Yanayojiri katika utoaji wa maoni katiba mypa Zanzibar,CCM waanza kupoteza dira

Malaria Sugu

JF-Expert Member
Jul 7, 2009
2,653
264
Maoni leo asubuhi WELEZO: Waliotaka Zanzibar iwe na mamlaka kamili kitaifa na kimataifa na kisha kuwa na Muungano wa Mkataba kati yake na Tanganyika ni 49; Waliotaka muundo wa sasa wa Muungano wa Serikali Mbili uendelee lakini ufanyiwe marekebisho ni 40; Waliotaka Serikali Moja ni 1; na ambao hawakufahamika ni 1.
Maoni leo jioni MWANAKWEREKWE IJTIMA’I: Waliotaka Zanzibar iwe na mamlaka kamili kitaifa na kimataifa na kisha kuwa na Muungano wa Mkataba kati yake na Tanganyika ni 44; Waliotaka muundo wa sasa wa Muungano wa Serikali Mbili uendelee lakini ufanyiwe marekebisho ni 35; na ambao hawakufahamika ni 1.
NYEPESI NYEPESI ZA LEO: Pamoja na maoni hayo, kuna matukio mawili yaliyojitokeza leo yanafaa ku-share na wengine.
LA KWANZA: Hili limetokea asubuhi Welezo ambapo Mzee Warioba alikuja kujumuika na wana-Tume iliyopo Zanzibar. Mwana-Mkataba mmoja alihoji vipi Wazanzibari waendelee na mfumo uliopo wakati nafasi zote kubwa kubwa katika mihimili mbali mbali ya Dola zinashikwa na watu wa Tanganyika tu. Mzee Warioba kama kawaida yake huwa hawezi kustahamili mawazo yasiyokubaliana na yake, akamwambia hivi hajui Tume ya Katiba Makamu Mwenyekiti wake ni Mzanzibari? Mwana-Mkataba akamjibu hivi huyo Jaji Agostino Ramadhani hana sifa za kuwa Mwenyekiti na wewe ukawa chini yake? Mzee Warioba akagwaya. Kimya!
LA PILI: Hili limetokea jioni Welezo. Mwana-Mkataba mmoja alipozungumzia Zanzibar kuwa na mamlaka kamili na Rais wa Zanzibar awe na hadhi kamili kama Mkuu wa Nchi ndani na nje. Mwenyekiti wa Timu iliyopo Zanzibar, Prof. Mwesiga Baregu akamwambia hivi sasa Rais Shein yupo Vietnam, kenda kama Rais. Mwana-Mkataba akamjibu kenda kama Rais lakini baada ya kupata kibali cha Waziri Benard Membe na kumuuliza na Rais wa nchi gani anayehitaji kibali cha Waziri ili apokelewe kama Rais? Prof. Baregu akabaki kimya!

SOURCE: MZALENDO.COM
 
Kuna kitu sikielewi labda wadau mtufahamishe.
Kwani ni Tume ya kukusanya maoni ya Katiba, au ni Tume ya kukusanya kura za maoni ya Katiba mpya?
 
asante mkuu, kwa kweli nimefurahi sana kwa hizo nyepesi mbili ulizotuwekea, pili nashukuru kuwa sasa tunapata mwelekeo na maono ya wa zanji wengi juu ya muungano tulionao.
kinachonisikitisha ni kuwa hayo maoni yao sijui kama yatafikiriwa kwa sababu hayapo kwenye hadidu za rejea. au wali-include kipengele cha kuujadili muungano?
 
Back
Top Bottom