Yanayojiri kesi ya Lissu leo-Lissu ambana shahidi

Isango

R I P
Jul 23, 2008
295
450
[h=1]YANAYOJIRI KESI YA LISSU LEO-LISSU AMBANA SHAHIDI..[/h][h=1]Mbunge wa jimbo la Singida mashariki, Mh. Tundu Lissu, ameiomba mahakama kuu inayosikiliza kesi yake ya kupinga matokeo ya uchaguzi kufutilia mbali utaratibu wa kuvua ushahidi. Hayo yamejitokeza leo asubuhi kufuatia shahidi wa 15, Musa Rajabu Mkanga kuanza kuzungumza vitu vipya kabisa ambavyo havipo katika tuhuma za mwanzo walizokuwa wanamtuhumu Tundu Lissu. [/h][h=1]Hata hivyo Wakili wa serikali waserikali Bw. Juma Ramadhani alimuunga mkono na kusisitiza kuwa Mahakama Kuu iwe mahakama ya sheria, isiwe kama Gachacha..................[/h][h=1]Akina mama wajazana mahakamani kusikiliza kesi ya Lissu.[/h][h=1]Kesi ya Tundu Lissu inaendelea na akina mama wengi sana wameingia mahakamani wakitokea Ikungi kuja kumsikiliza, wengi sana mpaka inatia huruma.[/h][h=1]Mojawapo ya mahojiano ya Lissu na Shahidi yapo hivi: TUNDU LISSU ANAMHOJI.[/h][h=1]T/L. Naomba utusaidie kuzungumza, Cleti Kidamwina na pikipiki yake. Ieleze mahakama je Pikipiki ni T799 BJP. Ndo unayosemea?[/h][h=1]NDIYO.[/h][h=1]Umesema pikipiki hii ni mali ya Cleti Kidamwina?[/h][h=1]Namwonaga nayo.[/h][h=1]Wewe ni M/Kiti wa Kijiji. Unafahamu au unafikiri?[/h][h=1]Nafahamu.[/h][h=1]Je ni sawa au si sawa, kuwa pikipiki ni nyekundu na Nyeusi?[/h][h=1]Ni Nyekundu na Nyeusi.[/h][h=1]T/L. Unamfahamu Joshua Gwae kama mchungaji wa kanisa?[/h][h=1]Namfahamu kama Mwanakijiji wangu, ila ana kanisa lililopo Unyamikumbi, na anaishi Unyaghumpi.[/h][h=1]Ndiyo.[/h][h=1]Unamfahamu Juma Said Daa?[/h][h=1]Ndiyo[/h][h=1]Hao wamesema pikipiki ya Cleti Kidamwina ni nyekundu. Wewe unasema ni nyekundu na nyeusi, nani ni mwongo.[/h][h=1]Mwongo simjui, ila nasema ninachojua mimi.[/h][h=1]T/L nikisema huu ushahidi wa Cleti Kidamwina ni wa kutunga, ni uzushi. Nikikwambia Cleti hajawahi kumiliki pikipiki, utasemaje?[/h][h=1]Nitasema aliwahi kuwa nayo[/h][h=1]Jaji, naomba nimwonyeshe hati ya pikipiki T 799 BJP, ambayo anasema ni ya Cleti Kidamwina.[/h][h=1]Pikipiki ni Mali ya Salehe Ally Dude.[/h][h=1]Unakubaliana?[/h][h=1]Sikubali.[/h][h=1]Umesema pikipiki hiyo ni nyekundu na Nyeusi ni kweli au si kweli?[/h][h=1]NDIYO.[/h][h=1]Mbona hati ya usajili inaonyesha ni nyeusi?[/h][h=1]Kwanini umeamua kuidanganya mahakama?[/h][h=1]SIJUI.[/h][h=1]Kwa hiyo ushahidi uliotolewa na mchungaji Joshua, na wa kwako na Daa ni wa uongo?[/h][h=1]Wenzako wamesema pikipiki ilikuwa nyekundu, hati inayonyesha pikipiki ni nyeusi kwanini Mnadanganya........ Sijui.[/h][h=1] [/h][h=1] [/h]
 
unanifurahisha sana staili yako ya kuripoti...

endelea ,mkuu..!
 
Waache kutupotezea mda hawa , wamwache Mbunge afanye kazi yake maana tuna uchaguzi mdogo Songea na Shinyanga Mjini unatusubiri
 
YANAYOJIRI KESI YA LISSU LEO-LISSU AMBANA SHAHIDI..

Mbunge wa jimbo la Singida mashariki, Mh. Tundu Lissu, ameiomba mahakama kuu inayosikiliza kesi yake ya kupinga matokeo ya uchaguzi kufutilia mbali utaratibu wa kuvua ushahidi. Hayo yamejitokeza leo asubuhi kufuatia shahidi wa 15, Musa Rajabu Mkanga kuanza kuzungumza vitu vipya kabisa ambavyo havipo katika tuhuma za mwanzo walizokuwa wanamtuhumu Tundu Lissu.

Hata hivyo Wakili wa serikali waserikali Bw. Juma Ramadhani alimuunga mkono na kusisitiza kuwa Mahakama Kuu iwe mahakama ya sheria, isiwe kama Gachacha..................

Akina mama wajazana mahakamani kusikiliza kesi ya Lissu.

Kesi ya Tundu Lissu inaendelea na akina mama wengi sana wameingia mahakamani wakitokea Ikungi kuja kumsikiliza, wengi sana mpaka inatia huruma.

Mojawapo ya mahojiano ya Lissu na Shahidi yapo hivi: TUNDU LISSU ANAMHOJI.

T/L. Naomba utusaidie kuzungumza, Cleti Kidamwina na pikipiki yake. Ieleze mahakama je Pikipiki ni T799 BJP. Ndo unayosemea?

NDIYO.

Umesema pikipiki hii ni mali ya Cleti Kidamwina?

Namwonaga nayo.

Wewe ni M/Kiti wa Kijiji. Unafahamu au unafikiri?

Nafahamu.

Je ni sawa au si sawa, kuwa pikipiki ni nyekundu na Nyeusi?

Ni Nyekundu na Nyeusi.

T/L. Unamfahamu Joshua Gwae kama mchungaji wa kanisa?

Namfahamu kama Mwanakijiji wangu, ila ana kanisa lililopo Unyamikumbi, na anaishi Unyaghumpi.

Ndiyo.

Unamfahamu Juma Said Daa?

Ndiyo

Hao wamesema pikipiki ya Cleti Kidamwina ni nyekundu. Wewe unasema ni nyekundu na nyeusi, nani ni mwongo.

Mwongo simjui, ila nasema ninachojua mimi.

T/L nikisema huu ushahidi wa Cleti Kidamwina ni wa kutunga, ni uzushi. Nikikwambia Cleti hajawahi kumiliki pikipiki, utasemaje?

Nitasema aliwahi kuwa nayo

Jaji, naomba nimwonyeshe hati ya pikipiki T 799 BJP, ambayo anasema ni ya Cleti Kidamwina.

Pikipiki ni Mali ya Salehe Ally Dude.

Unakubaliana?

Sikubali.

Umesema pikipiki hiyo ni nyekundu na Nyeusi ni kweli au si kweli?

NDIYO.

Mbona hati ya usajili inaonyesha ni nyeusi?

Kwanini umeamua kuidanganya mahakama?

SIJUI.

Kwa hiyo ushahidi uliotolewa na mchungaji Joshua, na wa kwako na Daa ni wa uongo?

Wenzako wamesema pikipiki ilikuwa nyekundu, hati inayonyesha pikipiki ni nyeusi kwanini Mnadanganya........ Sijui
 
Nadhani huyu wakili wa upande wa ccm ni mwana-CHADEMA damu damu, haiwezekani kukawa na wakili mweupe kiasi hiki, at least mashahidi wanaonesha hivyo.
 
Lazima CCM tufidie kiti cha Arumeru kwa kiti Singida au DSM au Arusha

...ndiyohiyo

naona maumivu ya kupigwa kule Arumeru bado yanakuletea kizunguzungu, tulia kwanza kama wenzako wakina Ribosome/Faiza Foxy, Rejao, Ritz and co
 
Nadhani huyu wakili wa upande wa ccm ni mwana-CHADEMA damu damu, haiwezekani kukawa na wakili mweupe kiasi hiki, at least mashahidi wanaonesha hivyo.

Tatizo la ccm vilaza wengi! Isitoshe, kutetea kitu usichokiamini ni ngumu sana!
 
Kama ccm in mwanasheria, basi ama amesahau taaluma yake na kugeukia uchama zaidi ama ccm haimpi nafasi ya kushauri kisheria ama ni kilaza tu.
 
watu wazima hovyo hivi wanapewa sh ngapi,unajua unanunua aibu ya maisha na vitakataka vdogo ambavyo havina msingi,upuuzi embu waache watu wafanye mambo ya maendeleo
 
Back
Top Bottom