Yanayojiri Mwanza Mjini: RC, DC na CD hawataweza tena kukalia ofisi zao

Walidhani wanamfurahisha bhana mkubwa, c walizoea kujipendekeza pendekeza, sasa Mkuu kawaumbua
 
Katika maneno ambayo utayatafuta saana kwenye kwenye kamusi ya CCM na usiyapate ni KUJIUZULU!
 
Ukifanya kazi na JPM utegemee sana KADHIA za namna hii.

Haoni shida hata kukugeuka hata kama hilo jambo lilikuwa limekubaliwa collectively na ninyi viongozi wote.

Kwa mfano angeweza kuizuia hii operesheni kwa kutoa maelekezo kimya kimya kwa Waziri au RC na hili Zoezi likasimama bila kuwadharaulisha hawa wateule wake kwa wananchi.

Lakini kaamua tamko alitoe mwenyewe kabisa kupitia kurugenzi yake ya mawasiliano.

Huku ni kutafuta cheap popularity.
atoe tamko kmyakmya ili asipate KIKI
 
Kumbe nchi hii yote ni kichwa cha mwendawazimu! Mtu anatoka hukoo anajifunzia hapo kunyoa..... Ding dong >> ding dong...
 
HATOWEZA KUWAONDOA kati ya vitu ambavyo.wanaogopa ni ASKALI yaani unapotaja neno askar mbele yao...yupo tayari kukuhonga ata nch... ndo maana ajira nyingi kipaumbele ni haohao...watumishi hewa kote wametafutwa ila makambini thubutu....kwahiyo maRC,DC na wengine msihofu mmepona........Waiter ZUNGUSHAAAAAAAA.....
Hakuna ambako hajagusa sema askari wananidhamu zao hawawezi kuropoka ila anawaudhi kwa sabaabu nothing is moving kwa mfano mpaka sasa hakuna anayejuwa kutakuwa na sherehe za tarehe tisa huku askari wako kwenye gwaride kwa kupenda sifa wa Magufuli kama amiri jeshi mkuu amefikia hata hasikilizi ushauri wa mageneral ,
 
Apa ma DC,RC na DO wa nchi nzima watazubaazubaa maofisini mwao Yani watagoma hadi 2017 March ndo tutawasikia
 
Sidhani kama kwa desturi ya Africa na wabongo kama kuna mwenye ujasiri wa kusutwa na nafsi akaamua kustep down bali wote wanasali tu wasitumbuliwe na mkuu wao.

Lakini kwa hili walipaswa kushuka chini na kuachia ngazi zao maana bosi ameshapoteza kabisa confidence nao.
 
Lakini hao machinga si walipewa notice? Au
Tatizo hapa sio hao Wamachinga kuondoka bali ni hao wateule kusubiriwa wametimiza wajibu wao kisha anakuja kutengua na kusema wamachinga warudi.

Hapo tayari wamachinga wameingia hasara kubwa kwa kuharibiwa miundo mbinu yao na serikali imepoteza fedha nyingi kugharamia shughuli hiyo, wakati kama alikuwa hataki angeweza kuzuia baada tuu ya ile notice ya kuwaondoa ilipotolewa.

Hii ni kama yale ya sherehe za mwenge Simiyu, kasubiri mpaka waalikwa wameshafika Bariadi kisha anasema sherehe hakuna na watu warejeshe fedha zote walizochukua wakati walishatumia kusafiria.

Hao viongozi wa Mwanza wataweza kufanya kazi hapo Mwanza tena baada ya kuaibishwa namna hii?
 
Rais wetu atupie macho huku Leguruki kuna mteule wake anatuhumiwa kuwanyanyasa wananchi sana
 
kama mtu ana dignity ya ukweli hapo ni kujiuzulu tu, ni kama yule mke wa Lukuvi alipoachia ngazi baada ya kusimangwa hadharai ila hawa hawana kazi nyingine sijui
Yani kama mtu una hela zako ni bora ujiuzulu amewaaibisha mno naona wanajuta huko walipo duh ni aibu kubwa angewaambia kimya kimya nao wangejua wafanyaje duh nmewaonea Huruma mno
 
polsi muache viherehere mzee kawambia mnatumiwa vibaya, mtaingia kwenye matatizo kwa kuwa endekeza wanasiasa
 
Hapa kwa ajili ya aibu msamiati huo utakuwepo. Naziona dalili za magari yao yakipita maeneo ya wamachinga kuzomewa.

mku chakaza huku africa ukipata cheo ndio umetoka kimaisha. Utambue kwa kupitia hayo madaraka ndio wanakaa nyumba nzuri, wanapeleka watoto shule nzuri tena wakati mwingine nje ya nchi. Wanatumia magari mazuri kwa gharama za serekali, nje ya hayo madaraka wanageuka ombaomba. Je katika mazingira hayo unatarajia wajihuzulu? Mi bora wadharauliwe wakiwa madarakani kuliko waheshimiwe bila madaraka. Na hilo ninalokuambia ni kuanzia mkuu kabisa mpaka wa chini.
 
FM Radio zote za jijini Mwanza sasa hivi ni mjadala wa maamuzi ya Rais na zinawekwa Clip za matamko ya Mkuu wa mkoa, Mkuu wa wilaya Nyamagana na Mkurugenzi (CD) wa jiji kuhusu suala la wamachinga waliyotoa siku zilizopita kuhusu suala hilo na kuonekana kuwa walikuwa tofauti kabisa na hiki alichosema Rais.
Hata mbunge wa Nyamagana alipohojiwa amepata nafasi ya kuwaruka kabisa viongozi hao kiasi cha kuonyesha maamuzi yao yalikuwa yao pekee kwa nia ya kukomoa Wamachinga na mama ntilie.
Hii ni fedheha kubwa sana kwa wateule hao wa kisiasa na kiutendaji na wanakosa kabisa sifa ya kuendelea kuwaongoza watu wa Mwanza kwa siku zijazo kwani hawawezi tena kuwa na maamuzi ambayo yatakuwa yamesimama bila kudharauliwa.
Jee wataamua wenyewe kujiuzulu ili kulinda heshima zao au watataka waendelee kufanya kazi kama picha tuu? Maana kila anayehojiwa mtaani anawaponda na kuwadharau kuwa kazi imewashinda ndio maana aliyewateua kaamua kuifanya mwenyewe.
Hawa wateule wake wamedhalilishwa mno,yule aliyewakosoa watoto Wa Obama USA, alijiuzulu,hawa waliodhalilishwa na boss wako,wamekataa kuachia ofiv,ngoja waisome namba ya jpm
 
Alaf Rais anasemakua Polisi wanatumika vibaya wakati yeye ndo anawatumia,Magufuli ivi wakati mwingine unawekawapi Akiliyako?
Kama anawaongoza watu kama ninyi ambao hata kuandika sentensi ni taabu kwanini asipete????
 
FM Radio zote za jijini Mwanza sasa hivi ni mjadala wa maamuzi ya Rais na zinawekwa Clip za matamko ya Mkuu wa mkoa, Mkuu wa wilaya Nyamagana na Mkurugenzi (CD) wa jiji kuhusu suala la wamachinga waliyotoa siku zilizopita kuhusu suala hilo na kuonekana kuwa walikuwa tofauti kabisa na hiki alichosema Rais.
Hata mbunge wa Nyamagana alipohojiwa amepata nafasi ya kuwaruka kabisa viongozi hao kiasi cha kuonyesha maamuzi yao yalikuwa yao pekee kwa nia ya kukomoa Wamachinga na mama ntilie.
Hii ni fedheha kubwa sana kwa wateule hao wa kisiasa na kiutendaji na wanakosa kabisa sifa ya kuendelea kuwaongoza watu wa Mwanza kwa siku zijazo kwani hawawezi tena kuwa na maamuzi ambayo yatakuwa yamesimama bila kudharauliwa.
Jee wataamua wenyewe kujiuzulu ili kulinda heshima zao au watataka waendelee kufanya kazi kama picha tuu? Maana kila anayehojiwa mtaani anawaponda na kuwadharau kuwa kazi imewashinda ndio maana aliyewateua kaamua kuifanya mwenyewe.
mkuu hivi bado hujagundua kuwa the whole thing ni Isidingo tupu? hakuna atakayefukuzwa hapo.

siku hizi mambo ni "kiki" kwa kwenda mbele baada ya watu kuanza kulia njaa huku mitaani na vijijini!
 
Back
Top Bottom