Yanayoendelea sasa hivi nchini ni hatari kwa uhai wa chama kilichopo madarakani na baadhi ya viongozi waliopo Serikalini

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Sep 9, 2020
6,860
12,291
Habari zenu ndugu zang watanzania mliopo humu. Ndugu zang nimekuwa nikifuatilia kwa ukaribu sana yanayoendelea nchini, hasa kuhusu tuhuma za ufisadi zinazoelekezwa kwa aliyekuwa Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hayati John P Magufuli.

Najua na inajulikana wazi tu kwamba tokea tulipopata uhuru mpaka leo hakuna awamu ambayo haikufanya madudu iwe madogo madogo au makubwa.

Kila serikali iliyoingia madarakani ilifanya mazuri na mabaya pia kwahiyo hili ni jambo la kawaida kwa tawala zote zilizopita kuanzia mwaka 1961 mpk 2020.

Kinachosikitisha ni kuona kila ufisadi au kila jambo baya lililofanyika, au lililofanywa na kiongozi au mtu yoyote aliekuwa katika serikali ya awamu ya tano lawama zote anabebeshwa hayati Magufuli.

Tunafaham kwamb kuna mamb mengi ya kimaendeleo na mazuri lkn watu kadhaa sijui kwa maslahi au faida ya nani wameamua kumchafua.

Na kwa vile mtu akishafariki hawezi kujitetea kwa shutuma zote zinazoelekezwa kwake iwe za kweli au za uongo, sasa sisi tulio hai tutaendelea kumtetea ili kufuta kbs uchafu unaotengenezwa kwa ajili yake.

Najua hata na yeye alikuwa binadamu kwa hiyo kukosea ni jambo la kawaida lkn asibebeshwe makosa na matatizo mengine ambayo hakuyafanya kwa masilahi ya kundi la watu fulani.

Najua kwa sasa wanaomchafua ambao baadhi yao wapo ndani ya CCM na wanaona fahari sana hayati Magufuli kuchafuliwa ili ionekane kwamba yeye na Serikali yake hawajafanya chochote lkn wakumbuke kuwa huyo wanaemsema ameshakwenda zake, sasa kazi kubwa imebaki kwao walio hai.

Mwaka 2025 unakuja wamejipangaje kupangua hoja za wapinzani wa CCM na serikali kwa ujumla kuhusu ufisadi huo unaoongelewa sasa hivi?
 
Sisi bado ni CCM hatariii gani unaosema hapa tunazungumza walichokifanya waliokuwepo madarakani ya kuiba ma pesa bila Huruma. Hatuna shida na serikali ya Mama Samia
Kumbuka raisi Samia alikuwa makamu wa raisi ktk serikali hiyo inayosemekana kuwa ilifanya ufisadi mkubwa, waziri mkuu pia na bila kuwasahau baadhi ya mawaziri ambao pia wapo ktk serikali hii mpya ya mama Samia.

Kama shutuma hizi zitaendelea na hao niliowataja hapo hawatojiuzulu nyazifa zao serikalini, basi 2025 CCM ijiandae kwa anguko kubwa, japo wengi hawalioni hili.
 
Kwa ufisadi mkubwa ulioibuliwa na CAG uliofanyika awamu ya tano, Makamu wa Rais wa kipindi hicho anakuwaje msafi ilihali ndiye aliyekuwa mtendaji wa karibu zaidi na Rais?

Tukiacha siasa, ni dhahiri kabisa haya yote yametendeka kutokana na uzembe wa mwendazake na wasaidizi wake akiwemo Rais wa sasa.

Msemakweli ni mpenzi wa Mungu.
 
Kwa ufisadi mkubwa ulioibuliwa na CAG uliofanyika awamu ya tano,makamu wa rais wa kipindi hicho anakuwaje msafi ilihali ndiye aliyekuwa mtendaji wa karibu zaidi na rais?Tukiacha siasa,ni dhahiri kabisa haya yote yametendeka kutokana na uzembe wa mwendazake na wasaidizi wake akiwemo rais wa sasa.

Msemakweli ni mpenzi wa Mungu.
ilikuwa ni serikali ya one-man show.Alitaka kujiuzulu mara nyingi sababu ya kutokubaliana na meko.
 
Mama samia asingeweza kufanya lolote vinginevyo wangemtundulisuu mapema.

Harafu mtoa mada usikaze ubongo mjinga wewe ,inamaana ulikuwa huoni yanayowakuta watendaji wake wanaoenda kinyume na yeye ....

Mfano cag aliyepita assad.

Huyo magu alijitengenezea bomu mwenyewe wacha limlipukie huko huko aliko.
 
Back
Top Bottom