Yanayojiri Arumeru: Kamata kamata PCCB yaendelea, Mwigulu meneja wa Chadema na Helikopta

Hii ya hapa Arumeru itakuwa fundisho kwa hawa mafisadi!

Hapo Arumeru Mashariki siyo Igunga!

Wamezoea sana!

Kila la heri mkuu...naamini haki itaweza kuushinda uovu.

By the way..Pole kwa dhahama iliyokukumba na washikaji wenzio wa Anfield!!

Babu DC!!
 
Kama Takukuru wangekuwa huru kufanya kazi zao na wangeweza kutumia meno ya chuma kung'ata, ni dhahiri kwamba Sioy asingekuwa mgombea wa ccm na hata kama amepitishwa bado kampeni hadi uchaguzi huu usingefunikwa na kiwingu cha rushwa.
Lakini kwakuwa ''taakuukuu'' wameamua kujivisha meno ya plastiki basi wacha noti zitembezwe arumeru mashariki na hatiamye nec watamtangaza mbunge baada ya uchaguzi kukamilika.
 
Kwa rafu walizochezeana CCM ARUMERU, ushahidi wa hili ukiwa ni kamatakamata ya TAKUKURU,CDM kupitia wananchi wa ARUMERU, wamepewa fursa ya kihistoria kuwakumbusha tena Watanzania kuwa mabadiliko yanawezekana na yanakuja.
Wana wa Arumeru sasa wafanye kile kilichofanywa na jirani zao wa Arusha mjini, Hai, na Moshi mjini.
 
Hivi wameru na wamasai watakubali kuongozwa na wachagga? amma kweli dunia imekwisha!
 
Nitashangaa CDM wakishindwa uchaguzi huu kwa namna yeyote! Kwanza Mgombea ubunge wa CCM hajazoea mikiki ya siasa kama wa CDM na hata uwezo wa kujenga hoja zilizokomaa Nassari ni mzoefu.Pili Mkapa anaekwenda kumpigia debe Sioyi ana kashfa lukuki kama Chadema wakianza mapema kuanika yote tena bila Aibu Mkapa atanywea,Tatu tycoon wa uchaguzi wa Arumeru ni EL ambaye na yeye hasafishiki na uozo wake ukianikwa vizuri kwisha kabisa.Siyoi hawezi kushinda bila akina EL hivyo ukitaka mifugo watawanyike piga mchungaji wao! Tatizo la CDM siku hizi toka wadanganywe kuwa eti hawana lingine zaidi ya ufisadi nao kelele zimepungua hadi Mkapa na El wanapata ujasiri wa kupambana nao majukwaani! Akina Dr Slaa,Lisu,Mbowe,Mnyika,Zitto,Mdee na wengine waumbueni hasa hao mafisadi hadi wakimbie huku mkiwaeleza wana Arumeru mtawafanyia nini!! Narudia tena Chadema mkishindwa Arumeru hata kama mtaibiwa kura mchana kweupe ndio Kifo rasmi cha upinzani kukamata dola! Ni wajibu wenu kudhibiti kila hila kwa mbinu zote! Nawatakia kheri!
Tunaomba tena mkapa ni wa kuanika kabisa kutokana na siri ya kugawa viwanda vilivyokuwa vinawanufaisha watanzania. Yaani huyu jamaa katurudisha nyuma sana. Huyu EL alishtuka akanunua vile viwanda kwa kutumia watu leo hii anamwaga hela kama mvua. Hizo pesa alizipata wapi wakati viongozi walitumikia serikali tunawaona.
 
Tunaomba tena mkapa ni wa kuanika kabisa kutokana na siri ya kugawa viwanda vilivyokuwa vinawanufaisha watanzania. Yaani huyu jamaa katurudisha nyuma sana. Huyu EL alishtuka akanunua vile viwanda kwa kutumia watu leo hii anamwaga hela kama mvua. Hizo pesa alizipata wapi wakati viongozi walitumikia serikali tunawaona.

CHADEMA wangesikiliza ushauri wangu na kumshawishi slaa asimame kugombea jimbo hili hii mechi ingeisha mapema sana kwa CHADEMA kuibika washindi,ukaidi wao ndio utawacost na kulipoteza jimbo hili mbele ya ccm vipande vipande huko Arumeru kutokana na majeraha ya kura za maoni.

Inasikitisha sana kushindwa na chama kilichogawanyika na kuwa weak kama ccm huko arumeru,slaa angeshinda kwa kishindo pale.
 
Back
Top Bottom