Yanayojiri Arumeru: Kamata kamata PCCB yaendelea, Mwigulu meneja wa Chadema na Helikopta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yanayojiri Arumeru: Kamata kamata PCCB yaendelea, Mwigulu meneja wa Chadema na Helikopta

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Mwana Mpotevu, Mar 4, 2012.

 1. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #1
  Mar 4, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Haya ni kwa mujibu wa Gazeti la mwananchi leo Jumapili. Kwa uchache:

  (a) PCCB bado yawaandama watoa rushwa kambi ya Sioi
  (b) Chadema huenda wakatumia helikopta katika kampeni
  (c) Kundi la Sarakikya na Elirehema Kaaya wapinga kupitishwa Sioi
  (d) Mwigulu apenya na kuwa meneja wa kampeni Arumeru
  (e) Mkapa kuzindua kampeni za CCM
  (f) Yaliyobakia jisomee mwenyewe hapa chini............


  CCM, Chadema sasa vita rasmi

  Sunday, 04 March 2012

  SLAA, MKAPA KUONGOZA MAPAMBANO ARUMERU, NASSARI, SUMARI WAPITISHWA

  Na Waandishi wetu, Dar na Arusha

  VYAMA vya CCM na Chadema vimetangaza rasmi vita ya kuwania Ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki, mkoani Arusha huku vikianika majina ya makada watakaoongoza mapambano kwa ajili ya kujihakikishia ushindi.

  CCM ambayo imempitisha Siyoi Sumari kuwania nafasi hiyo, imesema kampeni zake zitazinduliwa na Mwenyekiti mstaafu wa chama hicho ambaye pia alikuwa Rais wa awamu tatu, Benjamin Mkapa na Chadema itawatumia viongozi wake wa kitaifa, wakiongozwa na Mwenyekiti wake Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk Willibrod Slaa.

  Wakati huohuo, Kamati Kuu (CC) ya Chadema jana ilimpitisha, Joshua Nasari kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mdogo wa jimbo hilo.

  Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Mbowe aliwaeleza viongozi wakuu wa chama hicho, wapenzi na wafuasi wa Chadema waliojazana eneo la Hoteli The Ice Age Usa-River, wilayani Arumeru jana kuwa wamejiandaa kikamilifu kunyakua jimbo hilo na kamwe hawatakubali hujuma zozote kutoka kwa mtu au chama chochote.

  Mbowe aliyezungumza kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu wake, Dk Slaa kumtanga rasmi Nasari, alitamba kuwa mchakato wa kumtafuta mgombea kupitia chama hicho haujaacha nyufa wala mifarakano miongoni mwa wagombea na wafuasi wao kama ilivyotokea kwa vyama vingine vya siasa ambavyo hakuvitaja.

  Alisema mara nyingi mipasuko ndani ya vyama vya siasa hutokana na mchakato wa kupata wagombea kutokana na hila za baadhi ya viongozi, wanachama au wapambe wa wagombea, hali aliyosema haijajitokeza ndani ya Chadema kutokana na mfumo mzuri unaozingatia demokrasia kwa wote bila kujali umaarufu au ukwasi wa mtu.

  "Wagombea wote waliojitokeza kuchukua fomu kuomba uteuzi tumewaalika katika Kamati Kuu na wote wameridhika na ushindi na uteuzi wa mgombea mwenzao na wote watashiriki kikamilifu kwenye kampeni kuhakikisha ushindi wa chama unapatikana," alisema Mbowe.

  Akitangaza uamuzi wa Kamati Kuu, Dk Slaa, alisema kikao hicho kilichoshirikisha wabunge, mameya na wenyeviti wa halmashauri za wilaya zinazoongozwa na Chadema, kwa kauli moja kilipitisha jina la Nasari kuitikia sauti ya wananchi na wakazi wa Arumeru waliomchagua kwa kura 805 kati ya 888 zilizopigwa kwenye kura za maoni.

  "Wananchi Arumeru tumesikia kauli yenu kupitia kura zenu za maoni, Nasari ni kijana wenu siyo wa Dk Slaa, Mbowe wala Chadema.

  Katika kura za maoni, Nasari alimwacha mbali mgombea wenzake Anna Mghiwa aliyemfuatia kwa kupata kura 23 huku wagombea wengine wanne, wakipata kura chini ya 20.

  Chama hicho pia kinaendelea kufanya tathimini ya kutumia helikopta katika kampeni zake katika jimbo hilo.

  Nasari ashukuru

  Akitoa shukrani mbele ya wajumbe wa Kamati Kuu ya chama chake, Nasari aliwaomba wafuasi, wapenzi na wanachama wote wa Chadema kushikamana na kuwa tayari kwa mapambano ya haki, kuhakikisha wanaibuka na ushindi mnono kwenye uchaguzi huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

  "Wao (CCM), najua watatumia dola na fedha, lakini sisi tusihofu kwani tuna Mungu anayetupigania kwa sababu mapambano yetu ni kudai haki dhidi ya uovu.
  Kwa pamoja tukishirikiana kuondoa hofu kwani tutashinda," alisema Nasari.

  CCM
  Kwa upande CCM Kamati Kuu (CC) ya chama hicho jana ilimteua Mwenyekiti mstaafu ambaye pia ni Rais mstaafu wa awamu ya Tatu , Mkapa, kuongoza kampeni za kumnadi Mgombea Ubunge wa chama hicho, Siyoi Sumari katika jimbo la Arumeru Mashariki.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya CCM, Nape Nnauye, alisema kikao cha kamati hiyo kilichoketi jana, kilipitisha jina la Siyoi kuwania nafasi hiyo iliyoachwa na baba yake, Jeremia Sumari aliyefariki usiku wa Januari 18 mwaka huu.

  Nape alieleza kwamba, kamati hiyo pia imemteua Katibu wa Idara ya Uchumi na Fedha ya chama hicho, Mwingilu Nchemba kuratibu kampeni hizo.

  Katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Igunga ambao CCM ilishinda, Mkapa ndiye aliyefungua kampeni hizo huku, Nchemba akiratibu kuanzia mwanzo hadi mwisho.

  Akizungumzia tuhuma za rushwa ambazo zimekuwa zikiripotiwa katika mchakato wa uteuzi, aliitaka Takukuru kuhakikisha wanakamata mtandao mzima uliohusika na utoaji rushwa.

  Kauli ya Siyoi

  Sumari, aliambia Mwananchi Jumapili kuwa kwamba pamoja na kufurahishwa na uamuzi wa Kamati Kuu ya CCM kupitisha jina lake kupeperusha bendera ya CCM wilayani Arumeru Mashariki, chama hicho kinapaswa kutoa ushirikiano wa dhati kuhakikisha kinatetea jimbo hilo.

  Hata hivyo, alisisitiza kwamba changamoto zote alizozipitia katika mchakato wa uteuzi , zikiwemo tuhuma mbalimbali za rushwa ni misukosuko ya kisiasa ambayo haiwezi kuepukwa zaidi ya kukabiliana nayo.

  "Nashukuru chama kwa kupitisha jina langu, lakini changaomoto zote nilizokuwa nikipitia naamini ni misukosuko tu ya kisiasa, lakini tusahau yaliyopita sasa tusonge mbele kunyakua ushindi," alisema Sumari

  UVCCM

  Katika hatua nyingine Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM ) wilayani Arumeru, imefurahishwa na uamuzi uliofanywa na CC ya CCM kumpitisha Siyoi kupeperusha bendera ya chama hicho na kueleza kwamba kilio cha wanachama wa CCM wilayani humo, sasa kimesikilizwa.

  Hata hivyo, wakati jumuiya hiyo ikiupokea ushindi huo kwa furaha, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru) imeendelea na kamata kamata yake ambapo safari hii ilimshikilia na kumhoji kwa muda Katibu Hamasa wa umoja huo wilayani Arumeru Mashariki, John Nyiti kisha kumwachia huru.

  Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Esther Maleko alisema mbali na kilio cha wakazi wa jimbo hilo kusikika juu ya mgombea wao, umoja wao umejipanga kikamilifu kuingia ulingoni kuhakikisha ushindi unapatikana.

  Hekaheka za uchaguzi wa jimbo hilo wakati zikiendelea baadhi ya makada wa CCM na UVCCM wilayani humo wameendelea kukumbwa na misukosuko baada ya viongozi wake akiwemo Nyiti kushikiliwa na Takukuru kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya rushwa wilayani humo.

  Nyiti alipoulizwa juu ya taarifa hizo kwa njia ya simu alikiri kukamatwa na maofisa wa Taasisi hiyo.

  Kamanda wa Takukuru mkoani Arusha, Mbengwa Kasumambuto alipoulizwa na gazeti hili juu ya taarifa hizo hakuweza kukiri wala kukataa juu ya kuhojiwa kwa kada huyo na kudai kwamba wanaohojiwa na Taasisi hiyo wako wengi na wengine wanahojiwa kama mashahidi, hivyo alidai si vyema kuwataja majina kwa kuwa bado wanakamilisha uchunguzi wao.

  Hali ilivyo ndani ya vyama

  Makundi ya vigogo wa CCCM ambao wanajipanga kugombea Urais mwaka 2015, yametajwa kusababisha mpasuko mkubwa ndani ya chama hicho katika uteuzi wa mgombea wa Ubunge Arumeru Mashariki.

  Mpasuko wa makundi hayo, inaelezwa unaweza kuchangia chama hicho kupoteza jimbo hilo.

  Sumari amekuwa akiungwa mkono na kundi la Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa huku wagombea wengine, walikuwa wakiungwa mkono na kundi la na vigogo wa chama hicho wanaojipambanua kuwa ni wapiganaji dhidi ya ufisadi.

  Wakizungumza na Mwananchi Jumapili jana katika mahojiano maalumu baadhi ya viongozi wa CCM na makada wa Chama hicho, wameeleza mpasuko huo ni mkubwa tofauti na wengi wanavyofikiri.

  Asantaeli Erio alifafanua kuwa, kwa sasa baada ya Sumari kupitishwa, kundi la vigogo wa CCM na Serikali huenda wakasusa kumpigia kampeni hasa kutokana na kubainika wazi kutomuunga mkono na siri za hoja zao kuvuja.

  Wafuasi wa Sarakikya

  Kundi la wafuasi wa aliyekuwa mgombea wa ubunge wa CCM, William Sarakikya na Elishilia Kaaya jana, walieleza kutokubaliana na maamuzi ya Kamati Kuu kupitisha jina la Sumari kuwania jimbo hilo.

  Mmoja wa wafuasi hao, Emanuel Kanangira alisema wanapinga uteuzi wa Sumari na leo wanatarajia kurejesha kadi za CCM.

  Upande wa Chadema
  Ingawa Joshua Nasari ndiye amepitishwa kuwania nafasi hiyo ya ubunge, huenda ushindi wa Chadema katika jimbo hilo, ukawa mgumu kutokana na viongozi wa koo za kabila la Kimeru maarufu kama 'Washili' ambapo wengi wanatoka familia ya Sumari kutangaza mgogoro na chama hicho.

  Viongozi hao kupitia Mwenyekiti wao,Chief Sumari kutangaza kumzuia Mbunge wa Jimbo la Arusha mjini, Godbless Lema ambaye alitarajiwa kuwa meneja kampeni wa Chadema katika jimbo hilo, kutua Arumeru wakimtuhumu amewakashifu.

  Hata hivyo, mmoja wa wazee wa kabila hilo, Yohane Kimuto alitangaza juzi kupinga kauli hiyo na kusisitiza Lema atafika Arumeru na kufanya kampeni.

  Imeandaliwa na Freddy Azzah, Peter Saramba, Moses Mashalla, Mussa Juma, Arusha
   
 2. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #2
  Mar 4, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Chadema 2po vzuri,ivi nchemba anaifananisha igunga na meru.nchemba bana,utaishia kunawa wewe na mtoga sikio.
   
 3. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #3
  Mar 4, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mkapa + Mwigulu, ushindi lazima.

  CDM sioni sababu ya viongozi wote kuanzia mwenyekiti, katibu mpaka viongozi wa kada za chini kwenda kujikusanya Arumeru. Haya ni matumizi mabaya ya fedha za chama.
  Wachagueni wawakilishi wachache mnaoamini wanaweza kuwaletea ushindi.
   
 4. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #4
  Mar 4, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Hii ya hapa Arumeru itakuwa fundisho kwa hawa mafisadi!

  Hapo Arumeru Mashariki siyo Igunga!

  Wamezoea sana!
   
 5. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #5
  Mar 4, 2012
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Ngoja tusubiri mtifuano!! Maana mengi yanasemwa, hadi tunashindwa kupata picha halisi, huenda ni propaganda zimeshaanza kufanya kazi kwa hali ya juu!!
   
 6. Imany John

  Imany John Verified User

  #6
  Mar 4, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 2,777
  Likes Received: 262
  Trophy Points: 180
  Kama wewe huoni sababu,Basi wameru wanaijua sababu.
   
 7. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #7
  Mar 4, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Ngoja nichukue tiketi ya kwenda Arumeru,kuna mvua ya pesa kule!
   
 8. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #8
  Mar 4, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  I wish TAKUKURU wangetafuta kitu cha maana na cha manufaa kwa watanzania badala ya kuishia kusakama CHADEMA
   
 9. K-killer

  K-killer Senior Member

  #9
  Mar 4, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 143
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Unataka mwenyekiti na katibu wasiende ili muibe vizuri kura,nA matumizi mabaya ya fedha za chama kamA usemavyo we inakuhusu nini,umechAngia hata shilingi 10?acha porojo
   
 10. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #10
  Mar 4, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Mwigulu Arumeru siyo Igunga braza! Ukileta za Igunga wanakukata uume!
   
 11. M

  Mabewa Senior Member

  #11
  Mar 4, 2012
  Joined: Oct 30, 2011
  Messages: 128
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni ccm simuungi mkono Sioi aina yoyote ya matokeo kwangu sawa naamini atakaechaguliwa atawawakilisha wameru...kwisha.
   
 12. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #12
  Mar 4, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Igunga wote walikuwepo bado CD ikashindwa.
  Uzini tena viongozi wote wakaenda nako CDM ikaangukia pua..
  Naona na Arumeru yatawakuta ya Igunga na Uzini.

  Hapa hatuangalii nani amechangia nini, tunaangalia good governance!
   
 13. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #13
  Mar 4, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Tusubiri tuone..tar 1 siyo mbali!
   
 14. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #14
  Mar 4, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu nami naenda huko nikashuhudie kwa macho yangu.
   
 15. Said Bagaile

  Said Bagaile JF-Expert Member

  #15
  Mar 4, 2012
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 686
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kama Igunga, Mkapa na Nchemba walikuwa viongozi wa kampeni za CCM plus Chakula cha Msaada, plus Uchanga wa CDM jimboni kule, bado almanusra CDM walichukue jimbo, Itakuwaje kwa Arumeru ambapo CDM ni nyumbani na inajulikana kama Sala! Magamba are in really trouble!
   
 16. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #16
  Mar 4, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  hii inaonyesha cdm yote inawathamini watu wa meru!!
  Mkuu matumizi mabaya ya fedha ni kuwalisha watu pilau pale kirumba.
   
 17. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #17
  Mar 4, 2012
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Pilipili usiyoila yakuwashiani? Mmmesahau mlivyoiba pesa ya Kagoda BOT ili mshinde na mpaka leo mwashindwa kumpeleka Rostam Mahakamani, Nyie CCM ni mijizi iliyokubuhu na hamna huruma kwa watanzani na yafaa mg'olewe kama daktari anavyotoa saratani kwa mgonjwa wake
   
 18. m

  mpigilie JF-Expert Member

  #18
  Mar 4, 2012
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 306
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Naona safari hii hijabu wamevalishwa washiri
   
 19. S

  Swagatwende Member

  #19
  Mar 4, 2012
  Joined: Mar 1, 2012
  Messages: 36
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Tunavishauri vyama vyote hasa CDM na CCM kuonyesha siasa za ukomavu kwa faida ya wana Meru na Nchi kwa jumla, .
   
 20. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #20
  Mar 4, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,512
  Likes Received: 5,630
  Trophy Points: 280
  Nitashangaa CDM wakishindwa uchaguzi huu kwa namna yeyote! Kwanza Mgombea ubunge wa CCM hajazoea mikiki ya siasa kama wa CDM na hata uwezo wa kujenga hoja zilizokomaa Nassari ni mzoefu.Pili Mkapa anaekwenda kumpigia debe Sioyi ana kashfa lukuki kama Chadema wakianza mapema kuanika yote tena bila Aibu Mkapa atanywea,Tatu tycoon wa uchaguzi wa Arumeru ni EL ambaye na yeye hasafishiki na uozo wake ukianikwa vizuri kwisha kabisa.Siyoi hawezi kushinda bila akina EL hivyo ukitaka mifugo watawanyike piga mchungaji wao! Tatizo la CDM siku hizi toka wadanganywe kuwa eti hawana lingine zaidi ya ufisadi nao kelele zimepungua hadi Mkapa na El wanapata ujasiri wa kupambana nao majukwaani! Akina Dr Slaa,Lisu,Mbowe,Mnyika,Zitto,Mdee na wengine waumbueni hasa hao mafisadi hadi wakimbie huku mkiwaeleza wana Arumeru mtawafanyia nini!! Narudia tena Chadema mkishindwa Arumeru hata kama mtaibiwa kura mchana kweupe ndio Kifo rasmi cha upinzani kukamata dola! Ni wajibu wenu kudhibiti kila hila kwa mbinu zote! Nawatakia kheri!
   
Loading...