisarawe anabariki uporaji wa ardhi ya wakulima maskini na kuwapa wafugaji wenye pesa. Na wala mkuu huyo wa wilaya hatajiuzulu wala nini.
 
Ukifanya kazi na JPM utegemee sana KADHIA za namna hii.

Haoni shida hata kukugeuka hata kama hilo jambo lilikuwa limekubaliwa collectively na ninyi viongozi wote.

Kwa mfano angeweza kuizuia hii operesheni kwa kutoa maelekezo kimya kimya kwa Waziri au RC na hili Zoezi likasimama bila kuwadharaulisha hawa wateule wake kwa wananchi.

Lakini kaamua tamko alitoe mwenyewe kabisa kupitia kurugenzi yake ya mawasiliano.

Huku ni kutafuta cheap popularity.
 
HATOWEZA KUWAONDOA kati ya vitu ambavyo Pomb@ anaogopa ni ASKALI yaani unapotaja neno askar mbele yake...yupo tayari kukuhonga ata nch... ndo maana ajira nyingi kipaumbele ni haohao...watumishi hewa kote wametafutwa ila makambini thubutu....kwahiyo maRC,DC na wengine msihofu mmepona........Waiter ZUNGUSHAAAAAAAA.....
 
Tunahitaji kuwa na mpango kabla kufanya jambo. Kwa mtazamo kwenye ITV huweze kuupeleka umati wote ule mahali kwa mpigo kuwapangia vitalu/ vizimba vya biashara. Ilitakiwa kuwepo ramani tayari imeshaandikwa majina ya wahusika. Hii ilitakiwa wapewe viongozi wa kila Machinga group na kuwaonyesha eneo husika. Othrer wise it was not well planned and coordinated.
 
Hii ni aibu ya kufungia mwaka 2016. Mbona m mukuru alikua na nafasi ya kuwazuia mapema tu kwann asubili hadi shughuli ikamilike ndio atoe tamko hilo? Hapa MTU mwenye akili timamu ni kujua kuwa hutakiwi, ondoka. Aibu, aibu mikogo na majigambo yenu mtayaficha wapi? Aibu kwa MKUU wa wilaya ya nyamagana, ilemela, wakurugenzi wa halmashauri hizo, MKUU wa mkoa, mkurugenzi wa jiji, waziri wa tamisemi na naibu wake. Ondokeeeni,aibu!!!!!!???
 
Hii iliyofanyika ni timing ya kutafuta mashabiki,unapigwa katafunua na mama ukishaumia baba ndio anakusaidia
 
Hebu nimnukuu Mwandishi Kondo Tutindaga katika Mwanahalisi la Jumatatu Decemba 5-11,2016, anaposema, "...lakini kwa hulka yake na matendo yake, ni dhahiri aweza kuwa anafurahia mateso ya watu. Ni mtu anayemkanyaga mtu na mtu huyo akilia, rais aweza kuwa anacheka kwa furaha"
Nimeyatafakari sana maneno hayo ya Mwndishi Kondo. Pamoja na ukweli kuwa ustawi wa Machinga ni muhimu, lakini je, hakukuwa na njia nyingine ya kufikisha ujumbe wa kusitisha zoezi hadi iwe ni lazima kuwadhalilisha viongozi hawa?
Sasa ninaanza kuamini kuwa tuna kiongozi mwenye hulka ya kutaka sifa bila kujali kuwa kwa kufanya hivyo anawaumiza wengine!!!
 
Mimi sijui niko upande gani kwenye hili coz naona faida ya kuwepo hawa wafanyabiashara mjini na pia bado naona faida ya kuwepo sehemu ya pamoja.
Geez, aaaaaaaahhhh
 
Tanzania hii kuna viongozi wanafanya 'madudu' na hakuna hata mmoja wa kujiuzulu mwenyewe.
Mpaka watumbuliwe..
Mfano ni huku mkoa wa Pwani ambako mkuu wa wilaya ya Kisarawe anabariki uporaji wa ardhi ya wakulima maskini na kuwapa wafugaji wenye pesa. Na wala mkuu huyo wa wilaya hatajiuzulu wala nini...!!!
Kwani mkuu wa Wilaya anamlaka ya kisheria kugawa/kuuza ardhi? Au mihemuko yako tu
 
Back
Top Bottom