Yanayojiri Bungeni Dodoma: Leo Jumatano, Tarehe 26 Novemba, 2014

Status
Not open for further replies.
Duh kweli hii nchi inaendeshwa kibabe yan mtu analihairishia bunge kinyemela hivyo..
 
Sasa kama hawajapata order ya kusimamisha siwangewasilisha ripoti? Sasa kusubiri mpaka jioni si ndio kutoa nafasi ya kuwasilishwa kwa order? Ok kumbe! Halafu jioni wanarudi na sound kwamba tumeshakuwa-served hatuwezi kuendelea mpaka mahakama iamue. Tukirudi mahakamani kesi itatajwa tarehe 4/5/2015 maana majaji wanaenda likizo, watarudi Februari halafu wana kazi nyingi. Lakini kesi ya PAP inafunguliwa siku hiyo hiyo, inapangiwa majaji watatu siku hiyo hiyo, insikilizwa siku hiyo hiyo, na inatolewa uamuzi siku hiyo hiyo!! RUSHWA NI ADUI WA HAKI - NYERERE (RIP).
 
Kama wangekuwa na nia, wangeijadili sasa na kuendelea baadae. Kwamba hawajapokea court order kwa hiyo wameipa muda ije?? Huu usanii wa ajabu sana!
 
Hahah! Nani wa kufa peke yake? Nilijua tu! Hapo report itasomwa jioni vizuri kama ratiba ya bunge inavyosema ila wahusika watakuwa wameshapata chambo kwa wale watawala wanaopinga hii ishu.

Wataitwa mchana huu, watapigwa biti na fitna kwa sanaa, jioni wakirudi escrow itajadiliwa kinyongee na wachache wengi watakuwa na hofu ya kupoteza dhamana zao!

Ma-strategia wa huu mzozo wako vizuri, ila wawe na back-up plan manake lolote laweza kutokea manake muda wa kukaa madarakani ndio unaisha! Ni kuchagua kulinda vimaslahi viduchu vilivyobakia au kujijengea jina,heshima na uzalendo kwa Taifa lao.

Kazi bado mbichi, tutaona mood za wabunge wa chama tawala jioni watakuwa vip??? Wataleta amsha amsha kama sasa au ndio wata nywea!

Sent from my WhiteBerry using JamiiForums
 
Saa kumi na moja ifikapo utasikia bunge imepokea stop order mjadala hautajadiliwa!!pumbav sana!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom