Nucky Thompson
JF-Expert Member
- Sep 20, 2016
- 1,817
- 4,059
Baada ya tetesi za kutokuwa na maelewano mazuri ndani ya kundi la Yamoto Band kwa muda yaliyosababisha kutoachia kazi mpya, mmoja ya wasanii wanaounda kundi hilo Enock Bella amefunguka na kudai kwa sasa mambo yapo sawa.
Akiongea na kipindi cha E News cha EATV, Enock amesema japo kulikuwa na kutoelewana kati ya uongozi unaowasimamia na wao wasanii lakini kwa sasa wapo sawa na amemtaja Said Fella ndio mwenye uwezo wa kuwapoteza kwenye ramani ya muziki kwa kuwa yeye ndio aliyewatoa.
“Unajua hapo awali kidogo ni kweli tulikuwa na mvurugano kidogo kati ya wasanii na uongozi lakini sasa hivi hakuna tofauti yoyote ile na kila kitu kipo sawa kabisa, na upendo uleule na siyo kuvurugana,” amesema Enock.
wasanii walikuwa hawataki au kugombana kabisa, kwa sababu Mkubwa yeye ndiye aliyetuleta na yeye ndiye atakayetupoteza. Saidi Fella ni mzee wetu hivyo huwezi kusikia hata siku moja kuwa Yamoto Band wamegombana na Fella,” ameongeza.