Yanayo endelea kwenye siasa za hapa nchini nimepigia mstari hakuna mwenye uchungu na kodi zetu.!

Half Genious

JF-Expert Member
Feb 28, 2017
491
784
Binafsi hama hama ya wanasiasa haswa upepo mbaya ukiwa unaelekea upinzani kwa wanasiasa wao wengi kuhamia CCM na wote wana maelezo ya aina moja kumuunga mkono Rais... Tulishapata harufu ya rushwa Arusha juu ya hii hama hama ikazimwa kama taa na hawa wengine wanaendelea kwa mtindo ule ule.

Lakini swala la rushwa ni swala la kificho au kuahidiwa madaraka hiyo ni siri yao na mwisho wa siku ni uhuru wa mtu na demokrasia ukiacha makando kando....nimestuka jana mbunge kujiuzulu na kujiunga na chama kingine naogopa wabunge wangapi watafata siogopi wao kuhama i dont care ILA VIP KUHUSU KODI ZETU KWENYE CHAGUZI ZA MARUDIO BILA SABABU ZA MSINGI?

Wanaosuka hii mipango wanafikiria kweli juzi nimeona Tanga sehemu inaitwa Bombo, kuna shule moja ya miti wamejenga wananchi ina darasa moja na wanachanga kumlipa mwalimu huku watu hawajali kabisa...kodi zetu kodi zetu...kila wizara inashindwa kutekeleza miradi wanalia ufinyu wa bajeti..hakuna nia ya dhati.!
 
Rushwa ni adui wa haki sitatoa wala kupokea rushwa.hii ilikuwa tanu na ccm akina mwalimu sio hii ya sasa.
 
ipo hivi huu Mladi wa kuwanunua Wapinzani ni Mladi wa Madalali wa Siasa Wajanja wachache wakiongozwa na Maliyamungu Bashite, Lipumba, Le mutuz na Jerry muro ni Ufisadi wa kisayansi sana, Pesa ya kuwanunua Wapinzani inatoka Hazina kwa Doto ni pesa za walipa kodi pia, pesa za kurudia uchaguzi ni pesa za walipa kodi, pesa zote ni za walipa kodi, lakini Madalali wa Siasa wanakula cha juu 10% wao hawajali kama mtu ana mapenzi na CCM au nini wao kazi yao ni kuwanunua kisha wanawafundisha waseme Lugha moja ya kumuunga mkono Mtukufu Rais na wao kupata 10% yao matokeo ya Rohoni huko mbeleni hawajali wala kutaka kujua athari zake, pesa mbele kwanza mengine baadae, Pesa inayotumika kwa mambo ya hovyo hovyo kwa sasa ni pesa ambazo zingeweza kuleta maendeleo na wananchi wakawapigia kura CCM pasipo kuwanunua Wapinzani kuwakomoa kuwadhalilisha kuwadhoofisha, Maendeleo ya CCM yenyewe yangeweza kuwashawishi wananchi kuwachagua pasipo kutumia mbinu za uchakachuaji wizi wa kura kamata kamata wakala wa upinzani na wagombea, Watanzania wa sasa si wajinga wanajua kuwa Maliyamungu Bashite Lipumba na kikundi chao wanakula pesa zao kwa njia Haramu wanaendelea kumuomba Mungu awape maarifa ifike siku wajinasue na hayo mafisadi ya kijanja yalioyoanza kula pesa za Umma kwa mgongo wa kuwanunua Wapinzani.
 
Kufa kufaana Wapinzani wanunuliwa lakini akina Le mutuz wanashiba pasipo kujali matokeo ya baadae huko mbeleni
 
Awamu hii imetupatia funzo kuwa kabla ya kuwapigia kura liwepo sharti la kupimwa afya ya akili, kwani kwa haya yanayo endelea yanaleta kaukakasi flani hivi juu ya afya zao za akili.
 
kwa kweli ni ngumu kuelewa wakati dunia yote inaenda mbele na kuzunguka kwenye muhimili wake Tanzania pekee inazidi kurudi kinyume nyume na muda mwingine kusimama kwa muda bila sababu za msingi. Nadhani Tanzania ina mpango wa kujitoa duniani ili ijitenge ipate nafasi ya kumuunga mkono JPM na juhudi zake

Hii ndio Tanzania na watu wake na viongozi wake na mali zake.
 
Pesa iliyopotelea kwenye siasa za maji taka ingeweza kujenga Hosptal za rufaa kila mkoa na kuajiri madaktari toka India
 
Awamu hii imetupatia funzo kuwa kabla ya kuwapigia kura liwepo sharti la kupimwa afya ya akili, kwani kwa haya yanayo endelea yanaleta kaukakasi flani hivi juu ya afya zao za akili.
Mkuu hapa tatizo wala si afya ya akili, fikiria mbunge pamoja na maslahi yote anayopata anaammu kuacha nafasi yake bila kujali gharama, muda na pengine hata maumivu kwa baadhi ya watu eti kwa kumuunga mkono raisi.
Maamuzi haya hata asiye na akili kabisa hawezi kuwa nayo. Hapa kuna namna inafanyika, ila kwa vyovyote vile huyu mbunge atakuwa ni zaidi ya mgonjwa wa akili, Sijui! labda amepewa nini mpaka kufikia maamuzi yale
 
Hela alizo okoa kwenye kuminya safari za nje anazitapanya kununua wapinzani.
2025 atakuja Rais mwingine ataliweka wazi hili
 
Hivi huwezi kuunga juhudi za rais ukabaki huko huko uliko? Mbona Lyatonga na Cheyo wanamuunga mkono rais na wapo kwenye vyama vyao!
 
Back
Top Bottom