kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,408
- 7,190
Kuna hofu kwa raia wazalendo kwamba kuachiwa na dpp watuhimiwa wa ufisadi kunakotokea sasa bila kuhusishwa mahakama huenda kukapelekea madai ya mabilioni toka hazina kuu ya taifa.
Tuhuma kuhusiana na IPTL ya harbinder sighn na rugemalila ziliwekwa wazi. Tangu wahujumu hao kutupwa lupango tanesco ilitulia na matumizi na utendaji wa shirika lililokua linatoa mabilioni kwa hila ukaboreka.
Wananchi wangependa kujua kama rugemalira ameonekana hana hatia au ameachiwa vipi. Mfanyabiashara mkubwa hivyo kumzuia lupango miaka minne bila kosa gharama yake akidai hakika ni mabilioni. Umma tuliyoamini ni fisadi tuelezwe kama kuna maafikiano ya kuachiwa. Kama ni ubinadamu tu au amerejesha thamani aliyofisidi tujue.
Isije ikawa awamu ya 6 inatengeneza mazingira ya fisadi waliyoshughulikiwa awamu ya 5 kuweza kufisidi tena umma kwa kudai fidia serikali baada ya kuachiwa. Tumeona pia waziri wa nishati akibadilishwa isije kua maandalizi ya kutia chumvi juu ya kidonda.