cmp
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 6,086
- 6,723
Habari wana jukwaa,
Niende kwenye mada moja kwa moja,
Kuna kampuni inaitwa CSI hapa Kinyerezi two power plant inaajiri wafanyakazi haiwapi mkataba wowote wa ajira na huwa inawalipa wafanyakazi in weekly basis. Mfanyakazi hulipwa 150,000 hadi 170,000 kwa wiki na hupewa cash mkononi hivyo serikali inapoteza kodi kubwa kupitia kampuni hii.
Kampuni hadi inapewa tenda ya mradi mkubwa kama huu ina maana imejitosheleza na imekubaliana na sheria na taratibu za kazi ikiwemo kumpa bima ya afya mfanyakazi na stahiki zingine kama kumchangia mafao ya mifuko ya hifadhi ya jamii. Hawa wahindi ni wajanja wajanja hivyo serikali iwamulike ili wawalipe wafanyakazi mishahara kupitia benki, iwape mikataba ya ajira pamoja na kuchangia wafanyakazi mifuko ya jamii.
NB: Sina chuki wala hiyana na kampuni hii maana mimi nimeajiriwa hapa kwenye mradi huu nalipwa mshahara mkubwa tu na stahiki zote na sijaajiriwa na kampuni hii ya CSI bali najionea yanayoendelea na si vibaya kuwasemea wengine maana wanalalamika chini chini hawajui pa kuanzia kudai haki yao.
Kazi njema.