Yanayo tokea sasa Dodoma Bungeni-Lowasa kuulizwa Maswali kila Alhamisi

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,898
Bi Anna Makinda yuko hwani anasoma kanuni mpya ya kumweka Waziri mkuu kitomoto lakini naona wanajenga hoja ya kumlinda ipasavyo. Wanasema maswali binafsi hayatakiwi ,maswali ya kusikia hayatakiwi maswali ya uzushi hayatakiwi sasa sijui watakuwa wanamuuliza nini . Huu mtego sasa .Karibuni Dodoma Makinda bado analeta mipango yao .Kila Alhamisi Mamvi atakuwa hewani kwa dakuka 30 akilambwa maswali .Naendelea kusikiliza toka hapa Dodoma .
 
Kaboyonga , Zitto walia na muda wa waziri mkuu kuwa saa moja badala ya nusu saa.Mambo bambam
 
Spika aingilia kati asema wabakie na dakika 30 tu .Sasa anaongea Shelukindo sijui atasemaje sijui .
 
Mchezo wa kuigiza huu. Hivi inawezekana kweli maswali constructive yakaulizwa na kujibiwa kikamilifu ndani ya nusu saa! binafsi naona hi ni strategy ya kuwashawishi wafadhili kuwa "demokrasia" ya Tanzania ni kiboko manake hata PM anawekwa kiti moto bungeni.
 
Umemsikia Cheief Whip you sijui waziri nani jina lake nimelisahau anaanza kuogopa juu ya aina ya maswali . Iko kazi na nusu saa wanaona ndogo.

Maghimbi anazoza sasa anawahoji juu ya aina ya maswali na kipimo cha maswali ya maana ni kipi .
 
Kweli wanatutapeli tu!!! Hata mambo ya Buzwagi na BOT yalipoanza walidai ni uzushi, leter yamekuwa kweli. Anyway, may it is one step ahead!!!
 
Wameiga ya Waingereza, sasa waruhusu kila kitu, alimwe maswali yote ya nguvu.

Kwa viongozi wetu walivyo, swali moja atamaliza nusu saa nzima. Watu kama akina Zitto watapewa nafasi moja kwa mwaka, CCM watamwonyesha maswali yao kwanza, ili ajibu vizuri.

Ni usanii tu, tunaiga lakini tunachagua kuiga ya kijinga na kuacha ya maana.
 
hizi rangi kijani naona zimekuwa nyingi hii ni nini? au ni kuzima yale madai ya wenzetu wanaodai rangi ya buluu imeenea na hii ni chama fulani forum?

nnaomba kuelimishwa kulikoni?

jamani ni suala tu nisijibiwe kwa kubonyezwa kizenji
 
Sasa jamani hawa watu kweli hawako serious...dakika 30 kwa wanasiasa wetu ni swali moja...kwanza muuliza swali itamchukua dakika 15 kuuliza then Lowassa na yeye kujibu itamchukua nyingine 15...well wana ccm watasema at least kuna hizo dakika 30.
 
Dakika 30 zinatosha kama ni kwa kila week, i don't think kutakuwa na burning issues daily... bado serikali itakuwa inaulizwa maswali mengine kupitia mfumo mwingine!!!
 
hizi rangi kijani naona zimekuwa nyingi hii ni nini? au ni kuzima yale madai ya wenzetu wanaodai rangi ya buluu imeenea na hii ni chama fulani forum?

nnaomba kuelimishwa kulikoni?

jamani ni suala tu nisijibiwe kwa kubonyezwa kizenji

Mtu wa Pwani,

Hata mimi sijui, nasikia tu zinagawiwa na Mwanakijiji, sasa sijui kaanzisha chama chake nini?
 
Rangi ni Title kama Senior ama expert now hizi rangi ni Title mpya . Kaza mwendo utafikia . Ila mimi nitaomba ikfika zamu yangu nisiwepewe njano ama kijani tafadhali .

Mwelekeo wa dakika 30 nilishindwa kumalizia sijajua zimeishaje .Ila nadhani kanuni hii haitakuwa na maana kwa kuwa Wapinzani wanatafutiwa kona ya kubanwa kwa uzushi ama uongo .
 
Huu ni usanii mwingine,hapa watu wanataka kumlinda tu huyu PM. Iweje umlete mtu kuulizwa maswali halafu uanze kuchagua aina ya maswali ya kumuuliza,liwe swali la kizushi au la kusikia,siye twataka sikia majibu ya serikali atii. halafu huo muda wa dakika 30,jamani hebu tuache uongo na usanii,Mbunge wa CCM kabla hajauliza swali,anaanza kumpongeza JK kwa kumfukuza Balali mpaka aje kuuliza swali 15 minutes zimekwisha. Ama kweli siasa za usanii bongo zimezidi
 
Ndiyo Linyungu, Hapa watu wanatafuta jinsi ya kuwabana akina Zitto na Slaa wasiletee habari hot ambazo zitamfanya PM afumbe mdomo
 
Nina hamu ya kuona jinsi mfumo huu mpya utakavyofanya kazi.

KAMA WAZIRI MKUU ATAENDELEA KUWA HUYU el KWA KWELI AKAJIBU KWANZA LILE SWALI LA MWANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA KULE UKERERWE NDIPO AJE BUNGENI LA SIVYO .......
 
Me pia naona ni maigizo tu mengine kama tulivyozoea kuyaona mengine hakuna jipya hapa kutoka chama cha mafisadi.

Dkk 30 ni ndogo sana na hiki kiswahili chetu kirefu huu muda ni kututania tu huku na si kingine. Nadhani issue kama ilivyosemwa hapo juu ni kuwaplease wafadhili ili waendelee kutoa pesa na wao mafisadi waendelee kuzifisadi kwa kwenda mbele.

Pia me nahofu wabunge wa ccm watakuwa wanampa maswali mapema huyo fisadi el ili ayajibu kwa ufasaa ili kumsafishia njia ya ikulu mtaalamu wa performing art (mamvi)
 
Bi Anna Makinda yuko hwani anasoma kanuni mpya ya kumweka Waziri mkuu kitomoto lakini naona wanajenga hoja ya kumlinda ipasavyo. Wanasema maswali binafsi hayatakiwi ,maswali ya kusikia hayatakiwi maswali ya uzushi hayatakiwi sasa sijui watakuwa wanamuuliza nini . Huu mtego sasa .Karibuni Dodoma Makinda bado analeta mipango yao .Kila Alhamisi Mamvi atakuwa hewani kwa dakuka 30 akilambwa maswali .Naendelea kusikiliza toka hapa Dodoma .

Yaani dk 30! Huu ni Utani mwingine! Anyway, hata kama hawajui, itatusaidia WaTz tuone how unserious are our leaders.

Nadhani ingekuwa busara kutoa kipindi chote cha asubuhi kwa maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu lakini kwa dk 30 ni utani. Spika atampa mbunge gani nafasi ya kuuliza na amwache nani? Kwa Wabunge wengi itakuwa ni nafasi ya kuuliza maswali ya kujipendekeza na kumjengea umaarufu Lowasa, I tell you. Si mtaona?
 
Bunge lina wabunge 320 sasa fahesabu ni uwa vikao vya bunge vinakaa siku ngapi kwa mwaka na je kama mkuna uwezekano wa kuuliza hayo maswali si ajabu wakauliza wale anaowataka spika tuu na wengine kuambiwa nafasi hakuna.
 
Back
Top Bottom