Yanayojiri EU na Unabii wa Sanamu ya Nebukadneza

CharmingLady

JF-Expert Member
Apr 16, 2012
18,250
12,868
Habari za jioni wana jamvi,

Mimi sio mwandishi mzuri, ila ninachokiona, kusikia na kutizama duniani ni dhahiri kwamba Unabii wa Daniel sura ya 2 unatimia.

Wakristo wengi wanakifahamu kitabu cha Daniel hasa sura ya pili nzima inaongelea nini... Kwa kifupi nanukuu mistari hii kisha connect dots utaelewa.

Daniel 2:41 Na kama vile ulivyoziona hizo nyayo za miguu na vidole vyake, kuwa nusu udongo wa mfinyanzi, na nusu chuma, ufalme ule utakuwa ufalme uliogawanyika; lakini ndani yake zitakuwako nguvu za chuma, kama vile ulivyoona kile chuma kimechanganyika na udongo wa matope. 2:42 Na kama vidole vya zile nyayo vilikuwa nusu chuma na nusu udongo, kadhalika ufalme ule utakuwa nusu yake una nguvu, na nusu yake umevunjika. 2:43 Na kama vile ulivyokiona kile chuma kimechanganyika na udongo wa matope, watajichanganya nafsi zao kwa mbegu za wanadamu; lakini hawatashikamana, kama vile chuma kisivyoshikamana na udongo.

Kwa atakayeona haina mantiki apite tu. Ni mtazamo wangu binafsi.

CL
 
EU inatajwa vema sana katika unabii japo kwenye yule mfalme mwenye nguvu haimo ila inatajwa kupitia miguu ya sanamu (Daniel 2:42) ambayo mfalme Nebukadreza aliota ambapo aliona jiwe ambalo alikuchongwa na kazi ya mikono ya mwanadamu likiigonga ile sanamu na kupasuka vipandex2.

Hapo ndipo hiyo EU ya uingereza inayojitoa inaposemwa, so charminglady upo njiani kwenye kutoa elimu muswano. Thanks
 
Hekaya za Ellen G White.....

Hivi kweli inamaana hujui sababu za UK kujitoa EU...Punguzeni kudanganyana kwenye lessoni..
 
EU inatajwa vema sana katika unabii japo kwenye yule mfalme mwenye nguvu haimo ila inatajwa kupitia miguu ya sanamu (Daniel 2:42) ambayo mfalme Nebukadreza aliota ambapo aliona jiwe ambalo alikuchongwa na kazi ya mikono ya mwanadamu likiigonga ile sanamu na kupasuka vipandex2.

Hapo ndipo hiyo EU ya uingereza inayojitoa inaposemwa, so charminglady upo njiani kwenye kutoa elimu muswano. Thanks
Hivi unajua dhima ya vitabu hivi vyenye masimulizi ya ki-epokaliptiki....?? Unajua chimbuko lake..? Au unabwabwaja tu hapa...
 
Karibuni wana wa elen g white. Nabii aliyepagawa na mapepo
Mkuu hawa watu huwa wananiacha hoi...Yani hili kanisa lao kazi kubwa ni kutabiri vitu ambavyo hata havipo na kila wanapotabiri wanaangukia pua..

Kumbuka kipindi cha Great Disappointment na utabiri wa Miller uliokuja kupewa baraka zote na Kibibi Ellen G White....Yalitokea maangamizi makubwa ambayo dunia haitokaa kusahau..
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom