Maswali na Majibu
Swali: Je serikali ina mpango gani wa kukamilisha vituo vya afya Mima na Mboli katika jimbo la Mpwapwa?
Majibu: Serikali imetenga shilingi milioni 15 katika mwaka wa fedha 2016/17 kukamilisha kituo cha Mima. Aidha serikali imetenga kiasi cha shilingi milioni 35 kwa ajili ya kukamilisha kituo Mboli.
Swali: Je serikali ina mkakati gani kuwasaidia watoto kuepukana na ajira za watoto kwa upande wa Zanzibar
Majibu: Mpango wa TASAF umewaandikisha kaya 31,331. Mpango huu umesaidia kupatiwa chakula, elimu na kazi kwa wanakaya wakijihusisha na miradi midogomidgo.
Mpango wa TASAF umesaidia watoto kuhudhuria shule kwa asilimia 80 na kuepuka na ajira za utotoni.
Swali: Wakulima wa Rufiji wameibiwa milioni 900 kwa mwaka 2011. Ni lini serikali itawachukua hatua wahusika?
Majibu: Viongozi 41 wa wilaya ya Rufiji walihusika, mrajisi aliwaandikia hati ya madai ya zaidi shilingi milioni 68. Mpaka sasa shilingi milioni 24 zimerejeshwa.
Swali: Ni lini serikali itawahakikishia wakulima kuwa watapata malipo yao halali ya korosho kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani?
Majibu: Ni kweli kuna baadhi ya wakulima hawajapata malipo yao. Aidha kuna wakulima waliopunjwa salio la bonasi yao na serikali inafanya uchunguzi kubaini waliohusika na kuwachukulia hatua. Serikali imejipanga kupitia bodi ya korosho kuwaelimisha wakulima.
Swali: Tangu kuanzishwa kwa wilaya ya Simajiro haijawahi kupata huduma maji safi, ni lini serikali itatekeleza ahadi ya serikali ya awamu ya nne ya kuwapatia maji?
Maji: Mradi huu unatekelezwa kwa msaada wa BADEA na OFID. Mradi utagharimu kiasi cha dola za kimarekani milioni 18.4, serikali ya Tanzania inachangia kiasi cha dola za marekani milioni 2.4. Mradi utatekelezwa kwa awamu mbili.
Maboresho ya mradi yamewasilishwa BADEA. Awamu ya pili itaanza kutekelezwa hivi karibuni, katika bajeti ya mwaka 2016/17, serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 2 kutekeleza mradi huo. Mradi huu ukikamilika utahudumia wananchi 52,000
Swali: Je serikali itakuwa tayari kulipa fidia kwa wananchi waliopisha mradi wa maji katika jimbo la Singida mjini?
Majibu: Serikali imekamilisha uhakiki na kiasi cha shilingi bilioni 1.5 zimetumwa. Pia serikali inaendelea na uhakiki wa kiasi cha shilingi bilioni 2.6 na punde ukikamilika wananchi watalipwa.
Swali: Je ni lini serikali itaanzisha mpango wa maji safi na salama kwa wananchi wa Mlimba?
Majibu: Serikali inatekeleza miradi ya maendeleo ya maji katika halmashauri ya zote nchini.
Miradi nane kati ya hii ipo katika halmashuri ya manispaa ya Kilombero. Miradi hii imewahudumia wananchi 24,622. Serikali inaendelea na kukamilisha miradi ambayo bado haijakamilika.
Swali: Ni lini wananchi wa Geita watarudishiwa eneo lao walilonyang'anywa na GGM?
Majibu: Wananchi wanaomiliki ardhi eneo la mgodi wanaendelea na shughuli zao kama kawaida. Aidha wananchi waliotoa ardhi kwa mgodi huo tayari washalipwa fidia.