Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,444
- 7,801
Kampeni za urais zinaendelea na leo mgombea Urais kupitia chama cha mapinduzi, Dkt yuko Urambo. Kwa sasa aneongea ni Magreth Sitta na anawaombea kura madiwani, Rais na yeye mwenyewe kwenye nafasi ya ubunge kwa kupiga magoti mara tatu kwa kila nafasi.
3:28 Asubuhi: Dkt. Magufuli amewasili uwanjani na viongozi wa dini wanachukua nafasi yao ambao wamewakilishwa na Sheikh Zaid Nassor, Sheikh wa wilaya ya Urambo ambae anawaombea wagombea wote wapate wepesi katika safari yao, baba Paroko Edward Mtunge kutoka kanisa Katoliki Urambo analiyemuombea Rais Magufuli aendelee kuliongoza Taifa kwa salama na kuwaombea wapate kura mbunge na madiwani wa CCM na mwisho alimaliza Mchungaji Alfred kutoka Morovian na yeye aliliombea amani Taifa katika kipindi cha kampeni na kukiombea chama cha mapinduzi.
===================
Mmesikia kwenye Kampeni za hivi karibuni mnaambiwa yatatengenezwa Majimbo,Tanzania itagawanywa ni Chama fulani kina sera yake hiyo ya kuigawanya Tanzania katika Majimbo ya Utawala, ukishatengeneza Majimbo katika Nchi huo ndio mwanzo wa mfarakano”-JPM akiwa Urambo
Ukishagawanya Nchi katika Majimbo ni mwanzo wa ufarakano kwasababu kila Jimbo litakuwa linajitegemea lenyewe likiwa masikini linakuwa masikini wa kutupwa, Nyerere alipokuwa akiomba Uhuru wa Taifa hili angeligawa kwenye Majimbo tusingefikia hapa”-JPM akiwa Urambo
Tanzania tuna Makabila zaidi ya 121, Nyerere alituweka Watanzania kama Taifa moja, tangu 1961 hatujaingia mfarakano kati ya Kabila na Kabila, Dini na Dini, Maeneo, sitaki nitoe mifano ya baadhi ya Nchi ambazo ziliingia kwenye mtego wa Majimbo na wamefarakana”-JPM
Msisikilize maneno ya watu, mti wenye matunda ndiyo unapondwa mawe na watoto, hata mimi hapa mnasikia yanayozungumzwa juu yangu, tumehangaika tumeomba wote na Corona ikapotea na wao wakatukimbia lakini wakija hapa wanatutukana