Yanayoendelea afrika kaskazini fundisho tosha kwa jwtz | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yanayoendelea afrika kaskazini fundisho tosha kwa jwtz

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by YanguHaki, Feb 22, 2011.

 1. YanguHaki

  YanguHaki Senior Member

  #1
  Feb 22, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nafuatilia kwa ukaribu matukio yanayoendelea huko Afrika ya Kaskazini kuanzia Tunisia,Misri na kwa sasa Libya.Yote hayo ni mapinduzi ya kweli ya wananchi dhidi ya tawala dhalimu za viongozi (marais) waliongia madarakani kwa mabavu ama kwa hila na baadae kujichimbia madarakani kwa mgongo wa demokrasia. Ndani ya nchi zote hizi kumekuwa na chaguzi ambazo zimewapa uhalali hawa viongozi kuendelea kutawala pasipo kikomo kiasi ambacho wananchi wamewastukia na kuamua kuwaambia imetosha! Nendeni!
  Hebu jamani tazameni kwa uzuri gani kwa kiongozi wa nchi mpaka upendwe kwa miaka 30 au 40? Ni kituko kwa kweli! Hata ungefanya mazuri mangapi kwa taifa huwezi kueleweka hata kidogo kwa raia wenye ujuzi wa mambo.
  Jambo la msingi hapa ni jinsi maandamano ya raia wasio na silaha wanaopinga tawala hizi dhalimu yanavyoshughulikiwa na vyombo vya dola. Matumizi ya nguvu isiyo ya lazima na iliyozidi kupindukia imeshuhudiwa huko kote kasoro nchini Misri ambapo wanajeshi wameonesha wao ni jeshi la wananchi na sio la watawala. Dhana hii potofu kwamba jeshi ni mali ya rais kwa ajili ya kulinda maslahi yake ndio msingi wa tawala dhalimu barani Afrika na kokote Duniani.
  Hapa Tanzania wananchi wanaandamana kudai haki zao za kimsingi kabisa lakini utakuta polisi wanawazuia eti kwa sababu za kiusalama n.k. Marais wanaingizwa madarakani kwa kura za wananchi lakini wakaapo madarakani kiburi kinawajaa kuwaona wananchi wao wendawazimu hawajui kinachoendelea.
  Juzi juzi wakati wa uchaguzi mkuu wa 2010,Brigedia Jenerali Shimbo alivionya vyama vya siasa vikubali matokeo ya uchaguzi. Hii si kazi yake! Haya ni matokeo ya kutumika na watawala kwa vyombo vya dola nchini.
  Hili ni somo la bure kwa majeshi yetu ya ulinzi na usalama. Waache kutumiwa vibaya na watawala. Wautumikie umma wote wa Watanzania na sio Rais na chama chake CCM. Watambue wajibu wao wa kila siku na waipuuze ile kauli kuwa "wao wanaitumikia serikali ya siku ile". Ni vema wakasema wananchi wa siku hiyo!
   
Loading...