Yanayojiri Bungeni Dodoma: Alhamis 22 Mei 2014, Kikao cha 15 Mkutano wa 15, Bunge la Bajeti

Chabruma

JF-Expert Member
Sep 19, 2013
5,661
1,250
Wadau, ni matumaini yangu kuwa hamjambo na mnaendelea vema na jukumu la kusukuma gurudumu la familia na taifa. Nami pia namshukuru Mungu na nina afya njema tayari kuwaletea yanayojiri kwenye bunge la Bajeti. Leo ni Kikao cha 15 Mkutano wa 15. Jana Waziri wa Ujenzi John Pombe Magufuli alifanikiwa kuwashawishi wabunge wote bila ya kujali itikadi zao na hivyo kuweza kupitisha makadirio ya wizara yake kwa kishindo. Hii ni mara ya kwanza kwa wabunge wote kuweza kupitisha bajeti ya serikali na hii inaashiria kuwa hata wabunge wa upinzani wameanza kukubali kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya CCM.

Leo baada ya kipindi cha maswali na majibu, Waziri wa Afrika ya Mashariki, Sammuel Sitta atawasilisha makadirio ya Wizara yake kwa mwaka 2014/2015. Aidha, baada ya wabunge kupitisha bajeti ya Wizara hiyo, Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi atawasilisha makadirio ya Wizara yake. Naamini kuwa tutakuwa pamoja katika kuwahabarisha Watanzania juu ya kile kinachojiri hapa bungeni Dodoma.

**********UPDATES**************
*Nchi wanachama zimekamilisha mfumo wa forodha ya himaya moja kwa kutumia mfumo wa kielectronic wa kufuatilia bidhaa (Electronic cargo tracking system). Lengo ni kupunguza gharama za kufanya biashara katika nchi za afrika mashariki, kupunguza muda wa kusafirisha mizigo, kupunguza gharama na kuboresha ufanisi wa bandari zetu.
*thamani ya mauzo ya biashara za Tanzania na nchi wanachama wa Afrika ya mashariki. imefikia dola za kimarekani milioni 1120. Bidhaa zilizoongoza kwa mauzo ni pamoja na mashine mbalimbali
* Vikwazo 11 kati ya 33 vimeondolewa ambavyo ni pamoja na msongamano wa bidhaa kwenye bandari ya Dar na kulipaia bidhaa mara mbili.
*vituo vya ukaguzi wa miziko kwenda Rwanda, Burundi na DRC vitapunguzwa kutoka 15 hadi 3 ambavyo ni Vigwaza mkoani Pwani, Manyoni Singida na Nyakanazi
*maandalizi ya katiba ya Shirikisho la Kisiasa yameanza. Hii ni baada ya nchi wanachama kukamilisha mazungumzo ya model ya Shirikisho hilo la kisiasa
* Nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika ya Mashariki zimetakiwa kufungua mipaka yake ili kurahisisha biashara na jumuiya nyingine kama vile za SADC na COMESA
* Zanzibar imechaguliwa kuwa makao makuu ya lugha ya Kiswahili ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki
*Hospitali na Chuo kikuu cha Afya na Tiba cha Muhimbili kimeteuliwa kuwa kituo cha Tiba ya Magonjwa ya Moyo ya EAC
* Majadiliano yanaendelea ili Pass ya kusafiria ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki itumike kimataifa miongoni mwa nchi wanachama. Huenda utaanza kutumika Nobemba 2015
*Maombi ya Sudani ya Kusini kujiunga na EAC yataanza kujadiliwa Septemba 2014 mara baada ya serikali ya nchi hiyo kutoa elimu kwa umma kwa wananchi wake juu ya umuhimu wa kujiunga ha jumuiya hii
 
Manjagata

JF-Expert Member
Mar 7, 2012
6,346
2,000
Hivi bado kuna Wizara ya Kilimo na Mifugo? Ndivyo unavyowafundisha watoto wetu wewe Mulugo?
 
Weston Songoro

JF-Expert Member
Feb 17, 2014
2,794
1,500
Nawaona Wabunge wamepewa muda wa kutosha kuuliza maswali juu ya ugonjwa wa Malaria na Dengue. Hii ni kutokana na uzito wa magonjwa haya
 
Chabruma

JF-Expert Member
Sep 19, 2013
5,661
1,250
Nawaona Wabunge wamepewa muda wa kutosha kuuliza maswali juu ya ugonjwa wa Malaria na Dengue. Hii ni kutokana na uzito wa magonjwa haya
Hakika Mkuu. Ugonjwa wa Malaria na Dengue yanasababishwa na vimelea vinavyosambazwa na mbu. Hivyo Mwenyekiti wa Bunge, Zungu ametoa muda wa kutosha kwa wqbunge kuuliza maswali ya kutosha ili serikali itoe ufafanuzi utakaosaidia wabunge kusaidia kuhamasisha mapambano dhidi ya magonjwa haya
 
Ama Amaa

Member
Feb 29, 2008
75
95
Kauliza swali la nyongeza bungeni eti atapatiwa kazi wizara ya mawasiliano sayansi na teknolojia kama atakosa ubunge mbinga?
 
SWEET GIRL

JF-Expert Member
Dec 29, 2011
498
250
Mkuu chabruma kwan huyu profesa muhongo waziri wa nishati na madini amejibu nini alipokuwa anajibu swali la mbatia? Maana nimeona mbatia kaomba mwongozo kuwa profesa muhongo amemtukana Reginald mengi alipokuwa akijibu swali lake!hata hivyo mwenyekiti amemwambia atampa nafasi mwishon mwa bunge ili ndo aombe huo mwongozo!
Hata hivyo inaonyesha huyu waziri anachuki binafsi na bwana mengi!nina wasiwasi sana kama hii bajeti yake itapita!kama sio kumng'oa kabisa!mengi ni mzalendo!nakubali ana mapungufu yake lkn aliyoyafanya kwa faida ya taifa hili ni mengi!kama waziri anatakiwa kuwa na busara na si kuonyesha chuki binafsi kwenye chombo kiteule kama bunge!huyu waziri aonywe kuhusu hili jambo as yeye ni waziri hatakiwi kum-attack mwananchi wa kawaida namna hiyo tena bungeni!ameniboa sanaaa
 
Dada SWEET GIRL,Waziri Muhongo alikuwa anajibu swali kwa niaba ya Waziri Mkuu alilouliza mbunge wa viti Maalum Christina Lissu Mungwai. Mheshimiwa Chiristina alitaka kujua mkakati wa Serikali katika kuwasaidia wananchi wanaojihusisha na uchimbaji wa chumvi kwenye ukanda wa Bonde la Ufa. Waziri Muhongo alijibu vema kuwa wachimbaji wadogo wadogo wakiwemo wachimbaji wa chumvi wameunda vikundi vyao vya uchimbaji. Kwamba Serikali imetoa Dola za kimarekani 50,000 kwa awamu ya kwanza na watapewa tena Dola 50,000 awamu ya pili. Alisema kuwa lengo la mkakati huo wa serikali ni kuwawezesha wachimbaji hao katika shughulizao za uchimbaji ikiwa ni pamoja na kununua teknolojia za kisasa. mwisho alimalizia kuwatahadhalisha watanzania na hasa Wachimbaji juu ya jitihada zinazofanywa na baadhi ya watu kubeza juhudi zinazofanywa na serikali kusaidia wachimbaji wa kitanzania.
 
MAKAH

JF-Expert Member
Sep 27, 2010
1,589
0
Mkuu chabruma kwan huyu profesa muhongo waziri wa nishati na madini amejibu nini alipokuwa anajibu swali la mbatia? Maana nimeona mbatia kaomba mwongozo kuwa profesa muhongo amemtukana Reginald mengi alipokuwa akijibu swali lake!hata hivyo mwenyekiti amemwambia atampa nafasi mwishon mwa bunge ili ndo aombe huo mwongozo!
Hata hivyo inaonyesha huyu waziri anachuki binafsi na bwana mengi!nina wasiwasi sana kama hii bajeti yake itapita!kama sio kumng'oa kabisa!mengi ni mzalendo!nakubali ana mapungufu yake lkn aliyoyafanya kwa faida ya taifa hili ni mengi!kama waziri anatakiwa kuwa na busara na si kuonyesha chuki binafsi kwenye chombo kiteule kama bunge!huyu waziri aonywe kuhusu hili jambo as yeye ni waziri hatakiwi kum-attack mwananchi wa kawaida namna hiyo tena bungeni!ameniboa sanaaa

red = sidhani kama Muhongo alitamka jina la Mengi. Ametumia parables na huenda Mbatia ame read between the lines. Na sijui Mbatia amehamaki kuhusu "Mengi" kwa vile ni Mengi kama mtu au kama mchaga mwenzie.
 
Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,869

Mkuu, Mengi amewateka wachagga wote na ndio anaowatumia bungeni kumshambulia Mhongo. Huyu Mengi ni mnafiki na mzandiki. Katika maisha yake, hajawahi kufanya lolote katika mikoa ya Lindi na Mtwara. Ila kwa sasa kwa vile mikoa hiyo itaizidi mikoa ya Kaskazini kimaendeleo kutokana na nishati ya gesi na mafuta, mengi anafanya jitihada kukwamisha jitihada za serikali. Simpendi Mengi na sitakuja kumpenda kwa unafiki na fitina anazofanya. Hajawahi kuendesha harambee yoyote kuchangia maendeleo ya kusini iwe kanisani au kwenye public. Yeye harambee zake ni kaskazini tu. oia hajawahi kuajiri hata mtu mmoja wa kusini kwenye makampuni yake. Huyu Mengi anaijukia Kusini na chuki zake zimeongezeka baada ya kugunduliwa kwa gesi.
 
Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,869
2,000
Nimeipenda hii. Kauli mbiu ya Jumuia ya Afrika ya Mashariki ni One people, one destiny
 
buchenza

Senior Member
Aug 24, 2012
183
225
Nadhani wote wazima, jamani naomba ufafanuzi kidogo maana mimi sielewi hivi bungeni kwenye TV wanaonyesha kuwa BUNGE LA 16, KIKAO CHA 15 MKUTANO WA 14 Wanamaanisha nini?
 
ntahagaye

Member
Feb 28, 2013
92
0
akiomba muongozo wakati wa kipindi cha maswali na majibu asubuhi Hii, mbatia amemuomba muongozo Mwenyekiti wa bunge akimtaka atoe muongozo wake Kwa kile alichodai waziri muhongo asiingize tofauti zake na Reginald mengi Katika masuala nyeti ya taifa, Mwenyekiti amedai hayo Mambo ni makubwa atatolea Ufafanuzi baadae. stay tune
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom