Yanayojiri: Leo Tarehe 11/12/2013. Bungeni Dodoma

kiwatengu

Platinum Member
Apr 6, 2012
17,456
14,383
Kikao cha bunge ndiyo kimeanza dakika chache zilizopita..

Kipindi cha maswali na majibu sasa.
 
wizara ya Serikali za Mitaa, ndiyo wanajibu maswali ya wabunge sasa

kibiti wanadai mji mdogo na Mombo ni lini watapewa halmashauri ya mji..

Ghasia anasema vigezo vikifikiwa vitafanyiwa kazi...
 
kama tutangoja serikali na sera zake katika mazingira basi tuhesabu hatuna mazingira----A.Makinda(spika wa bunge)

hii kauli ina prove kuwa sera za serikali ya ccm ni ovyo na hazitekelezwi.
 
Kangi Lugola anamkosoa Ghasia hapa, juu ya uundwaji wa Wizara maalumu kwa ajili ya Walimu..

TAMISEMI inachangia walimu kuhangaika..

Ghasia anasema yeye hafahamu vigezo vya kuanzisha wizara maalumu..

Anasema matatizo ya walimu yamepungua kwa kiasi kikubwa sana walivyoamishiwa TAMISEMI.
Anasema hebu walimu waulizwe kama wanaridhika huko waliko.
 
hivi hakuna link ya mtandao inayoweza kutusaidia kufuatilia matangazo ya bunge moja kwa moja kwa njia ya mtandao?

Kuna kipindi ARUSHA MAMBO RADIO walikuwa wanarusha matangazo haya lakini siku hizi hamna kitu
Tafadhali mwenye kujua link ya mtandao inayoweza kutupatia uhondo huu naomba aweke hapa tufuatilie
 
huyu jamaa ni mtupu sana kichwani aisee, anasema Tanzania wailazimishe Uganda kutumia bandari ya Dar kulipa madeni..

huyu jamaa kweli ni mtupu aisee..
Nahodha kashamuumbua sasa!!

itakua poa kama bunge lingekua linaanza saa 1 usiku had saa 5 maana limekua ni kama sehem ya burudan,na muda huo ndo murua maada watz tutakua tunapumzisha vichwa kwa kuchekeshwa na watu kama akine Komber
 
Lugola anamaind hapa ni kwanini Mawaziri wanawataka kuwashauri wakati wa maswali.

Spika anasema ni sahihi lakini wabunge siyo wavumilivu.
 
Hoja za kamati zinaanzwa kujadiliwa hapa...

List ya wanaojadili kwa wakati huu ndiyo inasomwa
 
Misanga sasa anaanza mchango wake...

as usual anaanza kwa kupongeza kamati kwa kutimiza majukumu yao.

yeye anasema kwa ujumla.
anasema kuna nidhamu mbaya sana ya matumizi ya serikali
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom