Yanayojiri kutoka Arusha kwenye Mkutano Mkuu wa kuchagua Viongozi wa Kanda ya Kaskazini.

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
Baraza la Uongozi la (CHADEMA) Kanda ya Kaskazini linaketi leo Novemba 30, 2019 Jijini Arusha, Kufanya Uchaguzi wa Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Mwekahazina.
IMG-20191130-WA0000.jpg
IMG-20191130-WA0002.jpg


IMG-20191130-WA0003.jpg


IMG-20191130-WA0003.jpg


Wagombea nafasi ya Uenyekiti kanda ya Kaskazini Kuna Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema na Mbunge wa Jimbo la Rombo Joseph Selasini.
.......Updates.
Tayari baadhi ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wameshawasili ukumbini kwa ajili maandalizi kufanya uchaguzi.
IMG-20191130-WA0017.jpg

IMG-20191130-WA0019.jpg



IMG-20191130-WA0022.jpg
IMG-20191130-WA0020.jpg

Tayari Mwenyekiti wa Chadema Taifa Mhe Freeman Mbowe pamoja na wagombea wamefika ukumbuni.
IMG-20191130-WA0037.jpg



Matokeo Kanda ya Kaskazini
1.Mwenyekiti
Godbless Lema - 78 (Mshindi)
Joseph selathini - 23

2.Makamu Mwenyekiti
Yosepha Komba 76
Bahweje- 23
Emmanuel-5
Japhary - 1

3.Mwekahazina
Anna Gideria - 68 (Mshindi)
Prisca Kinabo - 35
Bahati David - 2
Salimu marijani (Alijitoa)
Msimamizi wa Uchaguzi Kanda ya Kaskazini Mhe.Halima Mdee ametangaza Matokeo ya Uchaguzi uliofanyika leo Novemba 30, 2019 katika Baraza la Uongozi la 6 lililoketi Jijini Arusha ambapo Mhe.Godbless Lema ametangazwa kuwa Mshindi wa nafasi ya Uenyekiti Kanda ya Kaskazini, Mhe.Yosepher Makamu Mwenyekiti pamoja na Mhe.Anna Gidarya Mweka hazina.
 

Attachments

  • IMG-20191130-WA0039.jpg
    IMG-20191130-WA0039.jpg
    58.6 KB · Views: 3
Safi sana makamanda kila la heri. Najua Kamanda Shana na vijana wake watakuwa viunga vya uzunguni hapo ili kuleta mtafaruku. Kuweni makini
 
Kuna kitu nimetonywa
Namtakia Godbless Lema ushindi mnono kwenye huo uchaguzi wa kanda
 
Leo unafanyika uchaguzi Mkutano Mkuu wa kuchagua Viongozi wa Kanda ya Kaskazini Uchaguzi huo unafanyika katika ukumbi wa Corridor Springs Hotel jijini Arusha timu ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya utangazaji tumefika ukumbini kuwaletea yanajiri kutoka ukumbi.
Picha ni maandalizi yakiendelea ukumbini.
View attachment 1276809View attachment 1276810

View attachment 1276811

View attachment 1276812

Wagombea nafasi ya Uenyekiti kanda ya Kaskazini Kuna Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema na Mbunge wa Jimbo la Rombo Joseph Selasini.
Wataangalia nani ni Mangi!
 
Hayo matumizi mabaya ya pesa, kupiga kura mnapamba kiasi hicho?!
Nani kakuambia kila linalofanywa na Chadema ni kwa pesa za chama?
Watu wana mapenzi mema sana na chama chao hivyo usishangae mwanachama wa kawaida kusema atagharamia mapambo au vinywaji.
Na mapenzi hayo ndio yamesababisha Serikali ya ccm kushindwa kuiua Chadema kama njama zao zilizo anza 2010 zitakavyo.
Hiyo ndio Peoples Power!
 
Kura kwa 30 , uongozi utawanyike,sio viongozi watoke asili moja. (Lema+mbowe --- Palestinians)
 
Mnafanya uchaguzi au maigizo?? Mbowe kishamchagua anayemtaka hapo, hakuna jipya!
 
Back
Top Bottom