Chabruma
JF-Expert Member
- Sep 19, 2013
- 5,660
- 1,777
Wadau, ni matumaini yangu kuwa hamjambo na mnaendelea vema na jukumu la kusukuma gurudumu la familia na taifa. Nami pia namshukuru Mungu na nina afya njema tayari kuwaletea yanayojiri kwenye bunge la Bajeti. Leo ni Kikao cha 15 Mkutano wa 15. Jana Waziri wa Ujenzi John Pombe Magufuli alifanikiwa kuwashawishi wabunge wote bila ya kujali itikadi zao na hivyo kuweza kupitisha makadirio ya wizara yake kwa kishindo. Hii ni mara ya kwanza kwa wabunge wote kuweza kupitisha bajeti ya serikali na hii inaashiria kuwa hata wabunge wa upinzani wameanza kukubali kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya CCM.
Leo baada ya kipindi cha maswali na majibu, Waziri wa Afrika ya Mashariki, Sammuel Sitta atawasilisha makadirio ya Wizara yake kwa mwaka 2014/2015. Aidha, baada ya wabunge kupitisha bajeti ya Wizara hiyo, Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi atawasilisha makadirio ya Wizara yake. Naamini kuwa tutakuwa pamoja katika kuwahabarisha Watanzania juu ya kile kinachojiri hapa bungeni Dodoma.
**********UPDATES**************
*Nchi wanachama zimekamilisha mfumo wa forodha ya himaya moja kwa kutumia mfumo wa kielectronic wa kufuatilia bidhaa (Electronic cargo tracking system). Lengo ni kupunguza gharama za kufanya biashara katika nchi za afrika mashariki, kupunguza muda wa kusafirisha mizigo, kupunguza gharama na kuboresha ufanisi wa bandari zetu.
*thamani ya mauzo ya biashara za Tanzania na nchi wanachama wa Afrika ya mashariki. imefikia dola za kimarekani milioni 1120. Bidhaa zilizoongoza kwa mauzo ni pamoja na mashine mbalimbali
* Vikwazo 11 kati ya 33 vimeondolewa ambavyo ni pamoja na msongamano wa bidhaa kwenye bandari ya Dar na kulipaia bidhaa mara mbili.
*vituo vya ukaguzi wa miziko kwenda Rwanda, Burundi na DRC vitapunguzwa kutoka 15 hadi 3 ambavyo ni Vigwaza mkoani Pwani, Manyoni Singida na Nyakanazi
*maandalizi ya katiba ya Shirikisho la Kisiasa yameanza. Hii ni baada ya nchi wanachama kukamilisha mazungumzo ya model ya Shirikisho hilo la kisiasa
* Nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika ya Mashariki zimetakiwa kufungua mipaka yake ili kurahisisha biashara na jumuiya nyingine kama vile za SADC na COMESA
* Zanzibar imechaguliwa kuwa makao makuu ya lugha ya Kiswahili ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki
*Hospitali na Chuo kikuu cha Afya na Tiba cha Muhimbili kimeteuliwa kuwa kituo cha Tiba ya Magonjwa ya Moyo ya EAC
* Majadiliano yanaendelea ili Pass ya kusafiria ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki itumike kimataifa miongoni mwa nchi wanachama. Huenda utaanza kutumika Nobemba 2015
*Maombi ya Sudani ya Kusini kujiunga na EAC yataanza kujadiliwa Septemba 2014 mara baada ya serikali ya nchi hiyo kutoa elimu kwa umma kwa wananchi wake juu ya umuhimu wa kujiunga ha jumuiya hii