Yanayofanyika Chato yanafanyika kote Nchini Tanzania

Yanayofanyika Chato; Yanafanyika Kote Nchini Tanzania

Na: Mzalendo wa kweli (ellyskywilly)

Serikali ya awamu ya tano imekuwa ikifanya kila liwezekanalo katika kuhakikisha Tanzania nzima inakuwa na maendeleo ya vitu na watu, hivi sasa kila ukipita kwenye maeneo mengi nchini utakutana na ama miradi imekamilika au inaendelea na ujenzi au ipo katika hatua za mwisho za kumalizika kwa miradi mbalimbali.

Ukianzia Jijini Dar es Salaam tunashuhudia miradi ya ujenzi wa miundombinu ya barabara, madaraja, hospitali na huduma nyingi sana za Kijamii, ukija Mkoa wa Pwani halikadhalika utakutana na ujenzi wa miundombinu mingi.

Ujenzi huo pia unafanyika kwenye maeneo mengi nchini.

Kinachofanyika Wilayani Chato ndicho kinachofanyika kwenye maeneo mengi nchini Tanzania, ninasema hivi kwa sababu wasioitakia mema nchi yetu mara nyingi wanahoji eti kwa nini maendeleo yanafanyika Chato! Wananchi wa Chato ni Watanzania kama ilivyokuwa kwenye maeneo mengine nchini ambayo maendeleo ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo unafanyika.

Swali la kujiuliza ni kwamba, hivi Chato ipo nchi gani? hivi Wananchi wa Wilaya hiyo hawahitaji hospitali? hawahitaji barabara? Hawahitaji huduma za kijamii kama ilivyo Dar es Salaam na Mikoa mingine? Wanaoeneza habari hizi za uzandiki bila shaka ni walewachumia tumbo ambao wanadhani huu ni muda wa propaganda

Wanahoji ujio wa hivi karibuni wa baadhi ya Viongozi wakuu wa nchi waliotembelea Chato eti kama dhifa za kitaifa na magwaride ya heshima kwa ajili ya Wakuu hao yamefanyika Chato, walitaka vifanyike wapi? Dar es Salaam? Dodoma? Au Kilimanjaro? Wamekosa hoja.

Kufanyika kwa mapokezi hayo Chato ni sawa sawa kabisa kwa sababu tukumbuke Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli anatokea Chato, kama ilivyo kawaida mahali anapotoka Rais ni lazima kuwe na Ikulu ndogo ambayo shughuli zote za Rais zinafanyika, tumeshuhudia Butiama kwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, tumeshuhudia kwa Rais wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi, awamu ya tatu, ya nne na ya sasa ya Dkt. Magufuli.

Chato kama ilivyokuwa maeneo mengi nchini inahitaji miundombinu ya usafirishaji kama inavyofanyika sasa ya ujenzi wa uwanja wa ndege wenye uwezo wa kutua na kurusha ndege kubwa sawa na viwanja vya ndege vya Dar Es Salaam, Kilimanjaro, Mwanza na Mbeya.

Chato inahitaji kuwa miongoni mwa Wilaya za kisasa kwa kuwa na miundombinu bora ya barabara na taa za kuongozea magari barabarani, hata ikiwa ni Wilaya pekee yenye miundombinu bora nchini ni Sawa kabisa kwani kwa miaka mingi tumeshuhudia miji ya Dar es Salaam ikiwa na miundombinu bora, mbona Chato hawakupiga kelele?

Wilaya ya Chato ni ya kipekee kwa vivutio vya Utalii ikiwepo hifadhi ya Taifa ya Burigi na hivyo kuwepo kwa ongezeko la Watalii ambao kwa namna moja au nyingine wamekuwa wakiliingizia Taifa fedha za kigeni hivyo kuna kila sababu ya kuiendeleza Wilaya hii.

Chato kama ilivyo kwa Wilaya na Mikoa mingine Nchini Tanzania ipo katika program za kuanzisha na kuendeleza michezo program ambazo zinaenda sambamba na ujenzi wa uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu pamoja na Michezo mingine mingi.

Kutokana na umuhimu wa Wilaya ya Chato kibiashara sasa Mabenki ya kibiashara na taasisi nyingine zimeona fursa na kuamua kuwekeza kwenye Wilaya hiyo inayokuja juu kibiashara.

Wilaya ya Chato kijiografia ipo katika Mkoa wa Geita Kaskazini-Magharibi mwa Tanzania, Chato ni mojawapo ya Wilaya tano za Mkoa wa Geita na kiuchumi Wilaya hii inafanya shughuli za kilimo cha kibiashara, uvuvi na shughuli nyingine za kiuchumi.

Kwa upande wa Sekta ya utalii, ni kwamba Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo katika Ziwa Victoria ipo nje kidogo ya Wilaya ya Chato. Hifadhi hiyo ilianzishwa mwaka 1965 na, kwa mujibu wa takwimu zilizopo sasa, hifadhi hiyo inatembelewa na wageni wengi sana kwa mujibu wa takwimu za Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA).

Wilaya ya Chato ilianzishwa mwaka 2005 kutoka iliyokuwa Wilaya ya Biharamulo, Mkoa wa Kagera. Mwaka 2012, Wilaya hiyo ilihamishiwa kwenye Mkoa mpya wa Geita.

Wilaya hii imekuwa maarufu zaidi Kutokana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyechaguliwa kama Rais wa Tanzania mwaka 2015, alizaliwa Chato mwaka 1959.

Hivyo basi kwa wanaobeza maendeleo ya Chato hawana hoja kwa sababu Wananchi wa Chato wanahitaji maendeleo pia, sio dhambi Rais kupeleka maendeleo na nyumbani kwao kama anavyofanya nyumbani kwa watanzania wengi kwenye Mikoa yote Nchini.

Hivi kuna dhambi mtu akajenga kwao, namaanisha yaani unafanya kazi alafu usijenge angalau nyumba ya chumba na sebule nyumbani kwako? Yaani utachekwa hadi na sisimizi, Magufuli anapaswa kuendeleza Chato kama anavyoendeleza Kilimanjaro, Arusha, Mbeya na kwingineko.

Sio vibaya nyumbani kwa Rais wa nchi kuwa na maendeleo au mambo mazuri, na wala sio sifa nyumbani kwa Mkuu wa Nchi kuwa pa hovyo hovyo au duni kimaendeleo, hili naomba Watanzania mlielewe.

Vipaumbele vya Watanzania ni maendeleo na ndio dhana ambayo inafanywa Rais Magufuli Nchini kote ikiwepo Wilayani Chato.

Ni ukweli usiopingika kwamba mambo mengi na mazuri yanayofanywa Chato hayatokani na uhusiano wake na Rais Magufuli bali uhusiano wa Wananchi wa Chato na fursa za kiuchumi katika Wilaya hiyo.

Watu wengi wanafurahia kuona Wilaya zilizopo pembezoni mwa Tanzania zikibaki kuwa maskini katika uendelezaji wa miundombinu yake hali ambayo Rais Magufuli ameiondoa kwenye akili za watu, Rais Magufuli anaiambia Dunia kuwa hata katika Wilaya hizo kunahitajika kuwepo kwa miundombinu bora.

Ikumbukwe kuwa Rais Magufuli amefanya mambo mengi makubwa ndani ya muhula wake wa kwanza, kwa maneno mengine, hata kabla ya kufikisha miaka minne kati ya mitano ya muhula wake wa kwanza, Rais Magufuli amefanya mambo makubwa nyumbani Tanzania nzima kuliko walivyofanya Marais wa Tanzania waliomtangulia katika miaka 54 waliyokuwa madarakani.

Rais Magufuli amefanya yote haya katika mazingira ya kikatiba, kisheria na kisiasa ambayo ni magumu zaidi kuliko ya watangulizi wake wote kwani tangu tuwe Jamhuri mwaka 1962.

Tangu kuingia madarakani kwa Rais Magufuli mwaka 2015 amekuwa na rekodi ya kipekee ya kuweza kufanya mambo makubwa nyumbani Nchini pengine Wananchi wanajiuliza amewezaje kufanya mambo haya makubwa!? Jibu rahisi sana, utayari na uchungu wa maisha ya Watanzania wenzake.

Aliyoyafanya Rais Magufuli nchini Tanzania kwa kipindi kifupi tu na ambayo hayajawahi kufanyika tangu Uhuru wa Taifa letu yanamuweka katika kundi la kipekee hata katika Bara zima la Afrika. Bara letu limekuwa na Marais wa aina hii wachache sana na huenda wasiwepo.

Ni Rais Magufuli ndie aliyerudisha nidhamu kwa Viongozi na wafanyakazi wa Serikali, ni Rais Magufuli ndie aliyekabiliana na rushwa na ufisadi, ni Rais Magufuli ndie anaependwa na mataifa mengi Duniani kwa namna anavyoiendesha nchi na kufikia hatua ya kukabiliana na majanga mbalimbali likiwepo janga la Corona linaloikumba Dunia kwa sasa.

Huu ndio upekee wa Magufuli katika Tanzania, katika Bara la Afrika na Duniani, ni upekee wa kujivunia sana.
Sasa kafa hofu fedha ilyotumika Chatto isiishie kama hii International Airport aliyojenga Mobutu kijijini kwao
 
Nawaza jinsi huyu mzee anavyojifungia huko Chattle kuogopa corona, siku akija mjini basi tunafunga turubai na Samia anakuwa Rais, Chattle itasahaulika na kurudi kwenye default setting. Nawaza tuu...
hii ilikuwa January 13, 2021,

Uligonga mule mule
 
Chato imesahaulika

images - 2023-06-13T225856.148.jpeg
 
Back
Top Bottom