Yanayoendelea hapa Kawe Ofisi za NIDA, Mh. Rais tupe tu mpaka March tupambanie kitambulisho

BASIASI

JF-Expert Member
Sep 20, 2010
9,735
5,003
Nimewahi kulalamika kuna watu wanatakiwa wajiondoe wenyewe maofisini kama wameshindwakwenda na kasi ya Mh. Rais.

Hapa Kawe ofisi za NIDA kumekuwa na udhalimu, rushwa kila aina; watu wanawahi, wengine wanakuja wanapelekwa mbele na walinzi wanaondoka munabaki.

Hilo siyo shida; utaratibu wa ku-share kazi kwa pamoja kati ya Uhamiaji na NIDA ni shida sana Mh. Rais.

Hivi natoka pale NIDA kuna fujo imeanza tokea watu wapo ndani NIDA wanachapa kazi.

Uhamiaji wanaondoka wanasema hawalipwi overtime.

Jamani, kweli kwa haya mambo mutafika kweli?

Boss anayehusika na Uhamiaji kakimbia kwa mlango wa nyuma akaanza kuzomewa.

Baada ya fujo, kaja mtu sijui ni mheshimiwa nani akapiga kwa boss wa Uhamiaji, naye akampigia boss wa pale akarudi. Ajabu amerudi kapokelewa na makelele "Tunamtaka rais wetuu"

Akaingia ndani akarudi kuongea na wananchi ati anaomba radhi huku yule mheshimiwa akiagiza kreti tano za soda wapewe wananchi waliojazana kila kona kisa namba.

Jamani hizi namba shida ni nini hasa? Mh. Rais tunaomba watu wako wapite kwenye hivi vituo muone yanayoendelea.

Hapa nawambiaa niliwahi kuomba namba za NIDA via simu nikaletewa namba za mtu mwingine, mwaka siyo wangu wala tarehe.

Bado narudi nipambane upya, Uhamiaji wanaleta mzaha.

Mh. Mkuu wa Uhamiaji, wale watu waliokimbia na kuacha wananchi nakushauri kesho wasionekane kabisa, wananchi hawawataki. Tuletee wenye kufanya kazi na speed ya Dkt. Magufuli please, else mtaitiwa majanga.

Wananchi wameacha watoto wao badala ya kunyonya bado wanawatesa tena, haipendezi kabisa!

Uhamiaji musipofanya kazi na NIDA kwa pamoja mtafanya hilizoezi kuwa gumu sana.

Hivi kama NIDA wao wanakaa mpaka jioni, Uhamiaji wao ni nani wasikae kushirikiana ili watu wapate ID namba zao jamani?

Tunaomba wekeni utu kwanza!
 
Hakujawahi usajili Wa line kuwa na deadline hao wateja wapya je watawapeleka wapi
 
Najua mko hapaaa mnajua kilichoendelea hapo nida kawe

Tunaomba ongezeni wafanyakazi na waliopo waache dharaauu wananchi wakichoka wataamwomba mh raisi hata kwa maandamano awasaidie wapate namba za nida

Watu wachache awawezi kukwamisha zoezi bora kabisa linalotangazwa.kila siku na mh raisi watu wapate namba za vitambulisho

Na kesho nikona kazi kawe ntawamonita mwanzo mwisho kwa kweli na kutoa taarifa husika hapa wananchi wapate haki zao
 
Kwakweli Uhamiaji hapo NIDA Kawe ni tatizo,binafsi nilipiga picha na kumaliza process zote isipokuwa Uhamiaji tarehe 22 Dec, tulikuwa wachache lakini waligoma kutuhudumia wakaondoka (Uhamiaji)
Leo hii nilikuwa hapo Kawe tokea saa 1 kamili asubuhi lakini watu ni wengi sana imebidi niondoke nikitegemea kurudi keshokutwa Alfajiri na ikishindikana basi.
Naunga mkono ombi la kuongezwa kwa muda, waongeze walau mpaka June mwaka huu.
WANATENGENEZA MIANYA YA RUSHWA ALAFU WAMESAHAU HIZI N ZAMA ZA JPM
SHAURI ZAOOO
 
Hilizoezi niliwahi sema n gumu sana

Jana niliweka yaliotokea hapo kawe nida
Leo baada ya kukamilisha kila kitu kwa upendo wa dhati na utiifu uliotukuka nimepokea mm na wenzangu promise ya namba baada ya wiki mbili

Nawashukuru wote waliofanikisha hata hii ahadi ikatoka all d best
 
Back
Top Bottom