Yametimia: TANESCO yakiri uhaba wa umeme. Kutoa 'Taarifa' watu wapange kazi zao

Saguda47

JF-Expert Member
May 1, 2016
9,514
2,000
Hivi huyu mama anayeitwa Rais Samia Suluhu Hassan sijui mpaka sasa anaendelea kufanya nini ofisini kama anaruhusu hizi hujuma dhidi ya wananchi wa Tanzania kufanyika mchana kwwupe kiasi hiki....??

Eti upungufu wa maji kwenye mabwawa yetu. HII SIYO KWELI...!!!

Kwa sàbàbu msimu uliopita wa 2020/2021 ulikuwa na mvua nyingi kiasi cha maji kuzidi kiwango kinachotakiwa hata kuwa mafuriko. Na msimu wa mvua ndo tu uliishilizia mwezi Juni, 2021. Leo iweje wanatoa kisingizio cha maji....?

HAPANA. Hizi ni hujuma!!

Huyu mama hafai kuwa Rais na anatakiwa atolewe ofisini hata leo ili nchi hii apewe mtu anayeijua vyema...

Katika hili Hayati Mwendazake John P. Magufuli alikuwa mzuri sana. Pamoja na mapungufu yake katika maswala ya haki za binadamu, demokrasia na utawala bora, lakini ktk usimamizi wa uwajibikaji na utendaji serikali alikuwa safi kabisa...

Katika miaka ya u- Rais wake wa karibu miaka 6 hakukuwahi kuwa na mgawo wa umeme na hali ya hewa ni hii hii haikuwahi kuwa tofauti...

Leo miezi sita baada ya kifo chake na kuingia huyu mama asiye na mbele wala nyuma, anatangaza ujinga huu. Why..???

Hii maana yake, kuna kikundi cha watu wanataka kutengeneza tatizo la upungufu wa umeme ili kupiga hela na wakati huohuo kuihujumu nchi na wananchi na yeye mwenyewe Rais, wakati huo huo wakimpangia ziara zisizo na tija kuzunguka zunguka tu duniani aimlessly ili huku nyuma kundi hili lifanye litakavyo...

Kwanini tatizo hili la umeme limeshika kasi Mara baada ya aliyekuwa waziri Wa nishati Medard Kalemani kutimuliwa na kumpisha January Makamba...????

By the way, Jenerali Ulimwengu was right kumbe. Alisema wazi, HUYU MAMA HAIJUI NCHI HII, HATAIWEZA...!

Look now, here we are. Taratibu maneno haya yanaanza kuthibitika....

Huyu Mzanzibar aondoke, arudi kwao. Atuachie nchi yetu ya Tanganyika!!!!!
Yaani mkuu taabu sana, huyu hana uchungu na taifa.
 

Wakabambee58

Senior Member
Aug 14, 2020
114
250
Duh!, Haya maji yalisubiri Magufuri kutoweka ndio yameanza kupungua?.

Kwa nini tangu tupate uhuru hadi karne hii bado tunategemea mito tu, kwanini tusianze kufikiria uzalishaji wa umeme wa upepo kule kwenye Mkoa kama Singida?, Au sehemu zenye Milima?.. Halafu ile gesi toka Mtwara imeishia wapi?.

Nawashauri mnapoanza kukata umeme kila Mkoa msisahau kufanya biashara zenu za kuuza Majenereta maana kwa sasa ni kama vile ufisadi umeanza kurudi.

JPM alikuwa na mapungufu yake mengi, ila kuna mahali alifanya vizuri.
Umeme wa upepo? Hujui kilichotokea miaka kama Sita au saba nyuma juu ya project hiyo. Wachina walitoka Ethiopia hadi hapa katikati mabosi wakaanza paruana kila mmoja anapendekeza joint venture na Hao Wachina. Big man akaona isiwe taabu futilia kwa mbali mradi wenyewe
 

sikwedawaz

Senior Member
Aug 11, 2018
105
225
😂Mambo ya "Hydroelectric power".....sisimizi kameza msumari 📌🐜

💪[Geothermal,nuclear,natural gas,wind mill]👍
 

Masanja

JF-Expert Member
Aug 1, 2007
4,457
2,000
Nadhani hatimae watu ndo wataelewa...

It's just last week nimehoji mara kadhaa hapa, kama sio 57% ya umeme unaotokana na gesi, nchi ingekuwa katika hali gani wakati umeme wa maji ni ONLY around 36%?!

Kiukame kidogo tu, tushaanza kutafutana...

Huku Misukule ikikazana kwamba, kwavile kuna Bwawa la Nyerere linajengwa basi ku-explore vyanzo vingine vya umeme ni kutaka kumhujumu JPM ili ionekane Mradi wa Bwawa la Nyerere haufai!!

Tuna taifa lenye viumbe wa ajabu sana...

Watanzania wengi tunapenda kuambiwa hadithi. Ukweli ni kwamba JPM angeruhusu vyombo vya habari kuandika hali halisi......tungetafutana kwenye giza.

Ukiishi kwenye jamii yoyote inayopenda kufanya mambo kwenye giza, ndo matokeo yake. Hata sasa hivi mambo mengi yanafanyika gizani na sisi wananchi tunashangilia. siku yakianza kututafuna sijui tutamlaumu nani.

Nuru na giza havichangamani.
 

Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
12,717
2,000
Watanzania wengi tunapenda kuambiwa hadithi. Ukweli ni kwamba JPM angeruhusu vyombo vya habari kuandika hali halisi......tungetafutana kwenye giza.

Ukiishi kwenye jamii yoyote inayopenda kufanya mambo kwenye giza, ndo matokeo yake. Hata sasa hivi mambo mengi yanafanyika gizani na sisi wananchi tunashangilia. siku yakianza kututafuna sijui tutamlaumu nani.

Nuru na giza havichangamani.
Na serikali za CCM zina-take advantage ya taifa kuwa na wajinga wengi kuliko werevu...

Wajinga hawa wakawa wamekaa mkao wa kula kumeza kila wanachoambiwa...
 

Masanja

JF-Expert Member
Aug 1, 2007
4,457
2,000
Na serikali za CCM zina-take advantage ya taifa kuwa na wajinga wengi kuliko werevu...

Wajinga hawa wakawa wamekaa mkao wa kula kumeza kila wanachoambiwa...

Leo GoV ya Tz inatwambia tuna mgao wa umeme kwa sababu ya kupungua kwa vyanzo vya maji. Lakini hao hao wakubwa wanatwambia kwamba tunajenga Stigler's ya kutupa umeme wa MG 2000+, sasa unajiuliza hayo maji yatatoka mbinguni au wapi? au yenyewe hayataathirika na ukame?

Ni ngumu sana kuwaelewa wanasiasa!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom