Yamkini hali si shwari Pemba, Askofu asema nyumba zapigwa 'X'

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,001
9,862
Viongozi wa dini Unguja, Pemba wamelaani tukio lilitokea Septemba 22 ktk msikiti mmoja huko Pemba ambapo watu watatu walishambuliwa kwa panga

Viongozi wa dini kutoka Zanzibar wako mubashara wakitoa tamko la amani wakati wa kampeni na uchaguzi, katika jambo alilozingumzia baba askofu amesema nyumba kadhaa zimechorwa 'X' na huku wakiwa hawajui inamaanisha nini, kama wanatafutwa na hao wahalifu au watafanyiwa nini. Hii ni siku moja baada ya jana alfajiri watu kupigwa mapanga.

Baba Paroko kasema wao kama wakuu wa dini watawaombea wanaodhani wanaweza kufanya lolote wanalotaka kinyume cha matakwa ya Mungu.

Pia, soma=> Pemba: Vyama sita vya siasa vyalaani vurugu za Alfajiri ya leo, waomba msaada wa IGP baada ya wananchi kukatwa mapanga
 
Nasisitiza tu viongozi wadini waikumbushe Serikali pamoja na vyombo vyake vyadola waangalie wapi ambapo hawakutenda haki, kisha baada yahapo warekebishe kama papo.

Hakiii
Hakii
Hakii
Penye haki hutamalaki amani.
 
Ni watu wachache tu wenye nia mbaya na nchi yetu ndio wanaotaka kutuletea vurugu. In sha Allah watashindwa.
 
Wanakutana kwa kongamano la amani badala ya kongamano la haki.....?

Huu uzwazwa ndio siupendi kabisa..... Wkt haki zinakiukwa wao walikua wapi kukemea na kulaani?
 
Viongozi wa dini Unguja, Pemba wamelaani tukio lilitokea Septemba 22 ktk msikiti mmoja huko Pemba ambapo watu watatu walishambuliwa kwa panga

Viongozi wa dini kutoka Zanzibar wako mubashara wakitoa tamko la amani wakati wa kampeni na uchaguzi, katika jambo alilozingumzia baba askofu amesema nyumba kadhaa zimechorwa 'X' na huku wakiwa hawajui inamaanisha nini, kama wanatafutwa na hao wahalifu au watafanyiwa nini. Hii ni siku moja baada ya jana alfajiri watu kupigwa mapanga.

Baba Paroko kasema wao kama wakuu wa dini watawaombea wanaodhani wanaweza kufanya lolote wanalotaka kinyume cha matakwa ya Mungu.

Pia, soma=> Pemba: Vyama sita vya siasa vyalaani vurugu za Alfajiri ya leo, waomba msaada wa IGP baada ya wananchi kukatwa mapanga
Washenzi hao wakamatwe na kupewa kibano kama Magaidi wa Uamsho ama wamaliziwe huko huko field kama magaidi wa Mkuranga, Kibiti & Rufiji
 
Walaaniwe viongozi wa dini wanaoombea amani badala ya kukemea na kulaani vitendo vya uvunjifu wa HAKI vinavyofanywa na serikali hii ya kishetani
 
Sasa CCM inahusikaje ? Kwa nini hautaji vyama kama ACT na Chadema kutokana na kauli za wagombea wao au viongozi wao ?

CCM wanatafuta vita kwa hali na mali ila Mungu hayupo upande wao!
 
Attachments

  • IMG_20200923_170441.png
    IMG_20200923_170441.png
    111.9 KB · Views: 1
Back
Top Bottom