Yanayoendelea CCM kuhusu wizi wa 200b za escrow

mkuu nakufananisha na yule waziri wa Iraq aliekua anatoa habaro kuusu vita vinavyoendelea kazi yake ilikua kukanusha kila habari

Kweli kabisa jamaa alikuwa anawapa moyo sana watu wake kuwa majeshi yao ynasonga mbele na wasiwe na wasiwasi. Ndio sawa na hawa jamaa, mambo yanaenda ndivyo sivyo lakini wanadai yapo kwenye mstari.
 
Juzi tarehe 26/05/2014 cabinet imekutana kwa "siri" kujadili escrow na leo huenda party caucus ya ccm ikakutana kuhusu escrow. Wabunge wa ccm wamegawanyika. Wengine wanaunga mkono hoja ya kuundwa kamati teule ya bunge kuchunguza na wengine wanashauri kudhibiti suala hili kupitia CAG na PCCB.

Simiyu Yetu, sisi Wananchi tumechoshwa na Siasa zenu za CCM zenye harufu ya kupuuza hoja za msingi kama hizi zinazogusa maisha yetu. Hoja kama hii ya Yericko Nyerere ni hoja ambayo iko very sensitive, lakini tayari umeanza kui-crash kwamba ni uongo, uongo uko wapi hapo! Tundu Lissu alivyosema hakuna hati ya muungano, na kama ipo ni feki, mkasema muongo...cha ajabu jana ITV Dr.W.Slaa amewaumbua kwa ushahidi wa barua ya UN kwa hiyo hapa nani muongo kati ya CCM na hawa watoa hoja, aidha mbona hatujasikia kwamba fulani kakamatwa kwa kosa la kuituhumu CCM au Serikali yenu bila ushahidi, au mnawaogopa? Mifano ya wazi ni Tundu Lissu, Jussa kuhusu Muungano na David Kafulila 200Billions
 
Last edited by a moderator:
Bahati mbaya Yericko Nyerere, Molemo +Tanzania daima hawaaminiki hapa jamvini.
Kuweni makini wasomaji wa story kutoka kwao
 
Last edited by a moderator:
Kama imekutana kwa siri wewe umejuaje kama ni kwa siri kwavile umeweza kujua kuwa ni kwa siri tuambie pia wajumbe walioketi kwenye hicho kikao ni nani na nani.

Mkuu simuyu yetu unatakiwa kuangalia ni nani kaleta habari. wala usiangaike na hii habari
 
Last edited by a moderator:
Wacha kuleta ushenzi kwa hoja ya za kipumbavu,wale waliogawana hizo pesa za escrow waliitisha mkutano wa hadhara wa kugawana??!! Mbona imejulikana??!!

Mara ngapi CCM wanaitishaga vikao vya siri kwa ajili ya kuzima hoja muhimu zinazohusu maslahi ya umma na uchumi wa Taifa?
hili jibu lililokwenda shule kwa hoja za kijinga!
 
CCM ni ukoo wa panya, hii hela imepigwa na Field Marshal Mwigulu Nchemba kwa amelekezo maalum, huenda washaagiza khanga, Tshirt na masufuria ya kupikia pilau kwa ajili ya mwakani uchaguzi. Watanzania tujiandae kisaikolojia kukosa hizo bilioni...
 
Bahati mbaya Yericko Nyerere, Molemo +Tanzania daima hawaaminiki hapa jamvini.
Kuweni makini wasomaji wa story kutoka kwao

Unaweza kuwa na point lakini kwa uelewa wako unakubali hoja kuwa "void" kwa kusema tu mtoaji haaminiki!!!!????
Ndio mtindo gani wa kukataa taarifa huu!!??????
Kama ni kweli hawaaminiki unatakiwa kuwapa wasomaji njia mbadala ya kuweza kubaini uongo wa hao unaowatuhumu ili wao watumie njia hizo kubaini hayo unayodai!!!!

Ni hayo tu kiongozi!!!!!
 
Back
Top Bottom