Yanayoendelea CCM kuhusu wizi wa 200b za escrow

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,977
20,243
Juzi tarehe 26/05/2014 cabinet imekutana kwa "siri" kujadili escrow na leo huenda party caucus ya ccm ikakutana kuhusu escrow. Wabunge wa ccm wamegawanyika. Wengine wanaunga mkono hoja ya kuundwa kamati teule ya bunge kuchunguza na wengine wanashauri kudhibiti suala hili kupitia CAG na PCCB.
 
Mambo nyeti ya nchi yanaamuliwa kwanza kichama!!!!!!!!!! maana yake maslahi ya kichama yanaangaliwa kwanza!!!!!! Chama kwanza nchi baadae.............mbona iko wazi sana......kwanini kama CCM wanadhamira safi wasiruhusu mjadala wazi ili sisi wananchi tujue wanachukia ufisadi na wabunge wao wapo huru kujadili kwa maslahi ya taifa?

Tunahitaji katiba bora itayosimamia hivi vyama ambavyo bado vinaota falsafa ya chama kushika hatamu.........
 
Hii kashfa haitakufa hivihivi lazima laana itawamaliza wahusika
 
Siyo kweli muongo hizi hoja ulizoweka hazibebi uhalisia wa mambo unayotaka kuyasema ni mawako yenye harufu ya ukawa ndani yake bila ushahidi tupishe ndugu.
 
Juzi tarehe 26/05/2014 cabinet imekutana kwa "siri" kujadili escrow na leo huenda party caucus ya ccm ikakutana kuhusu escrow. Wabunge wa ccm wamegawanyika. Wengine wanaunga mkono hoja ya kuundwa kamati teule ya bunge kuchunguza na wengine wanashauri kudhibiti suala hili kupitia CAG na PCCB.
Kama imekutana kwa siri wewe umejuaje kama ni kwa siri kwavile umeweza kujua kuwa ni kwa siri tuambie pia wajumbe walioketi kwenye hicho kikao ni nani na nani.
 
Mkutano wa wezi na wahujumu hata ufanywe kwenye pango kamwe hauwezi kubaki kuwa siri! Dhambi wanayotenda kwa umma wa Watanzania itawatafuna wao na vizazi vyao.

Ole wao wanaowashabikia kwa kurushiwa ama kujishibisha kwa masazo na makombo wanayobakishiwa ama kurushiwa na hao wezi kwani siku si nyingi watakumbwa na aibu ama fedheha ya ajabu!
 
Kama imekutana kwa siri wewe umejuaje kama ni kwa siri kwavile umeweza kujua kuwa ni kwa siri tuambie pia wajumbe walioketi kwenye hicho kikao ni nani na nani.

unajua kama kuna kitu kinaitwa MTONYAJI au CHANZO CHA KUAMINIKA?
 
Kama imekutana kwa siri wewe umejuaje kama ni kwa siri kwavile umeweza kujua kuwa ni kwa siri tuambie pia wajumbe walioketi kwenye hicho kikao ni nani na nani.

Wajua SIRI ni ya mtu mmoja tu?Ikifika kwa wa pili basi balaa limekukuta.Pole dada'ngu
 
Kama imekutana kwa siri wewe umejuaje kama ni kwa siri kwavile umeweza kujua kuwa ni kwa siri tuambie pia wajumbe walioketi kwenye hicho kikao ni nani na nani.

Hivi hujui nani ni wajumbe wa cabinet? Unajuaje kama mmoja wa wajumbe ndiye aliyempa hizi taarifa?
Je, hujui kuwa si wajumbe wote wa cabinet wanapenda ufisadi?
Tafakari.
 
Siyo kweli muongo hizi hoja ulizoweka hazibebi uhalisia wa mambo unayotaka kuyasema ni mawako yenye harufu ya ukawa ndani yake bila ushahidi tupishe ndugu.

mkuu nakufananisha na yule waziri wa Iraq aliekua anatoa habaro kuusu vita vinavyoendelea kazi yake ilikua kukanusha kila habari
 
Kama imekutana kwa siri wewe umejuaje kama ni kwa siri kwavile umeweza kujua kuwa ni kwa siri tuambie pia wajumbe walioketi kwenye hicho kikao ni nani na nani.

Wacha kuleta ushenzi kwa hoja ya za kipumbavu,wale waliogawana hizo pesa za escrow waliitisha mkutano wa hadhara wa kugawana??!! Mbona imejulikana??!!

Mara ngapi CCM wanaitishaga vikao vya siri kwa ajili ya kuzima hoja muhimu zinazohusu maslahi ya umma na uchumi wa Taifa??!!

Kazi yenu ya diversion ya hoja muhimu ni ya kulaaniwa,kuta kucha mnashinda mitandaoni kwa ids zile zile kutetea uozo kwa hoja za kipuuzi,ptuuuuuu!!!
 
Mambo nyeti ya nchi yanaamuliwa kwanza kichama!!!!!!!!!! maana yake maslahi ya kichama yanaangaliwa kwanza!!!!!! Chama kwanza nchi baadae.............mbona iko wazi sana......kwanini kama CCM wanadhamira safi wasiruhusu mjadala wazi ili sisi wananchi tujue wanachukia ufisadi na wabunge wao wapo huru kujadili kwa maslahi ya taifa?

Tunahitaji katiba bora itayosimamia hivi vyama ambavyo bado vinaota falsafa ya chama kushika hatamu.........

hilo ndilo tatizo pekee na udhaifu mkubwa aliouacha hayati baba wa taifa.....aliposema bila ccm madhubuti nchi itayumba...badala ya kuweka nguvu kubwa kwenye taasisi kama mahakama etc...nguvu zote za taasisi zikabebwa na chama...na hili ndilo limeua sana mashirika mengi ya nchi hii....maana waamuzi wakubwa wa mambo walikuwa viongozi wa chama katika mashirika hayo tena wasio na ujuzi na elimu yoyote....hali hiyo imeendelea kuwepo hadi leo katika namna nyingine kama hiyo hapo juu kwenye thread.
 
Wacha kuleta ushenzi kwa hoja ya za kipumbavu,wale waliogawana hizo pesa za escrow waliitisha mkutano wa hadhara wa kugawana??!! Mbona imejulikana??!!

Mara ngapi CCM wanaitishaga vikao vya siri kwa ajili ya kuzima hoja muhimu zinazohusu maslahi ya umma na uchumi wa Taifa??!!

Kazi yenu ya diversion ya hoja muhimu ni ya kulaaniwa,kuta kucha mnashinda mitandaoni kwa ids zile zile kutetea uozo kwa hoja za kipuuzi,ptuuuuuu!!!

Thanks mkuu kwakumpa ukweli
 
hilo ndilo tatizo pekee na udhaifu mkubwa aliouacha hayati baba wa taifa.....aliposema bila ccm madhubuti nchi itayumba...badala ya kuweka nguvu kubwa kwenye taasisi kama mahakama etc...nguvu zote za taasisi zikabebwa na chama...na hili ndilo limeua sana mashirika mengi ya nchi hii....maana waamuzi wakubwa wa mambo walikuwa viongozi wa chama katika mashirika hayo tena wasio na ujuzi na elimu yoyote....hali hiyo imeendelea kuwepo hadi leo katika namna nyingine kama hiyo hapo juu kwenye thread.

Upo sahihi kabisa mkuu
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom